Bible in 90 Days
1 Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wath esalonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. Tuna watakieni neema na amani.
Shukrani Kwa Imani Ya Wathesalonike
2 Tunamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu wote na kuwaom bea pasipo kukoma. 3 Tunakumbuka daima mbele za Mungu Baba yetu, kazi yenu inayotokana na imani, juhudi yenu kubwa katika upendo, na uvumilivu wenu unaotokana na tumaini mlilonalo kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 4 Ndugu zetu mnaopendwa na Mungu, tunafahamu kwamba Mungu amewachagua 5 kwa maana Injili yetu haikuwajia kwa maneno matupu bali ilidhihirishwa kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, mkawa na uhakika kamili. Ninyi mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi kwa faida yenu. 6 Nanyi mkatuiga sisi, mkamuiga na Bwana; kwa maana mlilipokea neno kwa furaha mliyopewa na Roho Mtakatifu ingawa mlipata mateso makali. 7 Kwa hiyo mkawa kielelezo kwa waamini wote wa Makedonia na Akaya.
8 Maana neno la Mungu limeenea kutoka kwenu, sio mpaka Make donia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imejulika na mahali pote. Kwa hiyo hatuhitaji kusema lo lote kuhusu imani yenu; 9 kwa maana wao wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea. Wanasimulia jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha ibada za sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli; 10 na kumngoja Mwanae kutoka mbin guni, ambaye alimfufua kutoka kwa wafu, yaani Yesu. Yeye anatu komboa kutoka katika ghadhabu ijayo.
Huduma Ya Paulo Huko Thesalonike
2 Wapendwa, ninyi wenyewe mnajua kwamba tulipokuja kwenu haikuwa bure. 2 Kama mjuavyo tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu, tulikuwa na uja siri wa kuwaambia Habari Njema ya Mungu pamoja na kwamba uliku wapo upinzani mkali. 3 Ujumbe wetu kwenu hautokani na kutokujua au nia mbaya au udanganyifu. 4 Kinyume chake, tunahubiri kama watu tuliopata kibali cha Mungu tukakabidhiwa Habari Njema. Nia yetu si kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu anayejua mawazo ya mioyo yetu. 5 Mnafahamu kuwa hatukutumia maneno matamu ya kujipendekeza kwenu, wala hatukutumia hila kuficha tamaa ya kujipatia fedha, kwa maana Mungu ni shahidi yetu. 6 Hatukutafuta kupata sifa kutoka kwa mwanadamu ye yote, kwenu au kwa mtu mwin gine.
7 Kama mitume wa Kristo tungaliweza kudai heshima kutoka kwenu, lakini tulikuwa wapole kwenu kama mama anayetunza watoto wake wadogo. 8 Tuliwapenda sana, kiasi kwamba tulifurahi kushiri kiana nanyi, si Habari Njema ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa maana tuliwathamini mno. 9 Ndugu zetu, bila shaka mnakumbuka juhudi yetu na kutaabika kwetu. Tulifanya kazi usiku na mchana kusudi tusiwe mzigo kwa mtu ye yote wakati tunawahubiria Habari Njema ya Mungu. 10 Ninyi ni mashahidi na Mungu pia ni shahidi yetu kwamba tulikuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama kati yenu mlioamini. 11 Maana mnajua jinsi tulivyowatendea kama baba awa tendeavyo watoto wake: 12 tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwa himiza muishi maisha yampendezayo Mungu, ambaye anawaita mshiriki ufalme wake na utukufu.
13 Nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma pia kwa sababu mlipo lipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu. Bali mlilipokea kama lilivyo hasa, yaani, neno la Mungu, ambalo linafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. 14 Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu ndani ya Kristo Yesu yaliyoko Yudea. Mliteswa na watu wenu wenyewe kama vile makanisa hayo yalivyoteswa na Wayahudi. 15 Wao walimwua Bwana Yesu na manabii, wakatufukuza na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu na tena ni adui wa kila mtu kwa kuwa 16 wanajaribu kutuzuia tusiwahubirie watu wa mataifa mengine ujumbe ambao utawaokoa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia.
Paulo Atamani Kuwaona Wathesalonike
17 Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa muda, ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu si kwa moyo, tulizidi kwa hamu kubwa kufanya kila jitihada tuonane uso kwa uso. 18 Maana tulitaka kuja huko, hasa mimi Paulo, nilijaribu zaidi ya mara moja, lakini shetani akatuzuia. 19 Kwa maana ni nini tumaini letu, furaha yetu au taji yetu ya utukufu mbele za Bwana Yesu Kristo atakapokuja? Si ninyi? 20 Hakika ninyi ndio utukufu wetu na furaha yetu.
