Onyo Kuhusu Upendeleo

Ndugu zangu wapendwa, msiwe na upendeleo mnapoishika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu. Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,”

Read full chapter