Font Size
Yohana 20:24-26
Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 20:24-26
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Anamtokea Tomaso
24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”
26 Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani iwe nanyi.”
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica