Bible in 90 Days
Kufufuka Kwa Kristo
15 Na sasa napenda kuwakumbusha ndugu zangu kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo ndio msimamo wenu. 2 Mnaoko lewa kwa Injili hii ikiwa mnashikilia imara neno nililowahubiria. Vinginevyo mtakuwa mmeamini bure. 3 Kwa maana niliyopokea ndio niliyowapa ninyi, nayo ni muhimu sana: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama ilivy oandikwa katika Maandiko. 4 Na kwamba alizikwa na kufufuka siku ya tatu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. 5 Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa. 7 Kisha akamtokea Yakobo, na ndipo akawatokea mitume wote. 8 Na mwisho wa wote, akanitokea na mimi, ambaye ni kama nilizaliwa kwa hali isiyo ya kawaida.
9 Kwa maana mimi ni mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya kazi kuliko mitume wote, ingawaje haikuwa mimi bali ni neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. 11 Hivyo basi, kama ilikuwa ni mimi au ni wao, haya ndio tuliyohubiri, na haya ndio mliyoamini.
Kufufuka Kwa Wafu
12 Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, inakuwaje baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13 Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi Kristo hakufufuliwa. 14 Na ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, mahubiri yetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Na zaidi ya hayo, tunaonekana kuwa tunamshuhudia Mungu uongo, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu ya kuwa alimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Na kumbe hakumfu fua, kama kweli wafu hawafufuliwi. 16 Kwa kuwa kama wafu hawa fufuliwi, basi hata Kristo hajafufuliwa. 17 Na ikiwa Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni bure; nanyi bado mngali katika dhambi zenu. 18 Pia waamini wote waliokufa wakimwamini Yesu wamepotea. 19 Na kama imani yetu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, basi sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wengine wo wote duniani. 20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wote waliolala. 21 Kwa maana kama vile kifo kilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 22 Kwa kuwa katika Adamu watu wote hufa, vivyo hivyo katika Kristo wote wata fanywa kuwa hai. 23 Lakini kila mmoja kwa mpango: Kristo ni mat unda ya kwanza ya ufufuo; kisha wale walio wake wakati atakapo kuja watafufuliwa. 24 Ndipo mwisho utafika, wakati ambao ataka bidhi Ufalme kwa Mungu Baba, akiisha angamiza kila mamlaka na uwezo na nguvu. 25 Kwa maana Kristo atamiliki mpaka Mungu ataka powaweka adui zake chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho kuan gamizwa ni kifo. 27 “Kwa maana Mungu ameweka kila kitu chini ya utawala wake, chini ya miguu yake.” Ni wazi kwamba maneno haya, “Kila kitu kimewekwa chini ya utawala wake,” hayamjumlishi na Mungu ambaye ameweka vitu vyote chini ya Kristo. 28 Vitu vyote vikishawekwa chini ya utawala wake, ndipo naye Mwana atakuwa chini ya Mungu ambaye ameviweka vitu vyote chini yake, ili Mungu awe yote katika yote.
29 Vinginevyo, kwa nini watu wanabatizwa kwa niaba ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa niaba yao? 30 Na kwa upande wetu kwa nini tunajitia hatarini kila wakati? 31 Nakufa kila siku, nasema kweli ndugu zangu, kama ninavyojivuna kwa ajili yenu katika Kristo Yesu, Bwana wetu. 32 Kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso kwa sababu za kibinadamu, nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, basi, “Tule na kunywa, kwa maana kesho tutakufa.” 33 Mtu asiwadanga nye, “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34 Pateni tena fahamu, muache kutenda dhambi. Kwa maana baadhi yenu hawam jui Mungu; nasema mambo haya ili muone aibu.
Ufufuo Wa Mwili
35 Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wanafufuliwaje? Wata kuwa na mwili wa namna gani?” 36 Wapumbavu ninyi! Mnachopanda hakiwi hai tena kama hakikufa. 37 Unapopanda, hupandi mwili unaoutegemea, bali unapanda mbegu, pengine mbegu ya ngano au ya nafaka nyingine. 38 Lakini Mungu huipa hiyo mbegu umbo kama alivyochagua mwenyewe, na kila aina ya mbegu ina umbo lake. 39 Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine na hali kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40 Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani; lakini uzuri wa miili ya mbinguni ni wa aina moja na uzuri wa miili ya duniani ni wa aina nyingine. 41 Jua lina uzuri wa aina moja, mwezi nao una uzuri wake na nyota pia; na nyota hutofautiana na nyota nyingine kwa uzuri.
42 Ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Mwili uliopandwa ni wakuharibika; utafufuliwa usioharibika; 43 unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu; unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu. 44 Unapandwa ukiwa mwili wa asili, unafufuliwa ukiwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 45 Kwa hiyo imeandikwa, “Adamu wa kwanza akawa kiumbe hai,” Adamu wa mwisho akawa roho inayohuisha. 46 Lakini si yule wa kiroho aliyekuja kwanza; bali ni yule wa mwili, na kisha yule wa kiroho. 47 Mtu wa kwanza alitokana na mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48 Na kama alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na alivyo mtu wa mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyochukua umbile la mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua umbile la yule mtu kutoka mbinguni. 50 Nawatangazia ndugu zangu kwamba nyama na damu haviwezi kurithi Ufalme wa Mungu, wala uharibifu hauwezi kurithi kutokuharibika.
51 Sikilizeni, nawaambia siri: sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52 ghafla, kufumba na kufumbua, tarumbeta ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa tarumbeta italia, wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53 Kwa maana hali hii ya kuharibika lazima ivae kutokuharibika, na hali hii ya kufa lazima ivae hali ya kutokufa. 54 Kwa hiyo, wakati kuharibika kutakapovaa kutokuharibika, na mwili wa kufa utakapovaa hali ya kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia, “Kifo kimemezwa na ushindi .” 55 “Mauti, ushindi wako uko wapi? Na uchungu wako uko wapi?” 56 Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 Lakini, Mungu ashukuriwe! Yeye anatupa tia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
58 Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana.
Matoleo Kwa Ajili Ya Waamini
16 Na sasa kuhusu matoleo kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Mungu. Kama nilivyoagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. 2 Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake, na fedha hiyo aiweke ili nitaka pokuja pasiwepo na haja ya kufanya mchango. 3 Nikishafika nita wapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili waweze kupeleka zawadi yenu Yerusalemu. 4 Kama ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami.
Mipango Ya Paulo
5 Baada ya kupitia Makedonia, nitakuja kwenu; maana natazamia kupitia Makedonia. 6 Pengine nitakaa nanyi kwa muda, au hata nitakaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili muweze kunisaidia katika safari zangu, po pote niendapo. 7 Kwa maana sipendi niwaone sasa nikiwa napita; natarajia kuwa na muda wa kutosha wa kukaa nanyi, kama Bwana akiruhusu. 8 Lakini nitakaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste. 9 Kwa maana mlango umefunguliwa kwangu kufanya kazi yenye matunda, na huko kuna wapinzani wengi . 10 Ikiwa Timotheo atakuja kwenu mkaribisheni asiwe na woga wo wote akiwa nanyi kwa sababu anaendeleza kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo. 11 Basi asiwepo mtu atakayemdharau. Msafirisheni kwa amani ili aweze kunirudia. Namtegemea yeye pamoja na hao ndugu.
