Lakini iwapo uovu wetu unadhihirisha wazi kwamba Mungu ni mwenye haki, tusemeje basi? Je, tuseme kuwa Mungu hana haki kutuadhibu? Hapa ninasema kibinadamu. La hasha! Mun gu ana haki kabisa kutughadhibikia! Kama sivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? Mtu anaweza kusema,“Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?”

Read full chapter