Add parallel Print Page Options

Kwa hiyo Yuda akaongoza kundi la askari hadi katika bustani hiyo pamoja na walinzi wengine kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Hawa walikuwa wamebeba mienge, taa, na silaha.

Yesu alikwisha kujua yote ambayo yangempata. Hivyo aliwaendea na kuwauliza, “Je, ni nani mnayemtafuta?”

Wakamjibu, “Yesu kutoka Nazareti.”

Akawaambia, “Mimi ni Yesu.”[a] (Yuda yule aliyehusika kumsaliti Yesu alikuwa amesimama hapo pamoja nao.)

Read full chapter

Footnotes

  1. 18:5 Mimi ni Yesu Kwa maana ya kawaida, “Mimi ndimi”, ambayo inaweza kuwa na maana ile ile hapa kama ilivyo katika 8:24,28,58; 13:19. Pia katika mstari wa 8.