je, hamtakuwa mmefanya ubaguzi mioyoni mwenu na kutoa hukumu itokanayo na mawazo maovu?

Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa: je, Mungu hakuwachagua wale walio fukara hapa duniani kuwa matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidi wale wampendao? Lakini ninyi mmemvunjia heshima aliye fukara. Je, si matajiri ndio wanaowagandamiza na kuwapelekeni mahakamani?

Read full chapter