12 Na sasa, kuhusu ndugu yetu Apolo. Nilimsihi sana awa tembelee pamoja na wale ndugu wengine, lakini haikuwa mapenzi yake kuja huko wakati huu. Atakuja apatapo nafasi.
Maneno Ya Mwisho
13 Kesheni; simameni imara katika imani, muwe shujaa na hodari. 14 Fanyeni kila kitu katika upendo. 15 Sasa ndugu zangu, mnafahamu kwamba watu wa nyumbani kwa Stefana walikuwa waamini wa kwanza katika Akaya, nao wamejitoa kuwasaidia watu wa Mungu. 16 Nawasihi mnyenyekee na kufuata uongozi wa watu kama hawa, na wa kila mtendakazi mwenzenu na kila anayejibidisha katika kazi. 17 Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa maana hawa wamenisaidia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. 18 Wao wameburudisha roho yangu na yenu pia. Watu kama hawa, wanastahili kutambuliwa. 19 Makanisa ya Asia wanawas alimu. Akila na Priska, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu katika Bwana. 20 Pia ndugu wote wanawasalimu. Sali mianeni kwa busu takatifu. 21 Mimi Paulo, kwa mkono wangu mwe nyewe, naandika salamu hii. 22 Kama mtu ye yote hampendi Bwana, na alaaniwe. ‘Maranatha.’ Bwana wetu, njoo! 23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.
1 Kutoka kwa Paulo mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu. Kwa Kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watu wote wa Mungu walioko Akaya yote.
2 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Faraja Katika Mateso
3 Ashukuriwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja zote. 4 Yeye anatufariji katika mateso yetu yote ili tuweze kuwafariji wale walio katika mateso yo yote, tukitumia faraja ambayo sisi tumepokea kutoka kwa Mungu. 5 Kama vile tunavyoshiriki mateso ya Kristo yaliyo mengi, ndivyo na far aja yetu inavyomiminika kwa wengine. 6 Kama tunateseka ni kwa faraja yenu na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa faraja yenu, ambayo mnapata wakati mkivumilia kwa subira mateso hayo hayo tunayopata sisi. 7 Matumaini yetu kwenu ni imara; kwa maana tunajua ya kuwa kama mnavyoshiriki katika mateso yetu, mtashiriki pia katika faraja yetu.
8 Hatupendi mkose kujua, ndugu wapendwa, kuhusu mateso tuliy oyapata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo ambayo ilikuwa zaidi ya uwezo wetu kuvumilia, kiasi kwamba tulikata tamaa kwamba tungeishi. 9 Kwa hakika tulijisikia kana kwamba tumehukumiwa kifo. Lakini hii ilitokea ili tusijitegemee wenyewe bali tumtege mee Mungu ambaye anawafufua wafu. 10 Alituokoa katika hatari hiyo ya kifo, na atatuokoa. Tumeweka tumaini letu juu yake kwamba ataendelea kutuokoa. 11 Ninyi pia mtusaidie kwa maombi ili wengi wamshukuru Mungu kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka tulizopokea kama majibu ya maombi ya wengi.
Paulo Abadili Mipango Yake
12 Hii ndio sababu tunajivuna. Dhamiri yetu inatushuhudia kwamba tumeishi katika ulimwengu, na hasa katika uhusiano wetu na ninyi, kwa utakatifu na ukweli utokao kwa Mungu. Hatukufanya hivyo kwa hekima ya mwanadamu bali kwa neema ya Mungu. 13 Kwa maana hatuwaandikii mambo ambayo hamwezi kusoma na kuyaelewa. Natumaini mtaelewa kikamilifu, 14 yale ambayo sasa mnayaelewa kwa sehemu, ili siku ile ya Bwana Yesu muweze kujivuna kwa ajili yetu, kama na sisi tutakavyojivuna kwa ajili yenu.
15 Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilipanga kuwatembelea kwanza ili mpate baraka mara mbili. 16 Nilipanga kuwatembelea nikiwa safarini kwenda Makedonia, na kurudi kwenu tena nikitoka Makedonia ili mnisaidie katika safari yangu ya kwenda Uyahudi. 17 Je, nilikuwa kigeugeu nilipotaka kufanya hivi? Au mimi ninafanya mipango yangu kama watu wa dunia, nikiwa tayari kusema, “Ndiyo” na wakati huo huo kusema, “Hapana”?
18 Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, ahadi yangu haikuwa “Ndiyo” na “Hapana” 19 Kwa kuwa Mwana wa Mungu Yesu Kristo, ambaye tulimhubiri kwenu tukiwa na Silvano, Timotheo, na mimi mwenyewe, hakuwa ‘ndio’ na ‘hapana.’ Katika yeye wakati wote ni ndio. 20 Kwa maana ahadi zote za Mungu ni ‘ndio’ katika Kristo. Ndio sababu tunatamka ‘Amina’ kwa ajili yake, kwa utukufu wa Mungu. 21 Ni Mungu mwenyewe ambaye anatuwezesha sisi na ninyi kusimama imara katika Kristo. Ametuweka wakfu; 22 ametutia mhuri wake juu yetu, akatupa Roho wake mioyoni mwetu kama uthibitisho.
23 Mungu ni shahidi wangu kwamba niliacha kurudi Korintho kwa kuwahurumia. 24 Hatutaki kuwaamrisha kuhusu imani yenu bali tunafanya kazi pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu; kwa maana mnasimama imara kwa imani.
2 Kwa sababu hiyo, niliamua kwamba sitafanya safari nyingine kuja kuwahuzunisha. 2 Kwa kuwa kama nawahuzunisha, ni nani ali yebaki kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? 3 Ndio sababu nikawaandikia ili nitakapokuja nisihuzunishwe na watu ambao wangenifanya nifurahi. Nilikuwa na uhakika kwenu kwamba furaha yangu ingekuwa furaha yenu nyote. 4 Kwa maana nili waandikia katika dhiki na kutaabika moyoni na kwa machozi mengi. Shabaha yangu haikuwa kuwahuzunisha bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.
Msamaha Kwa Mwenye Dhambi
5 Basi ikiwa mtu ye yote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama alivyowahuzunisha ninyi nyote; sipendi kuweka uzito zaidi kwa upande wenu. 6 Basi adhabu aliyop ewa na wengi inamtosha. 7 Na sasa mnapaswa kumsamehe na kumfariji ili asikate tamaa kabisa kutokana na huzuni kubwa mno aliyo nayo. 8 Kwa hiyo nawasihi mumhakikishie tena kwamba mnampenda. 9 Nili waandikia kuwajaribu ili nione kama mtakuwa watii kwa kila kitu. 10 Mtu ye yote mnayemsamehe na mimi namsamehe. Cho chote nili chosamehe, kama kulikuwa na cha kusamehe, nimesamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo 11 ili shetani asije akatushinda. Kwa maana tunajua mipango yake.
12 Nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo, nilikuta Bwana ameshafungua mlango. 13 Lakini sikuweza kutulia kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Kwa hiyo nikaagana nao nikaenda Makedonia.
