11 Maana jua huchomoza na kwa mionzi yake mikali hukausha mimea, na maua yake huanguka na uzuri wake hupotea. Vivyo hivyo tajiri naye atafifia akiwa katika shughuli zake.

Kujaribiwa

12 Amebarikiwa mtu ambaye anavumilia majaribu, kwa sababu akisha stahimili atapewa taji ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao. 13 Mtu akijaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu,” kwa maana Mungu hajaribiwi na uovu na yeye hamjaribu mtu ye yote.

Read full chapter