Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.

Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.”

Read full chapter