17 Kila kipawa chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni, ikishuka kutoka kwa Baba wa nuru za mbinguni ambaye habadiliki kama kivuli. 18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mavuno ya kwanza katika viumbe vyake.

Kusikia Na Kutenda

19 Ndugu wapendwa, fahamuni jambo hili: kila mtu awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema wala kukasirika.

Read full chapter