Add parallel Print Page Options

13 Malaika wakamwuliza Mariamu, “Mwanamke, kwa nini unalia?”

Mariamu akajibu, “Wameuondoa mwili wa Bwana wangu, na sijui wameuweka wapi.” 14 Wakati Mariamu aliposema hivi, akageuka nyuma na kumwona Yesu amesimama pale. Lakini hakujua kuwa huyo alikuwa ni Yesu.

15 Akamwuliza, “Mwanamke, kwa nini unalia? Je, unamtafuta nani?”

Yeye alifikiri kuwa huyu alikuwa ni mtunzaji wa bustani. Hivyo akamwambia, “Je, ulimwondoa Bwana? Niambie umemweka wapi. Nami nitaenda kumchukua.”

Read full chapter