Yesu Ajitambulisha Kwa Wanafunzi Saba

21 Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote.

Read full chapter