Timotheo Atumwa Kwenda Thesalonike
3 Hatimaye tuliposhindwa kuvumilia zaidi, tuliona afadhali tubaki Athene peke yetu. 2 Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika kuieneza Habari Njema ya Kristo, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo 3 ili asije mtu akababaishwa na mateso haya. Kama mjuavyo, tumepangiwa mateso. 4 Hata tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa, na kama mjuavyo ndivyo ilivyokuwa. 5 Ndio maana niliposhindwa kuvumilia nilituma mtu ili nifahamu msimamo wenu katika imani. Niliogopa kuwa pengine yule mjaribu shetani alikuwa amewajaribu na kwamba pengine juhudi yetu kwenu ingekuwa ni bure.
Taarifa Ya Timotheo
6 Lakini sasa Timotheo amekwisha rejea kutoka kwenu na ameleta taarifa nzuri kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuam bia kwamba mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna hamu siku zote kutuona kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaona. 7 Kwa sababu hiyo ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa ajili yenu, kutokana na imani yenu. 8 Maana sasa hakika tunaishi kwa kuwa ninyi mmesimama imara katika Bwana. 9 Tutawezaje kumshu kuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu? 10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tuwezeshwe kuwaona tena na kuwapa tieni kile ambacho bado kinapungua katika imani yenu.
11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kuja kwenu. 12 Bwana na awawezeshe ninyi kupendana zaidi na zaidi na kuwapenda watu wote kama sisi tunav yowapenda ninyi. 13 Tunamwomba awaimarisheni mioyo ili msiwe na lawama bali muwe watakatifu mbele za Mungu Baba yetu, wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake wote.
Maisha Yanayompendeza Mungu
4 Hatimaye, ndugu wapendwa, tuliwaelekeza namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli ndivyo mnavyoishi. Sasa tunawaombeni na kuwasihi katika jina la Bwana Yesu, mwendelee kufanya hivyo zaidi na zaidi. 2 Mnafahamu maelekezo tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Yesu.
3 Mungu anapenda ninyi muwe watakatifu, mjiepushe na maisha ya zinaa; 4 na kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuishi na mke wake mwenyewe kwa njia ya utakatifu na heshima; 5 si kwa kutawaliwa na tamaa mbaya kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu. 6 Katika jambo hili mtu asije akamkosea au kumdanganya ndugu yake. Kama tulivy okwisha kuwaambia na kuwaonya, Bwana atawaadhibu watu watendao dhambi zote za aina hii. 7 Kwa maana Mungu hakutuita tutawaliwe na mawazo machafu, bali tuishi maisha ya utakatifu. 8 Kwa hiyo mtu ye yote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
9 Hatuna haja ya kuwaandikia kuhusu upendo kati ya ndugu, kwa maana ninyi wenyewe mmekwisha kufundishwa na Mungu mpendane ninyi kwa ninyi 10 na kwa kweli mnawapenda ndugu wote wa Makedonia yote. Hata hivyo, ndugu zetu, tunawasihi mwendelee kuwapenda zaidi sana. 11 Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akishughulikia mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaambia. 12 Kwa njia hii maisha yenu ya kila siku yatawaletea sifa kutoka kwa watu wasioamini na wala hamtahi taji kuwategemea watu wengine.
Kufufuliwa Kwa Wafu Na Kuja Kwa Bwana
13 Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. 14 Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake. 15 Kama alivyosema Bwana mwenyewe, tunawaambieni kuwa sisi ambao tuko hai bado, tutakaokuwa hai mpaka Bwana arudi, kwa hakika hatutawatangulia wale waliokwisha kufa.
16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu; na wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu tukutane na Bwana angani. Na hivyo tutakuwa na Bwana milele. 18 Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.
Bwana Atakuja Ghafla
5 Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, 2 kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. 3 Wakati watu bado wanasema, “Kuna amani na usalama’
4 Bali ninyi, ndugu wapendwa, hamko gizani kuhusu mambo haya hata siku ile iwashtue kama mwizi. 5 Ninyi nyote ni wana wa nuru, wana wa mchana. Sisi sio watu wa giza au wa usiku. 6 Kwa hiyo basi, tusiwe kama baadhi ya watu wengine, waliolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. 7 Maana wale wanaolala hulala usiku, na wale wanaolewa hulewa usiku. 8 Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukivaa imani na upendo kama kinga ya kifuani na kuvaa tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. 9 Maana Mungu hakutuchagua ili tupate ghadhabu yake bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 10 Yeye alitufia ili kama tuko hai au hata kama tumekufa, tuishi pamoja naye. 11 Kwa hiyo farijianeni na kujengana kama mnavyofanya sasa.
