Add parallel Print Page Options

Kristo aliwakaribisha ninyi, hivyo nanyi mkaribishane ninyi kwa ninyi. Hili litaleta heshima[a] kwa Mungu. Ndiyo, haya ndiyo maneno yangu kwenu kwamba Kristo alifanyika mtumishi wa Wayahudi ili kuonesha kuwa Mungu amefanya yale aliyowaahidi baba zao wakuu. Na pia alifanya hivi ili wale wasio Wayahudi waweze kumsifu Mungu kwa rehema anazowapa. Maandiko yanasema,

“Hivyo nitakushukuru wewe katikati ya watu wa mataifa mengine;
    Nitaliimbia sifa jina lako.”(A)

Read full chapter

Footnotes

  1. 15:7 heshima Au “utukufu”. Tazama Utukufu katika Orodha ya Maneno.