38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma. 39 Na mapenzi yake yeye aliyenituma ni haya: kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa bali niwafufue wote siku ya mwisho. 40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni haya: wote wamwonao Mwana na kumwamini wawe na uzima wa milele. Nami nitawafufua siku ya mwisho.”

Read full chapter