Ushindi Ndani Ya Kristo
14 Lakini Mungu ashukuriwe, ambaye hutuongoza katika ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye hututumia sisi kueneza maarifa ya kumjua yeye kila mahali kama harufu nzuri. 15 Kwa Mungu sisi ni kama harufu nzuri ya manukato ya Kristo ambayo inatapakaa mion goni mwa wale wanaookolewa na wale wanaopotea. 16 Kwa wale wanaopotea sisi ni kama harufu ya kifo, lakini kwa wale wanaooko lewa sisi ni harufu iletayo uzima. Ni nani basi awezaye kufanya kazi hiyo? 17 Sisi si kama watu wengine ambao wanauza neno la Mungu wajipatie faida. Lakini kama watu wenye moyo safi, tuliot euliwa na Mungu mbele yake mwenyewe, sisi tunazungumza tukiwa ndani ya Kristo.
Wahudumu Wa Agano Jipya
3 Je mnadhani tunaanza kujisifu tena? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine wafanyavyo? 2 Ninyi wenyewe ni barua yetu ya utambulisho iliyoan dikwa katika mioyo yenu, ijulikane na kusomwa na kila mtu. 3 Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, matokeo ya kazi yetu. Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai.
4 Hili ndilo tumaini tulilo nalo kwa Mungu ndani ya Kristo. 5 Haina maana kwamba sisi tunaweza wenyewe kupima cho chote tuna chofanya, lakini uwezo wetu unatoka kwa Mungu. 6 Ni yeye ali yetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya, ambalo limefanywa, si kwa maandishi, bali kwa Roho. Kwa maana maandishi huleta kifo, lakini Roho huleta Uzima.
Utukufu Wa Agano Jipya
7 Sasa ikiwa huduma iliyoleta kifo, ambayo iliandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata ikawa Waisraeli wal ishindwa kutazama uso wa Musa kwa sababu ya kung’aa kwake, ingawa ulikuwa ukififia, 8 je? Huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? 9 Ikiwa huduma inayowahukumu watu ina utukufu, huduma inayoleta haki si itakuwa na utukufu zaidi? 10 Hakika kwa hali hii, kilichokuwa na utukufu hapo mwanzo, sasa hakina utukufu tena kikilinganishwa na utukufu uliopo. 11 Na kama kilichokuwa kina fifia kilikuja kwa utukufu, utukufu wa kile kinachodumu ni zaidi sana!
12 Kwa hiyo kwa kuwa tunatumaini hili, tuna ujasiri. 13 Sisi si kama Musa, ambaye alifunika uso wake kwa kitambaa ili Waisraeli wasione ule mng’ao ulivyokuwa ukififia na kutoweka. 14 Lakini akili zao zilipumbaa, kwa maana mpaka leo akili zao zinafunikwa na kitambaa wakati agano jipya linaposomwa. Hicho kitambaa hakijaondolewa kwa maana ni Kristo peke yake anayeweza kukiondoa. 15 Hata leo, sheria ya Musa inaposomwa, bado kitambaa kinafunika akili zao. 16 Lakini wakati wo wote mtu anapomgeukia Bwana, “kitambaa kinaondolewa.” 17 Basi, Bwana ni Roho, na mahali alipo Roho wa Bwana pana uhuru. 18 Na sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa tunaonyesha, kama kwenye kioo, utukufu wa Bwana. Nasi tunabadilishwa tufanane naye, kutoka utukufu hadi utukufu wa juu zaidi, ambao unatoka kwa Bwana ambaye ni Roho.
Hazina Za Roho Kwenye Vyombo Vya Udongo
4 Kwa hiyo tukiwa na huduma hii kwa rehema ya Mungu, hatu kati tamaa. 2 Tumekataa njia za siri na za aibu. Hatutumii njia za udanganyifu, wala hatupotoshi neno la Mungu. Badala yake, tunaeleza neno la kweli wazi wazi na kujitambulisha kuwa wa kweli kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu. 3 Na hata kama Injili yetu imefichika, basi imefichika kwa wale wanaopotea. 4 Kwa upande wao, mungu wa dunia hii ametia giza akili za wasioamini, ili wasione mwanga wa Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ana sura ya Mungu. 5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhu biri Yesu Kristo kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6 Kwa kuwa ni Mungu aliyesema, “Nuru iangaze katika giza,” ambaye ameangaza mioyoni mwetu kutupatia nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu ung’aao katika uso wa Kristo.
7 Hata hivyo tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kuonyesha kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, na si kutoka kwetu. 8 Tumegandamizwa kila upande, lakini hatujashindwa. Tumetatanishwa lakini hatukati tamaa; 9 tumeteswa lakini hatuku achwa upweke; tumetupwa chini lakini hatujateketezwa. 10 Tuna chukua katika mwili wetu kifo cha Yesu wakati wote ili uhai wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu. 11 Kwa maana sisi tunaoishi, maisha yetu yako katika hatari ya kifo wakati wote kwa ajili ya Yesu ili uhai wake uweze kuonekana katika miili yetu ya mauti. 12 Kwa hiyo, mauti inatuandama wakati wote, bali uzima unafanya kazi ndani yenu. 13 Maandiko yanasema, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Sisi pia tunaamini, kwa hiyo tunasema. 14 Kwa maana tunajua ya kuwa aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu na kutufikisha sisi na ninyi mbele zake. 15 Haya yote ni kwa ajili yenu, ili kwa kadiri neema ya Mungu inavyowafi kia watu wengi zaidi, wote watoe shukrani kwa utukufu wa Mungu.
16 Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa miili yetu inachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya kila siku. 17 Maana hii dhiki yetu nyepesi na ya muda mfupi inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa uzima wa milele unaozidi sana matatizo haya. 18 Kwa maana hatuweki mawazo yetu kwenye vitu vinavyoonekana bali kwenye vitu visivyoonekana. Maana vile vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini vile visivyoonekana vinadumu milele.
Makao Ya Mbinguni
5 Kwa maana twajua kwamba kama hema hii tunamoishi tukiwa ulimwenguni itaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba ya milele mbinguni, ambayo haikujengwa kwa mikono ya wanadamu. 2 Maana sasa twaugua, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni, 3 kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena tukiwa uchi. 4 Tukiwa bado tunaishi katika hema hii tunaugua na kulemewa, kwa maana hatutaki kukaa bila nguo bali tunatamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili ile hali ya kufa imezwe na uhai. 5 Mungu ndiye aliyetuandaa kwa shabaha hii, naye ametupa Roho wake kama mdha mana, kutuhakikishia mambo yajayo baadaye. 6 Kwa hiyo wakati wote tuna ujasiri mkuu. Tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na nyumbani kwa Bwana. 7 Tunaishi kwa imani na si kwa kuona. 8 Nasema tuna ujasiri na ingekuwa afadhali kuuacha mwili huu tukaishi nyumbani na Bwana. 9 Kwa hiyo, kama tuko nyumbani katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana. 10 Kwa kuwa sisi sote inatubidi kusimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo. Na kila mmoja atapokea mema au mabaya, kulingana na matendo yake alipokuwa katika mwili.
