Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe wanawake waliokamatwa wakizini, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” Walim wuliza hivi kwa kumtega, kusudi wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini akaanza kuandika kwa kidole chake mavumbini.

Read full chapter