Maagizo Ya Mwisho Na Salamu
12 Sasa tunawaomba, ndugu wapendwa, muwaheshimu wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu; ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. 13 Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao. Ishini kwa amani kati yenu. 14 Na tunawasihi, ndugu wapendwa, muwaonye wale walio wavivu, watieni moyo walio waoga, wasaidieni walio dhaifu na muwe na subira na kila mtu. 15 Hakikisheni kuwa mtu hamlipi mwenzake ovu kwa ovu bali daima jitahidini kutendeana wema ninyi kwa ninyi na watu wengine wote.
16 Furahini wakati wote, 17 ombeni pasipo kukoma, 18 shu kuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu. 19 Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 20 msidharau unabii. 21 Pimeni kila kitu. Yash ikeni kwa makini yaliyo mema. 22 Epukeni uovu wa kila namna.
23 Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase kabisa. Roho zenu, nafsi zenu na miili yenu na ihifadhiwe bila kuwa na lawama kwa wakati atakapokuja Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye aliyew aita ni mwaminifu naye atafanya haya.
25 Ndugu wapendwa, tuombeeni. 26 Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. 27 Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii.
1 Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wathes alonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. 2 Tuna watakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.
Sala Na Shukrani
3 Hatuna budi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu wapendwa; na ndivyo inavyostahili kwa sababu imani yenu inaongezeka zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu kwa mwen zake unazidi kuongezeka. 4 Ndio maana sisi tunajivuna kwa ajili yenu miongoni mwa makanisa ya Mungu. Tunajivuna juu ya uvumilivu wenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazopata.
5 Haya yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtastahili kupata Ufalme wa Mungu ambao mnateswa kwa ajili yake. 6 Mungu ni wa haki: atawalipa kwa mateso wale wanaowatesa ninyi 7 na kuwapeni ninyi mnaoteseka nafuu pamoja na sisi pia. Haya yatatokea wakati Bwana Yesu atakapodhi hirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 8 Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. 9 Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake, 10 siku ile atakapokuja kutukuzwa kwa ajili ya watakatifu wake na kustaajabiwa na watu wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa mion goni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
11 Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnastahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu. 12 Tunaomba hivi ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwa ajili yenu nanyi mtukuzwe kwa ajili yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.
Kuja Kwa Bwana Na Kudhihirishwa Kwa Mwovu
2 Basi, kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu mbele zake, tunawasihi, ndugu wapendwa, 2 msifadhaike au kuwa na wasiwasi kutokana na utabiri fulani, au taarifa au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, kusema eti kwamba siku ya Bwana imekwisha kuja. 3 Mtu asiwadanganye kwa namna yo yote maana siku hiyo haitakuja kabla ya uasi kutokea kwanza na yule mwasi adhi hirishwe, yule ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa. 4 Yeye anapinga kila ambacho watu hukiita mungu au cho chote kinachoabu diwa; naye hujiweka hata katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
5 Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambieni mambo haya? 6 Na mnajua kinachomzuia sasa, ili adhihirishwe wakati ufaao. 7 Maana ile nguvu ya siri ya uasi imekwisha anza kufanya kazi; lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo yule mwovu ataonekana, na Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa ufahari wa kuja kwake. 9 Kuja kwa yule mwovu kutafuata kazi ya shetani ambayo itaonyeshwa katika aina zote za ishara bandia na maajabu ya uongo; 10 na katika kila aina ya uovu unaotumiwa kuwadanganya wale wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 11 Ndio maana Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu ili waendelee kuu amini uongo; 12 na ili wote wasioamini kweli bali hufurahia uovu, wahukumiwe.
Simameni Imara
13 Lakini tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, maana Mungu aliwachagueni tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho na kwa kuiamini kweli. 14 Mungu amewaitieni jambo hili kwa njia ya mahubiri yetu ya Habari Njema, ili muweze kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 15 Kwa hiyo ndugu wapendwa, simameni imara na mshike sana yale mafundisho tuliyowapeni katika mahubiri yetu na kwa barua zetu.
16 Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, ali yetupenda akatupatia faraja ya milele na tumaini jema kwa neema, 17 na awafariji mioyoni mwenu na kuwaimarisheni katika kila jambo jema mnalosema au kutenda.
Ombi Kuhusu Maombezi
3 Hatimaye, ndugu wapendwa, tuombeeni ili neno la Mungu lienee upesi na kukubaliwa kama ilivyokuwa kwenu. 2 Ombeni pia kwamba tuokolewe kutokana na watu waovu na wasio na haki, kwa maana si watu wote wanaamini. 3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu. 4 Nasi tuna tumaini kubwa kwa Bwana juu yenu, kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. 5 Bwana aielekeze mioyo yenu kwenye upendo wa Mungu na katika ustahimilivu wa Kristo.
