Bible in 90 Days
Yesu Ashtakiwa Mbele Ya Baraza
57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekutanika.
58 Lakini Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu akaingia ndani pamoja na walinzi aone litakalotokea. 59 Basi makuhani wakuu na baraza zima wakatafuta ushahidi wa uongo ili wamwue Yesu, 60 lakini hawakupata, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza watu wawili, 61 wakasema: “Huyu mtu alisema, ‘Nina uwezo wa kuvunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena katika muda wa siku tatu .’ ”
62 Kisha kuhani mkuu akasimama, akamwambia Yesu, “Huna jibu? Husikii huo ushahidi waliotoa watu hao?” 63 Lakini Yesu hakusema neno. Basi kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa jina la Mungu aliye hai, tuambie kama wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.”
Mungu.”
64 Yesu akajibu, “Umetamka mwenyewe. Lakini nina waambieni nyote kwamba baada ya hapa, mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa Mungu mwenye uweza na akija juu ya mawingu ya mbin guni.”
65 Aliposikia maneno hayo, kuhani mkuu alirarua mavazi yake akasema, “Amekufuru! Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Si mmemsi kia akikufuru? 66 Mnaamuaje?” Wakajibu, “Anastahili kufa!”
67 Kisha wakamtemea mate usoni; wengine wakampiga ngumi na makofi, 68 wakasema, “Hebu toa unabii wewe Kristo! Ni nani ame kupiga?”
69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui usemalo.”
71 Kisha alipotoka nje, mlangoni mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwapo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Simfa hamu mtu huyo!” 73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesi mama pale walimwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao kwa maana namna yako ya kusema ni kama yao.” 74 Ndipo Petro akalaani na kuapa, akawaambia, “Simfahamu mtu huyo!” Wakati huo huo jogoo akawika. 75 Na Petro akakumbuka Yesu alivyomwambia, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.” Akaenda nje, akalia kwa uchungu.
Yesu Apelekwa Kwa Pilato
27 Asubuhi na mapema, makuhani wakuu wote na wazee walifanya mkutano, wakashauriana jinsi ya kumwua. 2 Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato ambaye alikuwa gavana.
Majuto Ya Yuda
3 Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehuku miwa alijuta. Akazirudisha zile fedha alizopewa kwa makuhani wakuu na wazee 4 akawaambia, “Nimetenda dhambi kwa maana nimem saliti mtu asiye na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
5 Basi Yuda akazitupa zile fedha Hekaluni, akaondoka; akaenda akajinyonga.
6 Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” 7 Kwa hiyo baada ya kujadiliana waliamua kuzitumia kununua shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. 8 Kwa hiyo shamba hili limeitwa ‘Shamba la damu’ hadi leo. 9 Ndipo yakatimia yale aliyonena nabii Yeremia kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na wana wa Israeli, 10 wakanunulia shamba la mfinyanzi kama Bwana alivyon iagiza.”
Yesu Mbele Ya Pilato
11 Yesu akapelekwa mbele ya gavana naye akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Hayo umetamka wewe.” 12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipomshtaki kwa mambo mengi hakujibu neno. 13 Ndipo Pilato akamwuliza, “Husikii mambo hayo yote wanayokushtaki nayo?” 14 Lakini Yesu hakujibu neno hata kwa shtaka moja. Gavana akashangaa sana.
15 Kila wakati wa sikukuu, gavana alikuwa na desturi ya kum fungua mfungwa mmoja atakayechaguliwa na watu. 16 Wakati huo alikuwapo mfungwa mmoja mwenye kujulikana sana, aliyeitwa Baraba. 17 Basi watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwa fungulie nani; Baraba au Yesu aitwaye Kristo?” 18 Kwa sababu alijua kuwa Yesu aliletwa kwake kwa ajili ya wivu wa viongozi wa Wayahudi. 19 Alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mke wake alimpelekea ujumbe, “Usijihusishe katika kesi ya huyu mtu asiye na hatia. Leo nimehangaika sana katika ndoto kwa ajili yake.”
20 Basi makuhani na wazee wakawashawishi umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe. 21 Gavana akawau liza tena , “Ni yupi mnataka niwafungulie?” Wakajibu, “Bar aba!” 22 “Sasa nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote , “Asulubiwe!” 23 Akasema, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Asulubiwe.”
24 Pilato alipoona kwamba hakuna zaidi ambalo angeweza kufa nya na kwamba ghasia ilikuwa ikianza, akachukua maji, akanawa mikono mbele yao, akasema, “Sina hatia na damu ya mtu huyu. Jambo hili ni juu yenu.”
Jambo hili ni juu yenu.”
25 Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
26 Basi akawafungulia Baraba, na baada ya kuamuru Yesu apigwe viboko, akamtoa asulubiwe.
Askari Wamdhihaki Yesu
27 Kisha askari wa gavana wakampeleka Yesu kwenye makao makuu ya gavana wakakusanya kikosi cha askari, wakamzunguka Yesu.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu ya rangi nyekundu. 29 Wakasokota taji ya miiba wakamvika kichwani. Wakamwekea fimbo mkono wake wa kulia, wakapiga magoti mbele zake wakamdhihaki wakisema, “Uishi maisha marefu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga nayo kich wani. 31 Baada ya kumdhihaki, walimvua ile kanzu, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka kumsulubisha.
Yesu Asulubishwa
32 Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakambebesha ule msalaba kwa nguvu. 33 Na wali pofika sehemu iitwayo Golgotha, maana yake mahali pa Fuvu la Kichwa, 34 wakampa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini baada ya kuionja, akaikataa.
