18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”

Yesu Anawatokea Wanafunzi Wake

19 Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana!

Read full chapter