Onyo Kuhusu Uvivu
6 Ndugu wapendwa, katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapeni. 7 Maana ninyi wenyewe mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa nanyi 8 wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya kazi kwa juhudi usiku na mchana ili tusimlemee mtu ye yote kati yenu. 9 Hatukufanya hivi kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada wenu, bali tulitaka tuwape mfano wa kuiga. 10 Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa mtu hatafanya kazi, basi asile.”
11 Tumesikia kwamba baadhi yenu ni wavivu, hawana shughuli maalumu isipokuwa kusengenya wenzao. 12 Sasa tunawaagiza na kuwaonya watu hao katika jina la Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi ili wajipatie chakula wanachokula. 13 Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema.
14 Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. 15 Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu.
Salamu Za Mwisho
16 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote.
17 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote.
1 Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu aliye tumaini letu. 2 Kwa
Walimu Wa Uongo
3 Kama nilivyokusihi wakati nikienda Makedonia, napenda ukae hapo Efeso uwaamuru watu fulani wasiendelee kufundisha mafund isho ya uongo. 4 Pia wasiendelee kupoteza wakati wao kwa hadithi na orodha ndefu zisizo na mwisho za majina ya vizazi ambazo huchochea mabishano badala ya kuwajenga katika maarifa ya kimungu yatokanayo na imani. 5 Shabaha ya maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli. 6 Watu wengine wamepotoka na kuingia katika majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa hawakuzingatia mambo haya. 7 Wanataka kuwa walimu wa sheria ingawa hawaelewi mambo wanayosema wala hayo wanayotilia mkazo.
8 Tunajua kwamba sheria ni njema iwapo inatumika ipasavyo. 9 Lakini tuelewe kwamba sheria haikuwekwa kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya waasi na wasiotii: wasiomcha Mungu na wenye dhambi; wale wasio watakatifu, walio wachafu; wale wanaow aua baba zao na mama zao; wale wanaoua binadamu; 10 wale wal iowazinzi, wafiraji; wale wanaoteka watu nyara, na waongo, na wanaoapa kwa uwongo; na mengine mengi ambayo ni kinyume cha mafundisho ya kweli, 11 ambayo yanaambatana na Injili tukufu ya Mungu Mbarikiwa, ambayo nimekabidhiwa. 12 Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu na kunihesabu kuwa ni mwaminifu kwa kunichagua nimtumikie. 13 Ingawa hapo mwanzo nilimkufuru na kumtesa na kumtukana, nili hurumiwa kwa sababu nilitenda hayo katika ujinga wangu na kutoku amini kwangu. 14 Na neema ya Bwana wetu ilimiminika tele kwa ajili yangu pamoja na imani na upendo uliomo ndani ya Kristo Yesu. 15 Neno hili ni la hakika tena linastahili kukubalika kabisa, kwamba Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi, ambao kati yao, mimi ni mwenye dhambi kuliko wote. 16 Lakini nilihurumiwa kwa sababu hii kwamba, kwa kunitumia mimi niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo aonyeshe uvumilivu wake, niwe mfano kwa wote watakaomwamini na kupata uzima wa milele. 17 Basi, heshima na utukufu ni wake yeye Mfalme wa milele, asi yekufa wala asiyeonekana, aliye peke yake Mungu, milele na milele. Amina.
18 Mwanangu Timotheo, ninakukabidhi agizo hili, kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa juu yako, ili kwa kuyafuata uweze kupigana ile vita njema, 19 ukishikilia imani na dhamiri njema. Watu wengine, kwa kukataa kuisikiliza dhamiri yao, wameangamiza imani yao. 20 Miongoni mwa watu hao wamo Himenayo na Aleksanda ambao nimewakabidhi kwa shetani, ili wajifunze wasimtukane Mungu.
Maagizo Kuhusu Ibada
2 Basi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote: 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani, tukimcha Mungu na kuwa wenye heshima kwa kila njia. 3 Jambo hili ni jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu 4 ambaye anapenda watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli. 5 Maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, 6 aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wote. Yeye ni uthibitisho wa mambo haya, uliotolewa kwa wakati wake. 7 Na hii ndio sababu nilichaguliwa niwe mhubiri na mtume, nasema kweli sisemi uwongo; nilichaguliwa niwe mwalimu wa watu wa mataifa katika imani na kweli.
8 Kwa hiyo, nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono iliyotakaswa pasipo hasira wala mabishano. 9 Kadhalika, nataka wanawake wajipambe kwa heshima na kwa busara. Mavazi yao yawe nadhifu, si kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu na mavazi ya gharama kubwa, 10 bali kwa matendo mema kama iwapa savyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu. 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu na unyenyekevu.
12 Simruhusu mwanamke ye yote kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya wanaume. Mwanamke anapaswa kukaa kimya. 13 Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza kisha Hawa; 14 na Adamu hakudanganywa bali mwanamke alidanganywa akawa mkosaji. 15 Lakini mwanamke ataoko lewa kwa kuzaa, kama ataendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kujiheshimu.
