Add parallel Print Page Options

20 Kwa sababu kufuata sheria hakumfanyi mtu akahesabiwa haki mbele za Mungu.[a] Sheria inatuonyesha dhambi zetu tu.

Mungu Anavyowafanya Watu Kuwa Wenye Haki

21 Lakini sasa Mungu ametuonesha jinsi alivyo mwema na mwaminifu. Alivyofanya haihusiani na sheria ingawa sheria na manabii walisema kuwa haya yangetokea. 22 Uaminifu wa wema wa Mungu umedhihirishwa kwetu kupitia imani katika[b] Yesu Kristo. Hufanya hivi kwa wote wanaomwamini Kristo. Kwa sababu kwa Mungu watu wote ni sawa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:20 Tazama Zab 143:2.
  2. 3:22 imani katika Au “uaminifu wa”.