11 Mimi naondoka ulimwenguni ninakuja kwako. Lakini wao wako ulimwenguni. Baba Mtakatifu, walinde kwa jina lako ambalo umenipa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo mmoja. 12 Nilipokuwa pamoja nao niliwalinda wakawa salama kwa uwezo wa jina ulilonipa. Nimewalinda na hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyeamua kupotea, ili Maandiko yapate kutimia. 13 Lakini sasa nakuja kwako na ninasema haya wakati nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kikamil ifu.

Read full chapter