Viongozi Katika Kanisa
3 Neno hili ni kweli, kwamba mtu akitaka kuwa askofu, anata mani kazi njema. 2 Basi, askofu awe mtu asiye na lawama. Awe mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtaratibu, mkarimu na aju aye kufundisha. 3 Asiwe mlevi, wala mgomvi bali awe mpole; asiwe mbishi wala mtu apendaye fedha. 4 Aweze kuisimamia nyumba yake vizuri akiwafanya watoto wake kuwa wanyenyekevu na wenye heshima katika hali zote. 5 Kwa maana kama mtu hawezi kuitawala nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu? 6 Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajiona na kuhukumiwa kama shetani alivyohukumiwa. 7 Kadhalika, awe mwenye sifa njema kati ya watu wa nje ya kanisa, asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa shetani.
Wasaidizi Katika Kanisa
8 Vivyo hivyo mashemasi wawe wenye kuheshimika, si wenye kauli mbili au wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha. 9 Wanapaswa kuizingatia ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 10 Ni lazima wapimwe kwanza na wakionekana kuwa wanafaa basi waruhusiwe kutoa huduma ya ushemasi. 11 Hali kadhalika, wake zao wawe wenye kuheshimika, si wasengenyaji bali wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote. 12 Shemasi awe mume wa mke mmoja; na aweze kuwatawala watoto wake na jamaa yake vema. 13 Watu wanaotoa huduma njema ya ushemasi hujipatia heshima kubwa na uha kika mkubwa katika imani yao kwa Kristo Yesu.
14 Ninakuandikia mambo haya sasa ingawa natarajia kuwepo pamoja nawe karibuni, 15 ili kama nikicheleweshwa, upate kujua jinsi watu wanavyopaswa kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 16 Bila shaka yo yote, siri ya dini yetu ni kuu: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, alithibitishwa katika Roho, alionwa na mal aika, alihubiriwa kati ya mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, aka chukuliwa juu katika utukufu.
Maagizo Kwa Timotheo
4 Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani. 2 Mafundisho hayo yanaletwa na wanafiki waongo ambao dhamiri zao zimekufa kama vile zimechomwa kwa chuma cha moto. 3 Wao wanawazuia watu kuoa; na wanawaamrisha watu wasile vyakula vya aina fulani - ambavyo Mungu aliviumba vipoke lewe kwa shukrani na wale wanaoamini na waliopata kuijua kweli. 4 Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema wala kitu cho chote kisikataliwe kama kinapokelewa kwa shukrani, 5 maana kina takaswa kwa neno la Mungu na kwa sala.
Mtumishi Mwema Wa Kristo
6 Ukiwapa ndugu mafundisho haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu ambaye amelishwa vema kwa maneno ya imani na yale mafundisho mema uliyoyafuata. 7 Usijishughulishe kabisa na hadithi zisizo za kidini ambazo hazina maana. Jizoeze kuishi kwa kumcha Mungu. 8 Maana japokuwa mazoezi ya mwili yana faida kiasi, kumcha Mungu kuna faida kwa kila hali, kwa sababu kumcha Mungu kuna faida kwa maisha ya sasa na maisha yajayo.
9 Neno hili ni la kweli na linastahili kupokelewa, 10 na kwa ajili yake sisi tunajitahidi na kutaabika, kwamba tumeweka tumaini letu kwa Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, hasa wale waaminio.
11 Agiza na kufundisha mambo haya. 12 Mtu asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe mfano mwema kwa waamini wote kwa maneno yako, kwa mwenendo wako, katika upendo, imani na usafi.
13 Mpaka hapo nitakapokuja, tumia wakati wako katika kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri, na kufundisha. 14 Usiache kutumia kipawa ulichonacho, ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee wa kanisa walipokuwekea mikono. 15 Tekeleza mambo haya. Tumia nguvu zako na wakati wako kuyatimiza ili watu wote waone maendeleo yako.
16 Jilinde sana, na utunze mafundisho yako. Yashikilie, maana kwa kufanya hivyo utajiokoa wewe mwenyewe na wale wanaoku sikiliza.
Maagizo Kuhusu Wajane, Wazee Na Watumwa
5 Usimkemee mzee bali umwonye kama baba yako. Vijana uwaten dee kama ndugu zako. 2 Uwaheshimu mama wazee kama mama zako na akina mama vijana kama dada zako , kwa usafi wote.