Huduma Ya Upatanisho
11 Kwa hiyo tukijua umuhimu wa kumcha Bwana tunajaribu kuwa vuta watu. Mungu anatufahamu fika. Tunaamini kwamba dhamiri zenu pia zinatufahamu tulivyo. 12 Hatujaribu kujipendekeza kwenu tena, lakini tunataka kuwapeni nafasi mjisifu juu yetu ili muweze kuwajibu hao wanaojisifia mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. 13 Kama tumeehuka, ni kwa ajili ya Mungu; lakini kama tuna akili timamu ni kwa faida yenu. 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo unatusukuma, tunaamini ya kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote kwa hiyo wote walikufa. 15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote ili wote wanaoishi, wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuka tena kwa ajili yao.
16 Tangu sasa hatumtazami mtu ye yote namna ya kibinadamu, ingawaje hapo mwanzo tulimtazama Kristo kwa namna ya kibinadamu. Hatumtazami hivyo tena. 17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja. 18 Haya yote yanatoka kwa Mungu, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo ametupatanisha na mwenyewe, na akatupa huduma ya upatanisho. 19 Ndani ya Kristo Mungu aliupatanisha ulimwengu na yeye mwe nyewe, asiwahesabie watu dhambi zao. Naye ametukabidhi ujumbe huu wa upatanisho.
20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, Mungu anatutumia sisi kuwasihi ninyi. Na sisi tunawasihi ninyi kwa niaba ya Kristo: mpatanishwe na Mungu. 21 Mungu alimfanya yeye ambaye hakujua dhambi, awe dhambi kwa ajili yetu ili ndani yake tupate kuwa haki ya Mungu.
6 Kama wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure . 2 Kwa maana Mungu anasema: “Wakati ufaao niliku sikiliza, na siku ya wokovu nilikusaidia. Tazameni, huu ndio wakati ufaao; leo ndio siku ya wokovu.”
Matatizo Ya Paulo
3 Hatutaki kumwekea mtu ye yote kikwazo ili huduma yetu isionekane kuwa na kasoro. 4 Badala yake, kwa kila njia tunaon yesha ya kuwa sisi ni watumishi wa Mungu kwa kuvumilia: katika taabu, katika misiba, katika shida 5 katika kupigwa, kufungwa gerezani na katika fujo; katika kazi ngumu, kukosa usingizi usiku na katika njaa; 6 katika usafi wa moyo, katika ufahamu, subira na wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli; 7 katika maneno ya kweli na katika uwezo wa Mungu; kwa silaha za haki mkono wa kulia na mkono wa kushoto; 8 katika utukufu na katika aibu, katika sifa na katika lawama; tukiwa wa kweli lakini tukionekana kuwa walaghai; 9 tukiwa maarufu lakini tukihesabiwa kama tusioju likana; tukiwa kama wanaokufa lakini tunaishi; tukiadhibiwa lakini hatuuawi; 10 tukiwa wenye huzuni lakini siku zote tukish angilia; tukionekana maskini lakini tukiwafanya wengi kuwa mata jiri; tukiwa kama wasio na kitu lakini tukiwa na vitu vyote.
11 Tumesema wazi nanyi, ninyi ndugu wa Korintho, na kuweka mioyo yetu wazi kabisa kwenu. 12 Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu usitufikie . 13 Na sasa nasema kama na watoto wangu: ninyi pia fungueni mioyo yenu kabisa kwetu.
Msiambatane Na Wasioamini
14 Msiambatane pamoja na watu wasioamini. Kwa maana kuna uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15 Kuna kuelewana gani kati ya Kristo na shetani? Mwamini ana uhusiano gani na asiyeamini? 16 Kuna uelewano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema, “Nitaishi ndani yao na kutembea kati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkajitenge nao, asema Bwana. Msiguse cho chote kisicho safi; ndipo nitawakaribisha kwangu. 18 Nami nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa vijana wangu na binti zangu, asema Bwana Mwenyezi.”
7 Kwa kuwa tumepewa ahadi hizi wapendwa, basi tujitakase kutokana na kila aina ya uchafu wa mwili na roho, na tufanye bidii kufikia ukamilifu kwa kuwa tunamcha Mungu.
Furaha Ya Paulo
2 Tupokeeni kwa moyo mweupe. Hatujamkosea mtu ye yote, hatu jampotosha mtu ye yote, wala hatujamdhulumu mtu ye yote. 3 Sisemi haya ili kuwahukumu; kwa kuwa, kama nilivyosema mwanzo, tunawath amini kiasi ambacho mpo mioyoni mwetu wakati wote, ikiwa ni kufa pamoja au kuishi pamoja. 4 Ninayo imani kubwa kwenu; ninawaonea fahari kubwa. Nimefarijika sana. Pamoja na taabu zetu zote, furaha yangu haina mfano.
5 Kwa maana hata tulipofika Makedonia, miili yetu haikuwa na amani. Tulitaabishwa kila upande, kwa nje kulikuwa na upinzani na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu. 6 Bali Mungu, ambaye hufariji wenye huzuni, alitufariji kwa kumleta Tito; 7 na si kwa kuwa Tito alifika tu, bali pia kwa kuwa ninyi mlimfariji. Alitueleza juu ya upendo wenu, huzuni yenu na jinsi mlivyonihurumia, kwa hiyo furaha yangu iliongezeka sana.
8 Hata kama barua yangu iliwasikitisha, sasa sijuti kwamba niliiandika ingawa nilikuwa nimejuta. Naona barua yangu iliwahu zunisha, lakini kwa muda mfupi. 9 Lakini sasa ninafurahi, si kwa kuwa mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunika kama Mungu anavyopenda watu wahuzunike na hivyo hatukuwadhuru kwa njia yo yote. 10 Kwa maana huzuni ikitumiwa na Mungu huwafanya watu watubu dhambi zao wapate kuokolewa; nao wanakuwa hawana majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha kifo. 11 Tazameni faida mlizopata kutokana na huzuni hii: bidii mliyo nayo; juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu, na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmethibitisha kuwa hamna hatia katika jambo hilo. 12 Kwa hiyo ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe muone, mbele za Mungu, jinsi mnavyotupenda kwa moyo wote. 13 Kwa hiyo tumefarijika. Pamoja na faraja tuliyopata, tumefu rahi zaidi kwa kuona jinsi Tito alivyofurahi kwa kuwa mlimwondo lea wasi wasi aliokuwa nao. 14 Nilikuwa nimejisifu kwake juu yenu nanyi hamkuniaibisha. Kama jinsi yale niliyowaambia yalivy okuwa ya kweli, hali kadhalika kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumeonekana kuwa kweli pia. 15 Upendo wake kwenu unaongezeka sana anapokumbuka jinsi mlivyokuwa watii na jinsi mlivyompokea kwa hofu na kutetemeka. 16 Nafurahi kwa sababu nina imani nanyi kabisa.
Kutoa Kwa Ukarimu
8 Tunapenda mfahamu ndugu zetu, kuhusu neema ambayo Mungu amewapa makanisa ya Makedonia. 2 Pamoja na majaribu makali na taabu walizopata, furaha yao na umaskini wao mkuu zimezaa utajiri wa ukarimu. 3 Ninashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya uwezo wao hata na zaidi ya uwezo wao. 4 Kwa hiari yao wenyewe, walitusihi wapewe nafasi ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watu wa Mungu. 5 Na hawakufanya tulivyotazamia bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana kwanza na ndipo wakajitoa kwetu, kufuatana na mapenzi ya Mungu. 6 Kwa hiyo tulimwagiza Tito, kwa kuwa ndiye aliyeanzisha jambo hili, akamilishe kazi hii ya neema pia kwa upande wenu. 7 Basi, kama mlivyo mbele sana katika yote: katika imani, katika kutamka, katika juhudi na katika kutupenda, hakik isheni kuwa mnakuwa wa kwanza pia katika neema hii ya kutoa.
