Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, pia alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake hapo mara kwa mara. Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha. Yesu alijua yata kayompata, kwa hiyo akawasogelea akawauliza, “Mnamtafuta nani?”

Read full chapter