Add parallel Print Page Options

10 Vyote nilivyo navyo ni vyako, na vyote ulivyo navyo ni vyangu. Kisha utukufu wangu umeonekana ndani yao.

11 Sasa nakuja kwako. Mimi sitakaa ulimwenguni, lakini hawa wafuasi wangu bado wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu, uwaweke hao salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Ndipo watapokuwa na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo. 12 Nilipokuwa pamoja nao niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Niliwalinda. Ni mmoja wao tu aliyepotea; yule ambaye kwa hakika angelikuja kupotea. Hii ilikuwa hivyo ili kuonesha ukweli wa yale yaliyosemwa na Maandiko kuwa yangetokea.

Read full chapter