8 Siwapi amri, lakini nawaonyesha jinsi wengine walivyo tay ari kutoa ili kupima ukweli wa upendo wenu. 9 Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ingawa alikuwa tajiri, alikubali kuwa maskini kwa ajili yenu, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri. 10 Ushauri wangu kuhusu jambo hili ni huu. Ni vyema mkamilishe sasa jambo ambalo mlinia na mkaanza kulifanya tangu mwaka jana 11 ili wepesi wenu katika kunia ulin gane na kumaliza kwenu kutoa kwa kadiri ya mlicho nacho. 12 Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kufuatana na kile mtu alicho nacho, si kufuatana na kile ambacho mtu hana. 13 Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka bali pawe na uwiano. 14 Kwa wakati huu wingi wa vitu mlivyonavyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao wakiwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu. 15 Ndipo patakuwa na usawa, kama maandiko yanavyosema, “Aliyekusanya kwa wingi, hakubakiza kitu, na aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.”
Tito Anatumwa Korintho
16 Tunamshukuru Mungu ambaye amempa Tito moyo wa kuwajali ninyi kama mimi ninavyowajali. 17 Si kwamba amekubali ombi letu tu, bali anakuja kwenu akiwa na ari na kwa hiari yake mwenyewe. 18 Pamoja naye tunamtuma ndugu ambaye anasifiwa na makanisa yote kwa huduma yake ya kuhubiri Injili. 19 Zaidi ya hayo, amechagu liwa na makanisa asafiri nasi kupeleka matoleo haya. Hii ni huduma ambayo tunafanya kwa utukufu wa Bwana na pia kuonyesha nia yetu ya kuwasaidia wengine. 20 Tumenuia kwamba mtu ye yote asiwe na sababu ya kutulaumu kuhusu jinsi tunavyosima mia matoleo haya ya ukarimu. 21 Tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunafanya haki machoni pa Bwana na machoni penu, na wala si kama sisi tuonavyo vyema. 22 Pamoja na hawa, tunamtuma ndugu yetu ambaye tumempima mara nyingi tukamwona kuwa wa kweli na mwenye juhudi, hasa zaidi sana kwa kuwa ana imani kubwa kwenu. 23 Kumhusu Tito, yeye ni mwenzangu na mfanyakazi pamoja nami kwa ajili yenu. Kuhusu hawa ndugu wengine, wao ni wawakilishi wa makanisa, nao wanamletea Kristo utukufu. 24 Kwa hiyo, waonyesheni hawa ndugu upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, ili makanisa yote yapate kuona.
Wasaidieni Wakristo Wenzenu
9 Hakuna sababu ya kuwaandikia kuhusu msaada unaotolewa kwa ajili ya watu wa Mungu, 2 kwa kuwa ninajua mlivyo tayari kutoa, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili yenu kwa watu wa Makedonia, nikiwaambia kuwa ninyi wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana. Ari yenu imewachochea wengi wao kuanza kutoa. 3 Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusije kukawa ni maneno matupu, bali muwe tayari kama nilivyosema mko tayari. 4 Isije ikawa nitakapokuja na watu wa Makedonia nikute hamko tayari niaibike, na ninyi zaidi, kwa kuwa nilishasema mko tayari. 5 Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kabla yangu, wafanye mipango yote ya matoleo ya zawadi mliyoahidi ili iwe tayari, si kama mchango wa kulazim ishwa bali kama zawadi ya hiari.
6 Kumbukeni kwamba, mtu anayepanda mbegu chache, atavuna mazao machache; na mtu anayepanda mbegu nyingi atavuna mazao mengi. 7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa kusita au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu anapenda mtu anayetoa kwa moyo. 8 Na Mungu anaweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili kila wakati muwe na kila kitu kwa kiasi cha kutosha na ziada kwa ajili ya kila kazi njema. 9 Kama Maandiko yanavyosema, “Yeye hutapanya kila mahali kuwapa maskini, haki yake hudumu milele.” 10 Na Mungu ambaye ndiye humpa mkulima mbegu za kupanda, na mkate kwa chakula, atawapa na kuzidisha mbegu mnazohitaji na kuziwezesha kukua zitoe mazao ya matendo mema ya haki. 11 Atawa fanya kuwa matajiri kwa kila hali ili mpate kuwa wakarimu kila wakati na kwa mchango wenu wa hiari kupitia kwetu, wengi wapate kumshukuru Mungu. 12 Huduma hii mnayofanya si kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu wa Mungu, bali utaleta mbubujiko wa shukrani nyingi kwa Mungu tu. 13 Kwa kutoa kwenu, mtakuwa mnatoa uthibitisho wa uhakika wa imani yenu. Ndipo watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu unaoambatana na kukiri kwenu kwa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wa mchango wenu kwao na kwa wen gine wote. 14 Nao watawaombea kwa upendo mwingi kwa ajili ya neema kuu mliyopewa na Mungu. 15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi hii isiyoelezeka.
Paulo Atetea Huduma Yake
10 Mimi Paulo nawaandikia nikiwasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo, mimi ambaye ni mpole ninapokuwa pamoja nanyi, lakini mwenye ujasiri nikiwa mbali nanyi! 2 Nawaomba msinifanye niwe mkali nitakapofika kwenu, kama ninavyotarajia kuwa mkali kwa watu fulani, ambao wanadhani kwamba nafuata kawaida za dunia katika mwenendo wangu. 3 Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani kama watu wa ulimwengu. 4 Silaha zetu si za kidunia, bali silaha zetu zina nguvu ya kimungu iwezayo kubomoa ngome. 5 Tunaharibu hoja na mabishano yaliyo kinyume cha kumjua Mungu. Tunateka mawazo yote na kuyafanya yamtii Kristo, 6 na tutakuwa tayari kuadhibu uasi wo wote baada ya kuhakikisha utii wenu. 7 Tazameni vizuri mambo yaliyo mbele ya macho yenu. Kama mtu ye yote anaamini kuwa yeye ni wa Kristo, basi ajiangalie tena, kwa maana na sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo. 8 Kwa sababu hata kama tunajivunia mno madaraka tuliyo nayo, ambayo Bwana ametupatia kwa ajili ya kuwa jenga na sio kuwagandamiza, sitaona haya kuyatumia. 9 Sitaki ionekane kama nataka kuwatisha kwa barua zangu. 10 Kwa maana wengine wanasema, “Barua zake zina uzito na ni kali lakini mtu mwenyewe ni mdhaifu na kuzungumza kwake hakuvutii.” 11 Watu kama hao wajue ya kuwa, wanavyotuona katika barua tukiwa hatupo nanyi, ndivyo tulivyo, na ndivyo tutakavyofanya tutakapo kuwa pamoja nanyi. 12 Hatuthubutu kujiweka kwenye kundi moja au kujilinganisha na hao wanaojiona kuwa wao ni wa maana sana. Wana pojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, wanaonyesha ya kuwa hawana busara. 13 Lakini sisi hatujajivuna kupita kiasi, bali majivuno yetu yatakuwa katika mipaka ambayo Mungu ametuwekea, na mipaka hiyo inawafikia hata na ninyi. 14 Kwa maana hatupiti mipaka tunapowajumlisha katika huduma yetu kwa sababu tulikuwa wa kwanza kuwaletea Injili ya Kristo. 15 Hatupiti mipaka na kujivunia kazi ya watu wengine. Lakini matumaini yetu ni kwamba, imani yenu inavyozidi kukua, huduma yetu kwenu itaendelea kupanuka, 16 ili tuweze kuhubiri Injili hata nchi zilizopakana nanyi, bila kujivu nia kazi iliyokwisha fanywa katika sehemu ya mtu mwingine. 17 “Anayejivuna na ajivune katika Bwana.” 18 Kwa maana sio mtu anayejisifu ambaye anapata kibali, bali ni mtu ambaye Bwana anamsifu.