35 Walipokwisha kumsulubisha wakagawana nguo zake kwa kuzi pigia kura. 36 Kisha wakaketi, wakamchunga. 37 Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.’ 38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja kulia kwake na mwingine kushoto kwake.
39 Watu waliokuwa wakipita njiani walimtukana, wakatikisa vichwa vyao 40 na kusema, “Si ulisema ungevunja Hekalu na kulijenga kwa muda wa siku tatu? Jiokoe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu shuka msalabani.” 41 Hali kadhalika, makuhani wakuu, walimu wa sheria na wazee walimdhihaki, wakisema, 42 “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye si Mfalme wa Israeli? Ashuke kutoka msalabani nasi tutamwamini. 43 Anamwamini Mungu; basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka. Kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 44 Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa naye walimtukana kwa njia hiyo hiyo.
Kifo Cha Yesu
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?”
47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu].
50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho. 51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52 Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliofariki ili fufuka. 53 Walitoka makaburini na Yesu alipofufuka walikwenda Mji Mtakatifu wakawatokea watu wengi. 54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yote yaliyotokea, waliogopa wakasema, “Hakika, huyu alikuwa
Mwana wa Mungu!”
55 Wanawake wengi walio kuwa wamefuatana na Yesu tangu Gali laya wakimhudumia, nao walikuwapo wakitazama kwa mbali yote yali yotokea. 56 Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo na Yusufu na mama yao wana wa Zebedayo.
Yesu Azikwa Kaburini
57 Ilipofika jioni, alifika tajiri mmoja kutoka Arimathea aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akaenda kwa Pilato akaomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59-60 Yusufu alichukua mwili wa Yesu akauweka katika sanda safi akauzika katika kaburi lake jipya ambalo lilikuwa limechongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe kubwa akafu nika mlango wa kaburi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikuwa wamekaa mbele ya kaburi.
Walinzi Wa Kaburi
62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.” 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka askari walinzi.
Yesu Afufuka
28 Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. 2 Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. 3 Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4 Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.
5 Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6 Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. 7 Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha waambia.” 8 Wakiwa wamejawa na hofu na furaha nyingi, wale wanawake waliondoka upesi pale kaburini, wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi habari hizo.
9 Mara, Yesu akawatokea, akawasalimia, “Salamu!” Wale wana wake wakamwendea wakajitupa chini wakaishika miguu yake, wakam wabudu. 10 Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, wataniona huko.”
Taarifa Ya Askari
11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea. 12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’ 14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yo yote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.
Yesu Awatuma Wanafunzi Wake
16 Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya kwe nye ule mlima ambao Yesu aliwaagiza. 17 Walipomwona, walimwabu du. Lakini baadhi yao waliona mashaka.
18 Yesu akawakaribia akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji
1 Huu ni mwanzo wa Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2 Kama alivyoandika nabii Isaya, Mungu alisema: “Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye ataandaa njia yako.” 3 “Mtu aitaye kwa sauti kuu jangwani. ‘Mtengenezeeni Bwana njia; nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”
4 Yohana alitokea nyikani, akawabatiza watu huko na kuwahubi ria kwamba watubu, wabatizwe, ili wasamehewe dhambi zao. 5 Watu kutoka eneo lote la Yudea na sehemu zote za Yerusalemu walikwenda kumsikiliza. Wakatubu dhambi zao, akawabatiza katika mto wa Yor dani. 6 Yohana alivaa mavazi ya manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa ni nzige na asali ya mwituni. 7 Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezo kunizidi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 8 Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawaba tiza kwa Roho Mtakatifu.”
Yesu Abatizwa
9 Baadaye Yesu akaja kutoka Nazareti katika sehemu ya Gali laya, akabatizwa na Yohana katika mto wa Yordani. 10 Yesu alipo toka kwenye maji aliona mbingu zikifunuka na Roho wa Mungu anam shukia kama njiwa. 11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa; nimependezwa nawe.”
Yesu Ajaribiwa Nyikani
12 Mara tu baada ya haya, Roho akamwongoza Yesu mpaka nyikani. 13 Akakaa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini aki jaribiwa na shetani. Alikaa na wanyama wa porini na malaika wal imhudumia.
Yesu Aanza Kuhubiri
14 Yohana mbatizaji alipokamatwa na kutiwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya akaanza kutangaza Habari Njema za Mungu, 15 akisema, “Wakati umefika: Ufalme wa Mungu umewasili. Tubuni, muamini Habari Njema.”
Yesu Awaita Wanafunzi Wanne
16 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa la Galilaya alimwona Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa kutumia nyavu; ndugu hawa wawili walikuwa wavuvi. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” 18 Wakaacha nyavu zao mara moja wakamfuata Yesu.
19 Alipokwenda mbele kidogo, akawaona Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo. Wao walikuwa katika mashua wakitengeneza nyavu zao. 20 Mara tu alipowaona akawaita, nao wakamwacha baba yao na wavuvi wa kuajiriwa, wakamfuata Yesu.
Yesu Afukuza Pepo Mchafu
21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda katika sinagogi akaanza kufundisha. 22 Watu waliom sikiliza, walishangazwa sana na mafundisho yake. Yeye hakufund isha kama walimu wao wa sheria. Alifundisha kama mtu mwenye mam laka.
23 Wakati huo huo, mtu mmoja aliyekuwa na pepo 24 akapiga kelele humo katika sinagogi akasema, “Mbona unatuingilia, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninafahamu wewe ni nani! Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 25 Lakini Yesu akamkemea akamwambia, “Kaa kimya! Mtoke!” 26 Yule pepo mchafu akamtikisa yule mtu kwa nguvu kisha akamtoka akipiga kelele.