3 Waheshimu Wajane walioachwa pekee, ipasavyo. 4 Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hao watimize wajibu wao wa kidini kwa familia, kwa kuwahudumia wazazi na hivyo wawarudishie wema wal iowatendea. Kwa kufanya hivyo watampendeza Mungu. 5 Mwanamke ambaye kweli ni mjane na ameachwa peke yake, anamwekea Mungu tumaini lake naye huendelea kusali na kuomba usiku na mchana. 6 Lakini mwanamke aishie kwa anasa, amekufa, ingawa anaishi. 7 Wape maagizo haya, ili wasiwe na lawama. 8 Kama mtu hatunzi jamaa yake, hasa wale waliomo nyumbani mwake, ameikana imani yake, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
9 Mjane ye yote ambaye hajafikia umri wa miaka sitini na ambaye alikuwa mwaminifu kwa mumewe, asiwekwe kwenye orodha ya wajane. Mjane anayestahili kuwekwa kwenye orodha hiyo lazima pia 10 awe mwenye sifa ya matendo mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliyekuwa mkarimu, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, ali yewasaidia watu wenye taabu na aliyejitolea kufanya mema kwa kila njia. 11 Lakini wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena. 12 Na kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kuivunja ahadi yao ya mwanzo. 13 Isitoshe, wajane kama hao wana tabia ya uvivu wakizurura nyumba kwa nyumba. Tena hawawi wavivu tu, bali pia huwa wasengenyaji, wajiingizao katika mambo yasiyowahusu na kusema mambo wasiyopaswa kusema.
4 Kwa hiyo napenda wajane vijana waolewe, wazae watoto na watunze nyumba zao, ili yule adui asipate nafasi ya kusema uovu juu yetu. 15 Kwa maana wajane wengine wamekwisha kupotoka na kumfuata she tani.
16 Lakini kama mama mwamini anao ndugu ambao ni wajane, basi awatunze mwenyewe, kanisa lisibebe mzigo huo, ili liweze kuwat unza wale wajane ambao hawana msaada.
Wazee
17 Wazee wa kanisa wanaoongoza shughuli za kanisa vema wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhu biri na kufundisha. 18 Maana Maandiko husema, “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa,” na tena, “Mfanyakazi anastahili msha hara wake.” 19 Usikubali kusikiliza mashtaka juu ya mzee wa kanisa kama hayakuletwa na mashahidi wawili au watatu. 20 Wale wanaoendelea kutenda dhambi uwaonye hadharani kusudi wengine wapate kuogopa.
21 Ninakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika wateule, tekeleza maagizo haya pasipo kubagua wala upendeleo. 22 Usiwe na haraka kumwekea mtu mikono wala usishiriki katika dhambi za mtu mwingine, jiweke katika hali ya usafi.
23 Usiendelee kunywa maji tu bali tumia divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako na maumivu yako ya mara kwa mara.
24 Dhambi za watu wengine ni dhahiri nazo zinatangulia huku muni mbele yao. Lakini dhambi za watu wengine huonekana baadaye. 25 Hali kadhalika matendo mema ni dhahiri na hata kama si dha hiri hayawezi kuendelea kufichika.
Watumwa
6 Watumwa wote wawahesabu mabwana zao kuwa wanastahili hesh ima zote, ili watu wasije wakalitukana jina la Mungu pamoja na mafundisho yetu. 2 Watumwa ambao mabwana zao ni waamini, wasikose kuwaheshimu kwa kuwa ni ndugu; bali watumike kwa ubora zaidi kwa sababu wale wanaonufaika kwa huduma yao ni waamini na ni wapendwa.
3 Fundisha na kuhimiza mambo haya. Mtu ye yote akifundisha kinyume cha haya na asikubaliane na maneno ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo, na mafundisho yanayo ambatana na kumcha Mungu, 4 huyo amejaa majivuno na wala hafahamu cho chote. Mtu kama huyo ana uchu wa ubishi na mashindano ya maneno ambayo huleta wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya, 5 na ugomvi wa mara kwa mara kati ya watu wenye mawazo maovu, ambao hawanayo ile kweli, na ambao hudhani kwamba kumcha Mungu ni njia ya kuchuma fedha.
6 Bali kumcha Mungu na kuridhika ni faida kubwa. 7 Kwa maana hatukuja na kitu cho chote hapa duniani, wala hatuwezi kutoka na kitu. 8 Lakini kama tuna chakula na mavazi, basi tutaridhika. 9 Watu wanaotamani kuwa matajiri huanguka katika majaribu na mtego na katika tamaa nyingi mbaya na za kijinga, ambazo huwato komeza wanadamu katika upotevu na maangamizi. 10 Maana kupenda fedha ni chanzo cha uovu wote. Tamaa ya fedha imewafanya wengine watangetange mbali na imani na kuteseka kwa huzuni nyingi.
