12 Nilipokuwa pamoja nao niliwalinda wakawa salama kwa uwezo wa jina ulilonipa. Nimewalinda na hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyeamua kupotea, ili Maandiko yapate kutimia. 13 Lakini sasa nakuja kwako na ninasema haya wakati nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kikamil ifu. 14 Nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao, kama mimi, si wa ulimwengu huu.

Read full chapter