27 Watu wakashangaa, wakaanza kuulizana, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya? Huyu mtu anatoa amri kwa mamlaka na hata pepo wanamtii!”
28 Sifa zake zikaenea upesi kila mahali katika mkoa wote wa
Yesu Amponya Mama Mkwe Wa Simoni
29 Yesu na wanafunzi wake walipoondoka katika sinagogi, walikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. Wanafunzi wengine waliokuwepo ni Yakobo na Yohana. 30 Mama mkwe wake Simoni alikuwa kitandani, ana homa. Na mara Yesu alipofika wakamweleza. 31 Yesu akaenda karibu na kitanda, akamshika yule mama mkono, akamwinua; homa ikamtoka, akawahudumia.
Yesu Aponya Wengi
32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni nani.
Yesu Aondoka Kapernaumu Na Kwenda Galilaya
35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda mahali pa faragha, akaomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta. 37 Walipomwona wakamwambia, “Kila mtu ana kutafuta!”
38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.” 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya nzima akihubiri katika masinagogi na kuponya watu waliopagawa na pepo.
Yesu Amponya Mtu Mwenye Ukoma
40 Akaja mtu mwenye ukoma, akapiga magoti mbele ya Yesu akamsihi, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.” 41 Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka upone, takasika.” 42 Mara ukoma wote ukaisha akapona kabisa. 43 Yesu akamruhusu aende lakini 44 akamwonya, “Usimwambie mtu ye yote habari hizi; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka ya utakaso kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwa watu.”
45 Lakini yule mtu alikwenda akatangaza habari za kuponywa kwake kila mahali. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia katika vijiji na miji waziwazi isipokuwa alikaa sehemu zisizo na watu, nao wakamfuata huko kutoka pande zote.
Yesu Amponya Mtu Aliyepooza
2 Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu; watu waka pata habari kuwa amerudi nyumbani. 2 Wakakusanyika kwa wingi isibaki nafasi hata mlangoni! Naye akawahubiria. 3 Wakaja watu wanamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4 Waliposhindwa kumfikia Yesu kwa ajili ya msongamano wa watu, wakatoboa tundu darini, wakamshusha ndani yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.
5 Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Mwa nangu, dhambi zako zimesamehewa.” 6 Baadhi ya walimu wa sheria waliokuwepo wakawaza mioyoni mwao, 7 “Mbona mtu huyu anasema maneno haya? Anakufuru! Hajui kuwa ni Mungu peke yake awezaye kusamehe dhambi?”
8 Yesu akatambua mawazo yao, kwa hiyo akawaambia, “Kwa nini mnawaza hivyo? 9 Ni jambo gani lililo rahisi zaidi, kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’? Au, ‘Inuka, chukua kitanda chako uende’? 10 Lakini ili kuwahakikishia kwamba mimi Mwana wa Adamu ninao uwezo hapa duniani wa kusamehe dhambi,” - akamwambia yule aliyepooza 11 “Nakuambia, inuka, chukua kitanda chako uende nyumbani.”
12 Yule mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akachukua kitanda chake akatembea mbele yao wote! Tukio hili likawashangaza watu wote, wakamsifu Mungu, wakasema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!”
Yesu Amwita Mathayo
13 Yesu akaenda tena kando kando ya Ziwa la Galilaya. Umati wa watu ukamfuata naye akaanza kuwafundisha. 14 Alipokuwa aki tembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi katika kibanda cha kukusanyia kodi, akamwambia, “Nifuate”. Lawi akatoka, akamfuata Yesu. 15 Yesu alipokuwa akila chakula nyumbani kwa Lawi, watoza ushuru wengi pamoja na wenye dhambi walikuwa wameketi mezani pamoja naye na wanafunzi wake; kwa maana watu wengi wa aina hii walikuwa wamemfuata. 16 Baadhi ya walimu wa sheria ambao wali kuwa Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, wakawauliza wanafunzi wake, “Yesu anawezaje kula na watoza ushuru na wenye dhambi?” 17 Yesu aliposikia haya aka waambia, “Wenye afya nzuri hawahitaji daktari, bali wagonjwa wanamhitaji. Sikuja kuwaalika wenye haki, bali wenye dhambi.”
Yesu Afundisha Kuhusu Kufunga
18 Wakati mmoja wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wamefunga. Baadhi ya watu wakaja kwa Yesu wakamwuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na wako hawafungi?”
19 Yesu akawajibu, “Inawezekanaje wageni wa bwana harusi wafunge wakati bwana harusi yungali nao? Maadamu bwana harusi yupo, haiwezekani wafunge. 20 Lakini wakati utafika ambapo bwana harusi atachukuliwa. Siku hiyo ndipo watakapofunga.
21 “Hakuna mtu anayeshonea kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, ile nguo iliyochakaa itachanika zaidi pale penye kiraka kipya na kuharibika zaidi. 22 Wala hakuna mtu anayeweka divai mpya katika viriba vya zamani. Akifa nya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, kwa hiyo ata poteza divai na viriba pia. Divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.”
Yesu Afundisha Kuhusu Sabato
23 Siku moja ya sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake, wal ikuwa wakipita katikati ya mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano. 24 Mafarisayo wakamwambia, “Mbona wanafanya jambo ambalo si halali kufanywa siku ya sabato?”
25 Yesu akawaambia, “Hamjasoma alivyofanya Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? 26 Aliingia katika nyumba ya Mungu wakati Abiatha akiwa kuhani mkuu, akala mkate wa sadaka walioruhusiwa kuula ni makuhani peke yao - na akawagawia wafuasi wake.” 27 Kisha akawaambia, “Sabato iliwekwa kwa faida ya mwanadamu, lakini mwanadamu hakuwekwa kwa ajili ya sabato. 28 Na mimi, Mwana wa Adamu, ni Bwana hata wa sabato.”
