Alisema haya ili lile neno alilosema lipate kutimia, ‘Kati ya wale ulionipa sikupoteza hata mmoja.’ 10 Ndipo Simoni Petro akachomoa upanga aliokuwa amechukua akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo lilikuwa Malko. 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?”

Read full chapter