10 na tajiri afurahi anaposhushwa kwa maana atatoweka kama ua la mwituni. 11 Maana jua huchomoza na kwa mionzi yake mikali hukausha mimea, na maua yake huanguka na uzuri wake hupotea. Vivyo hivyo tajiri naye atafifia akiwa katika shughuli zake.

Kujaribiwa

12 Amebarikiwa mtu ambaye anavumilia majaribu, kwa sababu akisha stahimili atapewa taji ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao.

Read full chapter