Yesu Akamatwa

18 Baada ya sala hii Yesu aliondoka na wanafunzi wake waka vuka kijito cha Kidroni wakaingia katika bustani iliyokuwa upande wa pili. Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, pia alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake hapo mara kwa mara. Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha.

Read full chapter