12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

13 Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 14 Lakini ye yote atakayekunywa maji nitakay ompa mimi, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa kama chemchemi itakayobubujika maji yenye uhai na kumpa uzima wa milele.”

Read full chapter