Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha. Yesu alijua yata kayompata, kwa hiyo akawasogelea akawauliza, “Mnamtafuta nani?” Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawaambia, “Ni mimi.” Yuda ambaye alimsaliti alikuwa amesimama na wale askari.

Read full chapter