Aliyetoka Mbinguni

31 “Yeye aliyekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. Anayetoka duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya hapa duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya watu wote. 32 Anayashuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia lakini hakuna anayekubali maneno yake. 33 Lakini ye yote anayekubali maneno yake, anathibitisha kwamba aliyosema Mungu ni kweli.

Read full chapter