Yesu Amponya Mtu Aliyelemaa Mkono
3 Yesu aliingia tena katika sinagogi na mtu mmoja aliyelemaa mkono alikuwapo pia. 2 Baadhi ya watu waliokuwa wakimtega, ili wapate sababu ya kumshtaki, walimtazama kwa makini waone kama atamponya huyo kilema siku ya sabato. 3 Yesu akamwambia yule mwe nye mkono uliolemaa, “Njoo hapa mbele.”
4 Yesu akawauliza, “Ni lipi lililo halali siku ya sabato? Kufanya jema, au baya? Kusalimisha maisha au kuua?” Wakakaa kimya.
5 Yesu akawatazama kwa hasira, akahuzunishwa na ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akauny oosha, nao ukapona kabisa! 6 Kisha Mafarisayo wakatoka nje, wakaenda kushauriana na kundi la wafuasi wa Herode mbinu za kum wua Yesu.
Umati Wa Watu Wamfuata Yesu
7 Yesu pamoja na wanafunzi wake waliondoka mahali hapo wakaenda ziwani wakifuatwa na umati mkubwa wa watu kutoka Gali laya na Yudea. 8 Na watu kutoka Yerusalemu, Idumaya, na eneo lote la ng’ambo ya Yordani, sehemu za Tiro na Sidoni, waliposi kia mambo aliyokuwa akitenda, wakamwendea. 9 Akawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua ili asisongwe na kubanwa sana na watu. 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wote wenye mar adhi walikuwa wakisukumana wapate kumgusa. 11 Na kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia kwa sauti kuu, “Wewe ni Mwana wa Mungu.” 12 Lakini aliwaamuru wasimtambulishe kwa watu.
Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili
13 Yesu alipanda mlimani akawaita wale aliowataka, nao wakaja. 14 Akawachagua kumi na wawili wafuatane naye na awatume kuhubiri na 15 wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16 Hawa ndio aliowachagua: Simoni, ambaye alimwita Petro, 17 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo ambao aliwaita Boanerge, yaani wana wa ngurumo; 18 Andrea; Filipo; Bartholomayo; Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Thadayo; Simoni, Mkanaani; na 19 Yuda
Yesu Na Beelzebuli
20 Yesu akarudi nyumbani. Umati wa watu ukamfuata tena, hata yeye na wanafunzi wake wakashindwa kula chakula. 21 Ndugu zake walipopata habari walikuja kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”
22 Walimu wa sheria waliotoka Yerusalemu walikuwa wakisema, “Amepagawa na Beelzebuli, mkuu wa mashetani; na ni kwa uwezo wa Beelzebuli anawafukuza mashetani.”
Beelzebuli anawafukuza mashetani.”
23 Basi Yesu akawaita akazungumza nao kwa mifano: “Shetani awezaje kufukuza shetani? 24 Ikiwa utawala wa nchi umegawanyika wenyewe, hauwezi kudumu. 25 Hali kadhalika kama jamaa moja ime gawanyika yenyewe kwa yenyewe, jamaa hiyo haiwezi kudumu. 26 Na kama shetani akijipiga vita yeye mwenyewe hatatimiza cho chote ila mwisho wake umekaribia. 27 Pia hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumwibia vitu vyake vyote pasipo kwanza kumfunga huyo mwenye nyumba mwenye nguvu. Akisha mfunga, ndipo anaweza kumwibia kila kitu.
28 “Nawaambieni kweli, dhambi zote watendazo wanadamu na maneno yote ya kufuru wasemayo, watasamehewa. 29 Lakini ye yote anayemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” 30 Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema ana pepo mchafu.
Mama Na Ndugu Wa Yesu
31 Mama yake Yesu na ndugu zake wakafika wakasimama nje wakamtuma mtu amwite. 32 Umati wa watu waliokuwa wameketi kum zunguka wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wana kutafuta.”
33 Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?”
34 Akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka, akasema, “Hawa ndio mama zangu na ndugu zangu. 35 Mtu ye yote anayetenda mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.”
Mfano Wa Mbegu
4 Wakati mwingine tena Yesu alianza kufundisha kando ya ziwa. Watu wengi walikusanyika wakasongamana mpaka ukingoni mwa ziwa. Ikambidi Yesu aingie kwenye mashua, akaketi humo. 2 Akawafundisha mambo mengi kwa kutumia mifano na katika mafundisho yake akasema:
3 “Sikilizeni! Mkulima mmoja alikwenda kupanda mbegu zake. 4 Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani; ndege wakaja wakazila. 5 Nyingine zilianguka kwenye mwamba ambapo kuli kuwa na udongo haba; zikaota haraka. Kwa kuwa udongo haukuwa na kina, 6 jua kali lilipowaka zilinyauka na kukauka kwa kuwa hazi kuwa na mizizi. 7 Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga kwahiyo hazikuzaa matunda.
8 Na mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua; zikazaa matunda; moja thelathini, nyingine sitini na nyingine mia moja.” 9 Kisha Yesu akasema, “Mwenye nia ya kusikia na asikie.”