Mawaidha Ya Paulo Kwa Timotheo
11 Lakini wewe mtu wa Mungu, epuka haya yote. Tafuta kupata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole. 12 Pigana ile vita njema ya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa ulipokiri lile ungamo lako jema mbele ya mashahidi wengi.
13 Mbele ya Mungu ambaye amevipa vitu vyote uhai, na mbele ya Kristo Yesu ambaye kwa ushuhuda wake mbele ya Pontio Pilato alikiri lile ungamo jema, 14 ninakuamuru utunze amri hii bila doa wala lawama mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakapokuja. 15 Jambo hili Mungu atalitimiza kwa wakati wake mwenyewe, Mungu Mbarikiwa ambaye peke yake ndiye Atawalaye, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. 16 Yeye peke yake ndiye asiyekufa, na ndiye aishiye katika nuru isiyoweza kukaribiwa; hakuna mwanadamu ali yepata kumwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
17 Uwaagize matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke matumaini yao katika mali ambayo haina hakika. Bali wam tumaini Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifu rahie. 18 Waambie watende wema, wawe matajiri katika matendo mema, wawe wakarimu na tayari kushiriki mali zao na wengine. 19 Kwa njia hii watajiwekea msingi imara kwa wakati ujao na hivyo watajipatia uzima ambao ni uzima kweli.
20 Timotheo, tunza vema yote uliyokabidhiwa. Epuka majadil iano yasiyo ya Mungu na mabishano ambayo kwa makosa huitwa elimu.
1 Kutoka kwa Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Ninakutakia neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
Paulo Amtia Moyo Timotheo
3 Ninamshukuru Mungu ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyomtumikia baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika sala zangu. 4 Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nijazwe furaha. 5 Nakumbushwa kuhusu imani yako ya kweli, imani ambayo walikuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo nina hakika, unayo. 6 Kwa sababu hii nakukum busha ukichochee kile kipawa ulichopewa na Mungu wakati nilipo kuwekea mikono. 7 Maana Mungu hakutupatia roho ya woga bali roho ya nguvu, ujasiri na kiasi.
8 Basi usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake, bali uishiriki taabu kwa ajili ya Habari Njema kwa kadiri ya nguvu upewayo na Mungu. 9 Yeye ametuokoa na kutuita tupokee maisha ya utakatifu; si kwa sababu ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya makusudio yake na neema yake. Tulipewa neema hii katika Kristo Yesu tangu milele 10 na sasa imedhihirishwa kwa kuja kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu ambaye ameondoa kifo kabisa na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 11 Nami nimechaguliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 12 Ndio sababu ninateseka hivi. Lakini sioni aibu kwa maana ninamjua huyo niliyemwamini na nina hakika ya kuwa anaweza kutunza kile nilichomkabidhi, mpaka siku ile.
13 Tumia kama kielelezo cha mafundisho sahihi maneno ya kweli ambayo umeyasikia kutoka kwangu pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. 14 Linda ile kweli ambayo umekabidhiwa na Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu. 15 Bila shaka unafahamu kuwa watu wote katika jimbo la Asia wameniacha, wakiwemo Filego na Hermogene. 16 Bwana aonyeshe huruma yake kwa jamaa ya Onesiforo kwa sababu alinitia moyo mara nyingi na hakuonea aibu minyororo yangu. 17 Bali alipofika Roma alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 18 Bwana amwezeshe kupata rehema kutoka kwa Bwana siku ile. Unafahamu pia jinsi alivyoni saidia huko Efeso.
Askari Mwaminifu Wa Kristo Yesu
2 Basi, wewe mwanangu, uwe imara katika neema iliyomo ndani ya Kristo Yesu. 2 Na mambo ambayo ulinisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu ambao wataweza kuwa fundisha watu wengine pia. 3 Vumilia mateso pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4 Hakuna askari ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kiraia kwa sababu nia yake ni kumrid hisha yule aliyemwandika kuwa askari. 5 Hali kadhalika mwanar iadha hawezi kupewa tuzo kama hakufuata masharti. 6 Mkulima mwe nye bidii ndiye anayestahili kupata fungu la kwanza la mavuno. 7 Yatafakari haya ninayokuambia, kwa maana Mungu atakupa ufahamu katika mambo yote.
8 Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyez aliwa katika ukoo wa Daudi. Hii ndio Injili yangu ninayoihubiri. 9 Nami ninateseka kwa sababu ya Injili hii nikivaa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halikufungwa minyororo. 10 Kwa hiyo ninavumilia taabu zote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi na wao pia wapokee wokovu uliomo ndani ya Kristo Yesu pamoja na utukufu wake wa milele.
