23 mimi nikiwa ndani yao na wewe ndani yangu; ili wakamilike katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma na kwamba unawapenda kama unavyonipenda mimi. 24 Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa. 25 Baba Mtakatifu, ijapokuwa ulimwengu haukufahamu wewe, mimi ninakufahamu, na hawa wanajua ya kuwa umenituma.

Read full chapter