Add parallel Print Page Options

Viongozi wa Kiyahudi Wasimama Kinyume na Yesu

22 Ulikuwa ni wakati wa baridi, na wakati wa Sikukuu ya Kuweka Wakfu[a] kule Yerusalemu. 23 Yesu alikuwa katika eneo la Hekalu katika Ukumbi wa Sulemani. 24 Viongozi wa Kiyahudi wakakusanyika kumzunguka. Wakasema, “Ni mpaka lini utatuacha na mashaka juu yako? Kama wewe ndiwe Masihi, basi tuambie wazi wazi.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 10:22 Sikukuu ya Kuweka Wakfu Hanukkah, au “Siku Kuu ya Mianga”, ni juma maalumu mwezi wa Disemba lililoadhimisha majira ya mwaka 165 KK wakati Hekalu la Yerusalem lilipotakaswa na kuwa tayari tena kwa ibada ya Wayahudi. Kabla ya hapo lilikuwa chini ya udhibiti wa jeshi la kigeni la Kiyunani na lilitumiwa kwa ibada za kipagani.