Paulo Na Mitume Wa Uongo
11 Natumaini mtanivumilia hata wakati ninapokuwa mjinga kidogo. Tafadhali nivumilieni! 2 Nawaonea wivu wa kimungu kwa kuwa mimi niliwaposea Kristo, ili niwatoe kama mwanamwali anavy otolewa kwa mume mmoja akiwa hana dosari. 3 Lakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa na ujanja wa yule nyoka, huenda akili zenu zimepotoshwa, mkaacha upendo wenu safi na wa kweli kwa Kristo. 4 Kwa sababu kama mtu akija akawahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au kama mkikubali Injili nyingine ambayo si ile mliyoikubali, mnaipokea kwa moyo mmoja! 5 Lakini sidhani ya kuwa mimi ni mdogo sana nikilinganishwa na hao ‘mitume wakuu’. 6 Hata kama mimi si mzungumzaji hodari, lakini ni hodari katika maarifa. Jambo hili ni dhahiri kwenu.
7 Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha mbele yenu na kuwainua ninyi, kwa kuwa niliwahubiria Injili ya Mungu pasipo gharama yo yote kwa upande wenu? 8 Nilipokea msaada kutoka kwa makanisa men gine, niliwanyang’anya wao ili niweze kuwahudumia ninyi. 9 Na nilipokuwa nanyi, nikipungukiwa na cho chote, sikuwa mzigo kwa mtu ye yote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walitosheleza mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia na nitaendelea kujizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yo yote. 10 Na kama ukweli wa Kristo ulivyo ndani yangu, hakuna mtu ye yote katika Akaya nzima atakayenizuia kujivunia jambo hili. 11 Kwa nini? Mnadhani ni kwa kuwa siwa pendi? Mungu anajua ya kuwa nawapenda!
12 Nami nitaendelea kufanya hivi ili kuwazima wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia. 13 Watu kama hao ni manabii wa uongo, ni wafany akazi wadanganyifu ambao wanajifanya kuwa mitume wa Kristo. 14 Na hii si ajabu, kwa sababu hata shetani hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. 15 Kwa hiyo si ajabu kama malaika wake shetani nao wanajigeuza waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao.
Paulo Anajivunia Mateso Yake
16 Nasema tena, mtu ye yote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata kama mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. 17 Ninayosema sasa, kwa majivuno, nasema kama mjinga na wala si kwa mamlaka ya Bwana. 18 Kwa sababu wengine wanajivunia mambo ya kidunia, basi na mimi nitaji sifu. 19 Ninyi mnawavumilia wajinga kwa kuwa mna hekima mno! 20 Tena mnavumilia hata kama mtu anawafanya watumwa au anawany onya na kuwadanganya au anajigamba mbele yenu au anawapiga makofi usoni. 21 Naona aibu kukubali kwamba sisi ni wadhaifu kiasi ambacho hatuwezi kufanya mambo kama hayo. Lakini cho chote ambacho mtu anathubutu kujivunia, sasa nasema kama mjinga, mimi pia naweza kuthubutu kujivunia.
22 Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. 23 Wao ni watumishi wa Kristo? Mimi ni mtumishi bora zaidi, nasema kama kichaa. Nimefanya kazi zaidi, nimefungwa gerezani zaidi, nimechapwa viboko visivyo na hesabu, na mara nyingi nilikuwa karibu kufa. 24 Mara tano nimechapwa viboko aro baini kupungua kimoja na Wayahudi. 25 Nimechapwa kwa chuma mara tatu. Nimepigwa mawe mara moja. Mara tatu nimevunjikiwa na meli. Nimeelea baharini usiku kucha na mchana kutwa. 26 Katika safari zangu nyingi, nimekuwa katika hatari za mafuriko, hatari za wany ang’anyi, hatari kutoka kwa Wayahudi wenzangu na hatari kutoka kwa watu wa mataifa mengine; nimekuwa katika hatari mijini, nyikani, baharini na katika hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 27 Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, siku nyingi nimekuwa bila usingizi, nimekuwa na njaa na kiu, mara nyingi nimekuwa bila chakula, katika baridi na bila nguo. 28 Na ukiacha mambo mengine nimelemewa na wasiwasi juu ya makanisa yote. 29 Je, ni nani ana kuwa mdhaifu nisijisikie mdhaifu? Nani anashawishiwa kutenda dhambi nisijisikie nachomwa na uchungu?
30 Nikilazimika kujisifu, basi nitajisifia yale mambo yanay oonyesha udhaifu wangu. 31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye amebarikiwa daima, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. 32 Kule Dameski, gavana aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliu linda mji wa Dameski ili wapate kunikamata, 33 lakini nilish ushwa kwa kapu kubwa kupitia katika dirisha ukutani nikaepuka kukamatwa.
Maono Ya Paulo Na Mwiba Aliokuwa Nao
12 Inanibidi nijisifu. Ingawa hakuna faida, nitawaeleza juu ya maono na mafunuo niliyopata kutoka kwa Bwana. 2 Namfahamu mtu aliyekuwa ndani ya Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alijikuta katika mbingu ya tatu. Kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. 3 Na ninafahamu ya kuwa huyu mtu alijikuta yuko Paradiso, kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. 4 Naye alisikia mambo ambayo hayawezi kusimuliwa, ambayo mtu hawezi kuyatamka. 5 Kwa niaba ya mtu huyu nitajisifu, lakini kwa ajili yangu mwenyewe sitajisifu isipokuwa kuhusu udhaifu wangu. 6 Lakini ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga kwa maana nitakuwa nasema kweli. Ila najizuia, ili mtu ye yote asije akaniona mimi kuwa bora zaidi kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema.
7 Na ili nisijione bora kuliko nilivyo, kutokana na mafunuo haya makuu, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mtumishi wa she tani, ili anitese. 8 Nimemsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu. 9 Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uwezo wangu unakamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu ili uwezo wa Kristo ukae juu yangu. 10 Basi, kwa ajili ya Kristo, naridhika na udhaifu, mat usi, taabu, mateso na maafa; kwa maana ninapokuwa mdhaifu ndipo nina nguvu.