Kwa Nini Yesu Alitumia Mifano
10 Alipokuwa peke yake, baadhi ya wale waliokuwepo, pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili, walimwuliza kuhusu mifano yake. 11 Akawaambia, “Siri ya Ufalme wa Mungu imefunuliwa kwenu, lakini kwa wale walioko nje ya Ufalme wa Mungu, kila kitu husemwa kwa mifano 12 ili: ‘Kutazama watazame lakini wasione, kusikia wasikie lakini wasielewe. Kwa maana kama wangesikia na kuelewa wangegeuka na kutubu, wakasamehewa.’ ”
Yesu Afafanua Maana Ya Mfano Wa Mbegu
13 Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Mtaelewaje basi mifano mingine? 14 Yule mtu aliyepanda mbegu, alipanda neno la Mungu. 15 Mbegu zilizoanguka njiani ni sawa na watu ambao husikia neno la Mungu na shetani akaja mara moja na kulichukua lile neno lililopandwa ndani yao. 16 Hali kadhalika, mbegu iliyoanguka kwenye mwamba ni sawa na watu ambao hulisikia neno na kulipokea kwa furaha. 17 Lakini kwa kuwa neno halipenyi ndani, linadumu kwa muda mfupi. Taabu au mateso yanapotokea kwa ajili ya hilo neno, wao hupoteza imani yao. 18 Na wengine, ni kama mbegu zile zilizoanguka kwenye miiba. Wao hulisikia neno, 19 lakini mahangaiko ya dunia, udanganyifu wa mali na tamaa za mambo mbalimbali hulisonga lile neno, lisizae matunda.
20 “Bali wengine ni kama ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri. Wao hulisikia neno wakalipokea na kuzaa matunda: wengine thelathini, wengine sitini, na wengine mia moja.”
Mfano Wa Taa
21 Akawaambia tena, “Je, mtu anapowasha taa, huifunika kwa bakuli au kuiweka mvunguni? Si anaiweka mahali pa wazi? 22 Hali kadhalika, kila kilichofichwa kitatolewa hadharani; na kila siri itafichuliwa. 23 Mwenye nia ya kusikia, na asikie.”
24 Akaendelea kuwaambia, “Myaweke maanani haya mnayosikia. Kipimo mnachotumia kwa wengine ndicho kitakachotumiwa kuwapima na ninyi, hata na zaidi. 25 Kwa maana aliye na kitu ataongezewa, na asiye na kitu atanyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”
Mfano Wa Jinsi Mbegu Inavyoota
26 Akawaambia tena, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27 Akishazipanda, usiku hulala na mchana huamka, wakati huo mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua inakuaje. 28 Udongo wenyewe huwezesha mimea hiyo kuchipua, kukua na kukomaa. 29 Mavuno yanapokuwa tayari, bila kupoteza wakati, yule mkulima huleta mtu akaikata hiyo mimea kwa kuwa wakati wa kuvuna umefika.”
Mfano Wa Mbegu Ya Haradali
30 Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuuelezea? 31 Tunaweza kuufa nanisha na punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. 32 Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wakaweza kujenga viota kwenye kiv uli chake.”
33 Yesu alitumia mifano mingine mingi kama hii kuwaelezea neno la Mungu, kwa kadiri walivyoweza kuelewa. 34 Hakuwafundisha lo lote kuhusu Ufalme wa Mungu pasipo kutumia mifano. Lakini ali pokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.
Yesu Atuliza Dhoruba
35 Siku hiyo, ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke, twende ng’ambo ya pili.” 36 Wakawaacha wale watu wakaingia katika ile mashua ambamo Yesu alikuwa amekaa. Pia palikuwa na mashua nyingine.
37 Pakatokea dhoruba kali, mawimbi yakaipiga ile mashua waliyokuwa wakivukia, ikaanza kujaa maji. Yesu alikuwa amelala akiegemea mto sehemu ya nyuma kwenye ile mashua. 38 Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kwamba tuna zama?’ 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akaiambia ile bahari, “Kaa kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari.
40 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa? Je, bado hamna imani?”
41 Lakini wao walikuwa wamejawa na hofu wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”
Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo
5 Wakafika upande wa pili wa ziwa wakaingia katika jimbo la Wagerasi. 2 Yesu alipotoka kwenye mashua, mtu mmoja mwenye pepo mchafu alitoka makaburini akaja kukutana naye. 3 Mtu huyu aliishi makaburini wala hakuna aliyeweza kumfunga hata kwa minyororo , 4 kwa maana mara nyingi alipofungwa kwa minyororo mikononi na vyuma miguuni, aliivunjavunja na hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Usiku na mchana alikaa makaburini na milimani aki piga makelele na kujikatakata kwa mawe.
6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia akapiga magoti mbele yake, 7 akapiga kelele kwa nguvu akasema, “Unataka nini kwangu, Yesu, Mwana wa Mungu Mkuu? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!” 8 Alisema hivi kwa kuwa Yesu alikuwa akimwambia, “Mtoke huyu mtu! Wewe pepo mchafu!”
9 Yesu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jina langu ni jeshi, kwa maana tupo wengi.” 10 Akamwomba sana Yesu asiwapeleke nje ya jimbo lile. 11 Hapo hapo lilikuwapo kundi la nguruwe likilisha kando ya mlima. 12 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Turuhusu tukawaingie wale nguruwe.” 13 Basi akawaruhusu. Wakamtoka yule mtu wakaenda wakawaingia wale nguruwe na kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likatimka kasi kwenye mteremko ule, wakazama ziwani, wakafa.
14 Wale waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotokea. Watu wakatoka kwenda kujionea mambo hayo.
15 Wakaja kwa Yesu, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akiwa ameketi, amevaa nguo na pia akiwa na akili timamu. Wakaogopa. 16 Wale walioyaona mambo haya waliwaeleza wengine yaliyomto kea yule aliyekuwa na pepo na lile kundi la nguruwe. 17 Basi watu wakaanza kumwomba Yesu aondoke katika wilaya yao.
