10 Wale wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.

Yesu Anamtokea Mariamu

11 Lakini Mariamu akakaa nje ya kaburi akilia. Na alipokuwa akilia akainama kutazama mle kaburini. 12 Akaona malaika wawili wamevaa nguo nyeupe, wamekaa pale mwili wa Yesu ulipokuwa, mmoja upande wa miguuni na mwingine upande wa kichwani!

Read full chapter