Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,” je, hamtakuwa mmefanya ubaguzi mioyoni mwenu na kutoa hukumu itokanayo na mawazo maovu?

Read full chapter