Upendo Wa Paulo Kwa Wakorintho
11 Nimekuwa mjinga, lakini ninyi mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ninyi ndio ambao mngenisifu. Kwa sababu sikuwa wa chini kuliko hawa “mitume wakuu,” hata ingawa mimi si kitu. 12 Mambo yanayomtambulisha mtume wa kweli, yaani ishara, miujiza na maaj abu, yalifanywa miongoni mwenu kwa uvumilivu wote. 13 Je, kuna kitu ambacho hamkupewa sawa na wengine, isipokuwa mimi sikuwa mzigo kwenu? Nisameheni kwa kosa hili.
14 Na sasa niko tayari kuwatembelea kwa mara ya tatu, nami sitahitaji msaada wenu kwa sababu sitaki mnipe mali yenu, ninaowahitaji ni ninyi. Kwa kuwa si sawa watoto waweke akiba kwa ajili ya wazazi wao bali wazazi waweke akiba kwa ajili ya watoto wao. 15 Nitafurahi kutumia kila nilicho nacho hata mwili wangu pia, kwa ajili yenu. Je kama nawapenda zaidi, mtanipenda kidogo tu kwa sababu hiyo? 16 Hata kama mnakubali kwamba sikuwa mzigo kwenu, wengine watasema nilikuwa mjanja nikawanasa kwa hila. 17 Je, niliwahi kuwadanganya kupitia mmojawapo wa hao watu nil iowatuma kwenu? 18 Nilimsihi Tito aje kwenu nikamtuma ndugu mwingine waje pamoja. Je, Tito aliwatoza cho chote? Je, sisi sote hatukutenda kwa kuongozwa na Roho mmoja na kufuata njia moja?
19 Pengine mnafikiri wakati wote kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu. Sisi tunajitetea mbele ya Mungu katika Kristo, na yote haya ni kwa nia ya kuwajenga ninyi, wapendwa wetu. 20 Kwa maana nina hofu kwamba nitakapokuja nitawakuta hamko kama ambavyo ningependa muwe, na ninyi mtakuta siko kama ambavyo mngependa niwe. Nina hofu kwamba kati yenu huenda kuna ugomvi, wivu, hasira, ubinafsi, uzushi, usengenyaji, majivuno na machafuko. 21 Nina hofu kuwa nitakapokuja tena Mungu wangu ata ninyenyekeza mbele yenu, na huenda nikaomboleza kuhusu wengi wenu ambao walitenda dhambi na hawajatubu na kuacha hayo matendo machafu, uasherati na ufisadi ambao walikuwa wakitenda.
Maonyo Ya Mwisho Na Salamu
13 Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuja kwenu. “Shitaka lo lote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” 2 Niliwaonya wale waliotenda dhambi na wengine wote, na sasa nawaonya tena nikiwa siko nanyi kama nilivyowaonya wakati nili powatembelea mara ya pili, kwamba nikija tena sitawahurumia. 3 Kwa kuwa mnataka kupata ushahidi kuwa Kristo anazungumza kupi tia kwangu, hiyo itakuwa ushahidi wangu. Yeye si mdhaifu anapow ashughulikia bali ni mwenye nguvu ndani yenu. 4 Kwa maana alisu lubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Hali kadhalika sisi ni wadhaifu ndani yake, lakini kwa nguvu za Mungu tutaishi pamoja naye ili tuweze kuwahudumia.
5 Jichunguzeni mwone kama mnashika imani yenu. Jipimeni. Je, hamtambui ya kuwa Kristo yuko ndani yenu, au pengine mmeshindwa kufikia kipimo hicho? 6 Natumaini mtagundua ya kuwa sisi hatu kushindwa kufikia kipimo hicho. 7 Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda jambo lo lote ambalo ni kosa; si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaone kana kuwa tumeshindwa. 8 Kwa maana hatuwezi kufanya lo lote kupinga kweli, bali kuithibitisha kweli. 9 Tunafurahi wakati wo wote sisi tunapokuwa wadhaifu na ninyi mkawa wenye nguvu. Tuna choomba ni kwamba mpate kukomaa katika imani. 10 Nawaandikieni haya wakati nikiwa mbali ili nitakapokuja nisiwe na sababu ya kuwa mkali katika kutumia madaraka ambayo Bwana amenipa kuwa jenga, na sio kuwagandamiza. 11 Hatimaye ndugu zangu, kwaherini. Sahihisheni mwenendo wenu, pokeeni ushauri wangu; sikilizaneni ninyi kwa ninyi; kaeni kwa amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. 13 Watakatifu wote wanawasalimu.
1 Kutoka kwa Paulo, mtume niliyetumwa, si kutoka kwa watu wala sikuchaguliwa na mwanadamu, bali nimetumwa na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu. 2 0 Nawahakikishieni mbele za Mungu kuwa ninayowaandikieni si uongo.
3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, 4 ambaye alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa kutoka katika nyakati hizi za uovu. 5 Yeye apewe utukufu milele na milele. Amina.
6 Nashangaa kuona kwamba mnamwacha upesi hivyo yule aliye waita kwa neema ya Kristo mkaanza kufuata Injili nyingine. 7 Ukweli ni kwamba hakuna Injili nyingine, ila nafahamu kuwa wako watu wanaowavuruga, ambao wanataka kuipotosha Injili ya Kristo. 8 Lakini hata ikiwa ni sisi au ni malaika atokaye mbinguni, kama mtu akiwahubiria Injili ambayo ni tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo na alaaniwe. 9 Kama tulivyokwisha sema kabla, sasa nasema tena, kwamba mtu ye yote atakayewahubiria Injili tofauti na ile mliyokwishaipokea, basi mtu huyo na alaaniwe.