18 Yesu alipoanza kuingia kwenye mashua, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akamsihi Yesu waende pamoja. 19 Yesu akamka talia. Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Bwana na jinsi alivyokuhuru mia.” 20 Yule mtu akaenda akaanza kutangaza katika Dekapoli - yaani miji kumi, mambo makuu aliyomtendea Bwana. Na watu wote wakastaajabu.
Yesu Amponya Mama Aliyetokwa Damu
21 Yesu alipokwisha vuka tena na kufika ng’ambo ya pili, umati mkubwa wa watu ukamzunguka, yeye akiwa kando ya ziwa. 22 Kisha kiongozi mmoja wa sinagogi aliyeitwa Yairo akamjia Yesu akapiga magoti miguuni pake, 23 akamsihi, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali njoo umguse kwa mikono yako apate kupona na kuishi.” 24 Basi Yesu akaongozana naye. Umati mkubwa wa watu waliomfuata wakawa wanamsonga.
25 Na alikuwepo mama mmoja aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili. 26 Mama huyu alikuwa amehangaika sana, akiwa ametibiwa na waganga wa kila aina na kutumia fedha yake yote kwa waganga lakini hakupata nafuu. Hali yake ilizidi kuwa mbaya. 27 Alikuwa amesikia habari za Yesu kwa hiyo alimfuata kwa nyuma, akapenyeza kati ya watu, akaligusa vazi lake. 28 Maana alisema moyoni mwake, “Nikiligusa vazi lake tu, nitapona.” 29 Mara damu iliyokuwa inamtoka ikakauka; akajisikia amepona kabisa.
30 Yesu akafahamu kuwa nguvu zimemtoka. Akageuka, akawauliza wale watu, “Ni nani amenigusa?”
31 Wanafunzi wake wakamjibu, “Mbona unauliza ni nani ameku gusa? Huoni umati huu ulivyokusonga?” 32 Lakini Yesu alizidi kutazama aone ni nani aliyemgusa. 33 Kisha yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni kwake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. 34 Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako.”
Yesu Amfufua Binti Yairo
35 Alipokuwa akiongea, watu wakafika kutoka nyumbani kwa Yairo wakamwambia, “Usimsumbue tena mwalimu, binti yako amefar iki. ” 36 Lakini Yesu hakuyatilia maanani maneno hayo, akamwam bia Yairo, “Usiogope, bali amini tu.”
37 Hakumruhusu mtu mwingine amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo.
38 Walipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi, Yesu aliona vurugu na watu wengi wakilia na kuomboleza kwa nguvu. 39 Alipoingia ndani, aliwaambia, “Kwa nini mnafanya vurugu na kuomboleza? Mtoto hakufariki bali amelala.” 40 Wale watu wakam cheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaenda pale alipokuwa yule mtoto. 41 Akamwinua mtoto akamwam bia, “Talitha kumi!” Maana yake, “Binti mdogo, nakwambia amka!’ ’
42 Mara yule mtoto akasimama, akaanza kutembea. Alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili. Walipoona haya, walistaajabu sana. 43 Yesu akawaamuru wasimweleze mtu jambo hili, na akawaambia wampe yule mtoto chakula.
Watu Wa Nazareti Wamkataa Yesu
6 Yesu akaondoka mahali hapo, akaenda mji wa kwao, akifu atana na wanafunzi wake. 2 Ilipofika siku ya sabato, alianza ku fundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia walishangaa. Wakasema, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya? Amepataje kuwa na hekima ya namna hii? Amepata wapi uwezo wa kutenda miujiza ya namna hii? 3 Huyu si yule seremala mtoto wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Dada zake si tuko nao hapa?” Basi hawakumwamini.
4 Yesu akawaambia, ‘ ‘Nabii huheshimiwa kila mahali isipokuwa katika mji wake na kati ya jamaa na ndugu zake.” 5 Hakufanya miujiza yo yote huko isipokuwa kuwagusa wagonjwa wachache na kuwaponya. 6 Alishangazwa sana na jinsi walivyokuwa hawana imani.
Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili
7 Akawaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili na akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu.
8 Akawaagiza wasichukue cho chote safarini isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mfuko, wala fedha. 9 Ila wavae viatu lakini wasichukue nguo ya kubadili. 10 Pia akawaambia, “Mkiin gia nyumba yo yote, kaeni hapo hapo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 Na mahali po pote ambapo hamtakaribishwa wala kusikili zwa, mtakapoondoka hapo, kung’uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, kama onyo lenu kwao.”
12 Kwa hiyo wakatoka, wakaenda wakihubiri kwamba watu wat ubu, waache dhambi. 13 Wakawatoa watu wengi pepo, wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.
Kifo Cha Yohana Mbatizaji
14 Mfalme Herode akapata habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limefahamika kila mahali. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu ndiyo maana uwezo wa kutenda miujiza unafanya kazi ndani yake!” 15 Wengine walisema, “Huyo ni Eliya!” Na wengine wakasema, “Ni nabii kama wale manabii wa zamani.” 16 Lakini Herode ali posikia habari hizi alisema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji niliyem kata kichwa; amefufuka!” 17 Kwa maana Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, awekwe gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa kaka yake, Filipo, ambaye alikuwa amemwoa. 18 Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali wewe kumwoa mke wa kaka yako.” 19 Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwe kea kinyongo Yohana akataka kumwua. Lakini hakupata nafasi, 20 kwa sababu Herode alimwogopa Yohana ambaye alifahamu kuwa ni mtu mwenye haki na mtakatifu, akawa anamlinda. Ingawa Herode alifadhaika sana kila alipomsikiliza Yohana, bado alipenda kumsi kiliza.
