Hii ni kwa sababu watu wasiomcha Mungu ambao tangu zamani wamekwisha kuandikiwa hukumu hii, wamejiingiza miongoni mwenu kwa siri. Hawa ni watu ambao wanapotosha neema ya Mungu wetu na kuitumia kama kisingizio cha kutenda maovu. Wao wanamkana Yesu Kristo ambaye pekee ndiye Mkuu na Bwana wetu.

Sasa nataka kuwakumbusha jambo ambalo tayari mnalijua: kwamba, Bwana aliwaokoa watu wake kutoka Misri, lakini baadaye akawaangamiza wale ambao hawakuamini. Na malaika ambao hawaku tunza madaraka yao wakaacha maskani yao halisi; hao amewafungia gizani kwa minyororo ya milele hadi wahukumiwe katika siku ile kuu.

Read full chapter