Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.

Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate.

Read full chapter