21 Baadaye Herodia alipata nafasi aliyokuwa akiitafuta. Wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwa mfalme Herode, mfalme alifanya sherehe kubwa, akawaalika viongozi wakuu wa ikulu, makamanda wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. 22 Binti yake Herodia akaja akacheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake. Mfalme Her ode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.” 23 Akala kiapo akamwambia, “Cho chote utakachoomba, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu, nitakupa.”
24 Yule binti akaenda akamwuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama yake akajibu, “Mwombe kichwa cha Yohana Mbati zaji.” 25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia .” 26 Mfalme akajuta sana, lakini hakuweza kumkatalia kwa kuwa alikuwa ameapa mbele ya wageni wake, na hakupenda kuvunja ahadi yake. 27 Kwa hiyo Herode akamtuma mmojawapo wa walinzi wake mara moja akamwagiza alete kichwa cha Yohana. 28 Yule mlinzi akaenda gerezani akamkata Yohana kichwa kisha akakileta kwenye sinia akampa yule binti; naye akampatia mama yake.
29 Wanafunzi wa Yohana walipopata habari hizi, walikuja wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.
Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda mahali pasipo na watu.
33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda. Wakawahi kufika.
34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda. 36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba na vijiji vya jirani.”
37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya kutosha kulisha watu wote hawa.”
38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”
39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.
Yesu Atembea Juu Ya Maji
45 Wakati huo huo Yesu akawaamuru wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye anawaaga watu. 46 Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kusali. 47 Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imeshafika katikati ya ziwa na Yesu alikuwa peke yake nchi kavu. 48 Aliwaona wanafunzi wake wakihangaika na kuvuta makasia kwa nguvu kwa sababu upepo ulikuwa ukielekea walikotoka. Karibu na mapambazuko, Yesu aka waendea wanafunzi wake akitembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, walid hani ni mzimu, wakapiga yowe, 50 kwa maana wote walimwona wakaogopa. Lakini mara Yesu akasema nao, “Tulieni! Ni mimi, msi ogope!” 51 Akapanda kwenye mashua yao na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa. 52 Walikuwa bado hawajaelewa hata maana ya u le muujiza wa mikate. Walikuwa bado hawajafunuliwa akilini mwao.
53 Walipokwisha kuvuka, walifika katika wilaya ya Gene zareti, wakatia nanga. 54 Waliposhuka kutoka katika mashua yao, watu walimtambua Yesu mara moja, 55 wakapita vijiji vyote haraka haraka, wakawabeba wagonjwa kwenye machela wakamfuata mahali po pote waliposikia kuwa yupo. 56 Na kila mahali Yesu alipokwenda, ikiwa ni vijijini, mijini na mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa angalao waguse pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.
Mafundisho Ya Kale
7 Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu. 2 Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi. 3 Wayahudi, na hasa Mafarisayo, hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata mila za wazee wao. 4 Na kwa sheria wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu, na vyombo vya shaba.
5 Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria walimwuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee wetu, na badala yake wa nakula kwa mikono najisi?”
6 Yesu akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa: ‘Watu hawa wanani heshimu kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. 7 Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ 8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.” 9 Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu! 10 Kwa mfano, Musa alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtuka naye baba au mama auawe.’ 11 Lakini ninyi mnasema mtu akimwambia baba yake au mama yake kuwa, “Msaada ambao ningekupa ni Kor bani,” yaani umetengwa kama sadaka kwa Mungu, 12 basi hawaji biki tena kumsaidia baba yake au mama yake. 13 Kwa njia hiyo mnadhalilisha neno la Mungu kwa taratibu zenu mlizojiwekea. Na mnafanya mambo mengi ya jinsi hii.”
14 Yesu akaita tena ule umati wa watu akawaambia, “Nisiki lizeni nyote kwa makini na muelewe. 15 Hakuna kitu kinachomwin gia mtu kutoka nje ambacho kinaweza kumfanya mchafu. Kitu kina chotoka ndani yake ndicho kinachomfanya mchafu. 16 Mwenye nia ya kusikia na asikie.”
17 Alipoachana na wale watu aliingia ndani. Wanafunzi wake wakamwuliza maana ya mfano ule. 18 Akawajibu, “Hata nanyi hamwelewi? Hamtambui kwamba kitu kimwingiacho mtu kutoka nje hakiwezi kumfanya mchafu? 19 Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje. Kwa kusema hivi, Yesu alifundisha kuwa aina zote za vyakula ni halali kuliwa.
20 Akaendelea kusema, “Kile kitokacho ndani ya mtu ndicho kinachomfanya awe mchafu. 21 Kwa maana ndani ya mtu, yaani moy oni mwake, hutoka: mawazo mabaya, uasherati, 22 wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matusi, kiburi na upumbavu. 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, na ndio yanayomfanya mchafu.”
Yesu Amponya Binti Ya Mama Mtaifa
24 Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia nyumba moja, ambapo hakupenda mtu afahamu yupo. Lakini hakuweza kujificha. 25 Mama mmoja ambaye binti yake mdogo ali kuwa na pepo mchafu aliposikia habari za Yesu, alikuja mara moja akajiangusha miguuni pake. 26 Huyo mama hakuwa Myahudi, alikuwa Mgiriki aliyezaliwa Siria-Foinike. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.
27 Yesu akamwambia, “Tuwaache watoto wale washibe kwanza, kwa maana si halali kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”
28 Yule mama akajibu, “Ni kweli Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.” 29 Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, unaweza kwenda nyumbani. Yule pepo ameshamtoka binti yako.”