10 Je, sasa mimi nataka nipate upendeleo kutoka kwa bina damu au kutoka kwa Mungu? Au nataka niwapendeze watu? Kama ningekuwa najaribu kuwapendeza watu, nisingekuwa mtumishi wa
Wito Wa Paulo
11 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba Injili niliyo wahubi ria siyo Injili ya binadamu. 12 Kwa maana mimi sikuipokea Injili kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali nili pata mafunuo moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo. 13 Ninyi mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi; jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu na kujaribu kuliangamiza. 14 Nami niliwashinda wengi miongoni mwa Wayahudi wenzangu kwa maana nilikuwa nimejawa na juhudi ya kushika mapo keo ya baba zetu. 15 Lakini yeye aliyenichagua hata kabla sijazaliwa na akaniita kwa neema yake, 16 alipopenda kumdhihiri sha Mwanae kwangu ili nimhubiri miongoni mwa watu wa mataifa, sikushauriana na mtu ye yote. 17 Sikwenda kwanza Yerusalemu kuonana na wale waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda Arabuni, ndipo nikarudi Dameski. 18 Kisha baada ya miaka mitatu nilikwenda Yerusalemu kuo nana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano. 19 Lakini siku waona wale mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 21 Baadaye nilikwenda sehemu za Siria na Kilikia. 22 Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa wakristo wa makanisa ya huko Uyahudi. 23 Ila walisikia wengine wakisema, “Yule mtu ambaye zamani alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akitaka kuiangamiza.” 24 Kwa hiyo wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
Paulo Akubaliwa Na Mitume
2 Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nilikwenda tena Yeru salemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito ili awe pamoja nami. 2 Nilikwenda kwa sababu nilikuwa nimefunuliwa na Mungu, kwamba nikawaeleze kwa faragha wale waliokuwa viongozi, Injili ninayohubiri kwa watu wa mataifa mengine. Nilifanya hivyo ili kazi yangu niliyokwisha fanya na hii ninayofanya sasa isije ikawa bure. 3 Hata hivyo Tito ambaye alikuwa ni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa. 4 Lakini walikuwepo ndugu wengine wa uongo ambao walikuja kwa siri kupeleleza uhuru tulio nao katika Kristo Yesu, ili waturudishe kwenye utumwa wa sheria. 5 Sisi hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Injili uendelee kutunzwa kwa ajili yenu. 6 Lakini wale ambao walionekana kuwa viongozi wao, mimi sijui wala sijali kama walikuwa na vyeo gani, kwa sababu Mungu haangalii cheo cha mtu; nasema kwamba hao watu hawakuongezea cho chote katika ujumbe wangu. 7 Badala yake walitambua kwamba Mungu alikuwa amenipa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengi ne kama vile Petro naye alivyotumwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi. 8 Kwa maana ilikuwa dhahiri kwamba Mungu aliyemwezesha Petro kuwa mtume kwa Wayahudi ndiye aliyekuwa akifanya kazi katika huduma yangu kama mtume kwa watu wa mataifa mengine. 9 Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, ambao walikuwa nguzo za kanisa, walipotambua kwamba Mungu alikuwa amenijalia neema yake, walitushika mikono, mimi na Barnaba, kama ishara ya ushirikiano wetu. Walikubaliana kwamba sisi twende kwa watu wa mataifa mengine na wao waende kwa Wayahudi. 10 Walichotuomba ni kwamba katika huduma yetu tuende lee kuwasaidia maskini; jambo ambalo nimekuwa nikijitahidi kufa nya.
Paulo Anampinga Petro
11 Lakini Petro alipofika Antiokia, mimi nilimpinga hadhar ani kwa kuwa alikuwa amekosea. 12 Kwa sababu kabla ya watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini baada ya hao watu kufika ali ji tenga, akaacha kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuwaogopa wale wa kundi la tohara. 13 Pia Wayahudi wengine wal iungana naye katika unafiki huu, hata Barnaba naye akashawishika kuwaunga mkono.
14 Nilipoona kwamba msimamo wao kuhusu ukweli wa Injili hau kuwa wazi, nilimwambia Petro mbele za watu wote, “Ikiwa wewe uliye Myahudi unaishi kama watu wa mataifa, na huishi kama Myahudi, unawezaje kuwalazimisha watu wa mataifa mengine waishi kama Wayahudi?” Habari Njema Aliyohubiri Paulo
15 Sisi tulio Wayahudi wa kuzaliwa na sio watu wa mataifa ‘wenye dhambi,’ 16 tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki kwa kutii sheria. 17 Lakini ikiwa sisi katika jitihada ya kuhesabiwa haki katika Kristo, bado tunaonekana tun gali wenye dhambi, je, hii ina maana kwamba Kristo amekuwa mwene zaji wa dhambi? La hasha! 18 Lakini ikiwa mimi nina jenga tena kile ambacho nimekwisha bomoa, basi ninadhihirisha kwamba mimi ni mvunja sheria. 19 Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria, ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. 20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake kwa ajili yangu. 21 Siwezi nikadharau neema ya Mungu; kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa kutimiza sheria, basi Kristo alikufa bure.
Kuhesabiwa Haki Kwa Njia Ya Imani
3 Ninyi Wagalatia wajinga! Nani aliyewaloga? Yesu Kristo alielezwa wazi wazi mbele yenu kwamba alisulubiwa. 2 Nataka mni jibu swali moja: je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kutimiza sheria au kwa kuamini mliyosikia? 3 Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Baada ya kuanza na Roho wa Mungu, sasa mnataka kuwa wakamilifu kwa uwezo wenu wenyewe? 4 Je, mateso yote yaliyowapata hayakuwa faa kitu? Kweli yalikuwa bure? 5 Je, Mungu anawapa Roho wake na kufanya miujiza kati yenu kwa sababu mnatii sheria au kwa sababu mnaamini Injili mliyosikia?
6 Tazameni mfano wa Abrahamu: “Yeye alimwamini Mungu, na Mungu alimhesabu kuwa mtu mwenye haki.” 7 Kwa hiyo mnaona kwamba watu wanaomwamini Mungu ndio watoto halisi wa Abrahamu. 8 Na Maandiko yalitabiri mambo ya baadaye, kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa mengine kwa njia ya imani. Kwa hiyo Maandiko yalitangulia kumtangazia Abrahamu kwa kutamka, “Kwa ajili yako mataifa yote yatabarikiwa.” 9 Hivyo basi, walio na imani wana barikiwa pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa mtu wa imani.
Sheria Na Laana
10 Wote wanaotegemea kutimiza sheria, wako chini ya laana. Kwa sababu Maandiko yanasema, “Mtu ye yote asiyeshika na kufu ata mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, amelaani wa.” 11 Ni wazi kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kutimiza sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” 12 Lakini sheria haitegemei imani kwa maana, “Atimizaye maagizo ya sheria ataishi kwa sheria.” 13 Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kuchukua laana hiyo kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Mtu anayetundikwa msalabani amelaaniwa.” 14 Lakini alitukomboa ili baraka aliyo pewa Abrahamu iwafikie na watu wa mataifa mengine kwa njia ya Yesu Kristo. Na kwa kutegemea imani, sisi tupate kupokea Roho wa
Sheria Na Ahadi
15 Ndugu zangu, napenda nitoe mfano kutoka katika maisha ya kila siku. Hakuna mtu anayetengua wasia wa mtu au kuuongezea ukishatiwa sahihi. 16 Abrahamu alipewa ahadi yeye pamoja na mzawa wake. Lakini Maandiko hayasemi, “Na wazao wake,” Kwa maana ya wengi, bali yanasema, “Na mzawa wake,” yaani mmoja, ambaye ndiye Kristo. 17 Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka mia nne na thelathini baadaye, haiwezi kutangua agano lililothibitishwa na Mungu na kulifanya duni. 18 Kwa maana, kama urithi wetu unategemea sheria, basi hauwezi tena kutegemea ahadi ya Mungu. Lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi. 19 Kwa nini basi ipo sheria? Sheria iliwekwa kwa ajili ya uhalifu hadi atakapokuja yule wa uzao wa Abrahamu, ambaye ali tajwa katika ahadi hiyo. Sheria ililetwa na malaika kwa mkono wa mjumbe. 20 Lakini mjumbe huwakilisha zaidi ya mtu mmoja; bali
Lengo La Sheria
21 Je, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La, sivyo! Kama ingetolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki mbele za Mungu ingepatikana kwa kutimiza sheria. 22 Lakini Maan diko yanasema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi, kwa sababu hiyo, ile ahadi inatolewa tu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo na wanaoipokea ni wale wenye imani.
23 Kabla imani haijakuwepo tulikuwa tumefungwa chini ya sheria, mpaka imani ifunuliwe. 24 Kwa hiyo, sheria ilikuwa kama kiongozi wa kutufikisha kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 Lakini sasa kwa kuwa imani imekuja hatusimamiwi tena na sheria.
Copyright © 1989 by Biblica