11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia.

Read full chapter