30 Akaenda nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo amemtoka.
Yesu Amponya Mtu Aliyekuwa Bubu Na Kiziwi
31 Yesu akaondoka katika eneo la Tiro, akapita katikati ya Sidoni akaenda hadi Ziwa la Galilaya kwa kupitia katika eneo la Dekapoli. 32 Hapo, watu walimletea kiziwi mmoja ambaye pia alikuwa hawezi kusema sawa sawa, wakamwomba amwekee mikono ili apone. 33 Yesu akampeleka yule kiziwi kando mbali na watu, akain giza vidole masikioni mwake kisha akatema mate na akaugusa ulimi wake. 34 Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akahema kwa uchungu, akamwambia, “Efatha!” yaani “Funguka!” 35 Wakati huo huo masikio ya yule mtu yakafunguka na ulimi wake ukawa huru akaanza kusema vizuri.
36 Yesu akawaamuru wasimwambie mtu ye yote habari hizi. Lakini kadiri alivyowazuia ndivyo walivyozidi kutangaza habari zake. 37 Watu wakastaajabu mno. Wakasema, “Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!”
Yesu Alisha Watu Elfu Nne
8 Muda si mrefu baadaye, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 2 “Ninawaonea huruma hawa watu. Wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. 3 Nikiwaruhusu waende bila kula, watazimia njiani na baadhi yao wametoka mbali.”
4 Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha?”
5 Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Saba.”
6 Akawaambia watu wakae chini. Kisha akaichukua ile mikate saba na baada ya kushukuru akaimega, akawapa wanafunzi wake wawa gawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. 7 Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. 8 Watu walikula wakatosheka na baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba. 9 Na watu waliokula walikuwa wapata elfu nne. Baada ya kuwaaga, 10 aliin gia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake akaenda sehemu za Dal manutha.
11 Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12 Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Nawaambieni kweli, hakitapewa ishara yo yote.” 13 Kisha aka waacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ng’ambo ya pili.
Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode
14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 15 Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”
16 Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema,“Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.”
17 Yesu alifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mna zungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 18 Mbona mna macho lakini mnashindwa kuona, na masikio lakini mnashindwa kusikia? Je hamkumbuki? 19 Nilipoimega mikate mitano kuwalisha watu elfu tano, mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” 20 “Na nilipomega mikate saba kuwalisha watu elfu nne mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Saba.” 21 Aka wauliza, “Je, bado tu hamwelewi?”
Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida
22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta kipofu mmoja wakamsihi Yesu amguse. 23 Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamwuliza, “Unaona cho chote?”
24 Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu; wanaonekana kama miti ikitembea.”
25 Yesu akamwekea tena mikono machoni. Ndipo akaona vizuri. Macho yake yakapona kabisa akaweza kuona kila kitu sawa sawa.
26 Yesu akamruhusu aende nyumbani kwake akisema, “Hata kijijini usipitie.”
27 Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria Filipi. Walipokuwa njiani Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”
28 Wakamjibu, “ Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”
29 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, ‘ ‘Wewe ndiye Kristo.”
30 Akawaonya wasim wambie mtu ye yote habari zake.
Yesu Azungumza Juu Ya Kifo Chake
31 Akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa yeye, Mwana wa Adamu, atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, na makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na baada ya siku tatu atafufuka. 32 Aliyasema haya wazi wazi. Ndipo Petro akam chukua kando akaanza kumkemea. 33 Lakini Yesu alipogeuka na kuwatazama wanafunzi wake alimkaripia Petro akamwambia, “Ondoka mbele yangu, shetani! Mawazo yako hayako upande wa Mungu bali upande wa wanadamu.”
34 Ndipo akawaita wale watu pamoja na wanafunzi wake aka waambia, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwe nyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 35 Kwa maana mtu ye yote aipotezaye nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, ataiokoa. 36 Mtu atafaidi nini kama atapata ulimwengu wote lakini akayaangamiza maisha yake? 37 Au mtu atatoa nini apate tena maisha yake? 38 Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu, na mimi, Mwana wa Adamu, nitamwonea aibu wakati nitakapokuja katika utu kufu wa Baba yangu na malaika watakatifu.”
9 Yesu akaendelea kuwaambia, ‘ ‘Ninawahakikishia kuwa wapo watu hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”
Yesu Ageuka Sura
2 Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana akawapeleka juu ya mlima mrefu ambapo walikuwa faraghani, peke yao. Na huko, wakiwa wanamtazama, Yesu akageuka sura. 3 Mavazi yake yakametameta kwa weupe, yakang’aa, yakawa meupe kuliko ambavyo dobi ye yote duniani angaliweza kuyang’aarisha. 4 Musa na Eliya wakawatokea nao walikuwa wakizungumza na Yesu.
5 Petro akamwambia Yesu , “Mwalimu, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Tutengeneze vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Musa na kingine cha Eliya.” 6 Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.
7 Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, na sauti kutoka katika wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu nimpendaye, msikilizeni yeye.” 8 Mara walipotazama huku na huku hawakuona mtu mwingine tena isipokuwa Yesu.
9 Walipokuwa wakiteremka mlimani, Yesu akawakataza wasim wambie mtu ye yote mambo waliyoona, mpaka yeye Mwana wa Mungu atakapofufuka kutoka kwa wafu. 10 Wakatii agizo hilo, lakini wakawa wanajadiliana kati yao maana ya ‘Kufufuka kutoka kwa wafu.’ 11 Wakamwuliza, “Kwa nini walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza kabla mambo haya hayajatokea?’ ’ 12 Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya anakuja kwanza kusawazisha mambo yote. Hata hivyo, mbona imeandikwa kwamba Mimi, Mwana wa Adamu ni lazima niteseke sana na kudharauliwa? 13 Lakini nina waambia, Eliya amekwisha kuja na wamemtendea walivyopenda, kama Maandiko yasemavyo juu yake.”
Copyright © 1989 by Biblica