10 Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakush taki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?” 11 Yule mwa namke akajibu, “Hakuna Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”]

Yesu Ni Nuru Ya Ulimwengu

12 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.”

Read full chapter