17 Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”

Yesu Anawatokea Wanafunzi Wake

19 Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.”

Read full chapter