11 Neno hili ni kweli kabisa: kwamba kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia. 12 Kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia; kama tukimkana, naye pia atatukana. 13 Tusipo kuwa waaminifu, yeye huendelea kuwa mwaminifu kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Mfanyakazi Mwenye Kibali Mbele Za Mungu
14 Wakumbushe mambo haya na uwaamuru mbele za Bwana waache kubishana juu ya maneno. Hii haiwasaidii cho chote bali huwaanga miza wanaowasikiliza. 15 Jitahidi kujidhihirisha mbele za Mungu kama mtu aliyepata kibali chake, mfanyakazi asiyekuwa na sababu yo yote ya kuona aibu, ambaye hulitumia neno la kweli kwa usa hihi. 16 Jiepushe na maneno ya kipuuzi, yasiyo ya kimungu, kwa maana hayo huwavuta watu mbali na Mungu zaidi na zaidi. 17 Mafundisho yao yataendelea kuenea kama donda ndugu. Kati yao wamo Himenayo na Fileto 18 ambao wametanga tanga na kuiacha kweli wakisema kwamba ufufuo umekwishapita. Wanapotosha imani ya baadhi ya watu. 19 Lakini msingi thabiti wa Mungu umesimama imara ukiwa na muhuri wenye maneno haya: “Bwana anawajua walio wake,” na tena, “Kila anayelitaja jina la Bwana aache uovu.”
20 Katika nyumba ya kifahari kuna vyombo vya dhahabu na fedha na pia vimo vyombo vya mbao na vya udongo. Baadhi ya vyombo ni vya heshima lakini vingine sio. 21 Kama mtu akijitakasa na kujitenga na visivyo vya heshima atakuwa chombo cha kutumika kwa shughuli za kifahari; chombo kilichotakaswa kimfaacho Bwana wa nyumba, ambacho ni tayari kwa matumizi yote yaliyo mema. 22 Basi, kimbia tamaa za ujana, na utafute kupata haki, imani, upendo na amani pamoja na wote wamwitao Bwana kwa moyo safi.
23 Usijishughulishe na mabishano yasiyo na maana na ya kipumbavu kwa kuwa unajua ya kwamba hayo huleta ugomvi. 24 Na tena mtumishi wa Bwana hapaswi kuwa mgomvi. Anapaswa kuwa mpole kwa kila mtu na mwalimu mwenye uwezo, na mvumilivu. 25 Anapaswa kuwaonya wale wanaompinga kwa upole, kwa matumaini kwamba Mungu anaweza kuwajalia watubu na kuifahamu kweli; 26 fahamu zao ziwarudie tena, watoke katika mtego wa shetani ambaye amewafunga wafanye kama apendavyo.
Hatari Za Siku Za Mwisho
3 Lakini fahamu jambo hili: kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio na utakatifu; 3 wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; 4 wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno, wapendao anasa badala ya kumpenda Mungu. 5 Hao ni watu ambao kwa nje wataonekana kuwa wana dini, huku wakikana nguvu ya imani yao. Jiepushe na watu wa jinsi hiyo.
6 Maana miongoni mwao wamo wale waendao katika nyumba za watu na kuwateka wanawake dhaifu waliolemewa na dhambi na kuyumbishwa na tamaa za kila namna. 7 Wao humsikiliza kila mtu lakini hawawezi kutambua kweli. 8 Kama vile Yane na Yambre walivyopin gana na Musa, kadhalika watu hawa nao wanapingana na ile kweli. Ni watu wenye akili potofu, wenye imani ya bandia. 9 Lakini hawa tafika mbali, kwa sababu ujinga wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri ujinga wa hao watu wawili.
Maagizo Ya Paulo Kwa Timotheo
10 Bali wewe umeyafahamu mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudio yangu, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu, ustahimilivu wangu, 11 mateso yangu, taabu zangu. Umefahamu yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonia na Listra, mateso yote niliyostahimili; lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya kumcha Mungu ndani ya Kristo Yesu watateswa. 13 Lakini watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14 Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitam bua umejifunza hayo kutoka kwa nani; 15 na jinsi ambavyo tangu utoto wako umeyafahamu Maandiko matakatifu ambayo yanaweza kukuelekeza kupokea wokovu kwa kumwamini Kristo Yesu. 16 Andiko zima lina pumzi ya Mungu nalo lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki 17 ili mtu wa Mungu awe kamili akiwa na nyenzo zote za kutenda kila jambo jema.
Maagizo Ya Mwisho
4 Ninakuamuru mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu ambaye atawahukumu walio hai na wafu; na kwa kuja kwake na ufalme wake: 2 hubiri Neno; lisisitize wakati ufaao na wakati usiofaa; sadik isha, kemea, na kuonya kwa uvumilivu mkuu na mafundisho thabiti. 3 Maana wakati unakuja ambapo watu hawatavumilia kusikia mafund isho yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajilundi kia walimu tele watakaowaambia yale ambayo masikio yao yanatamani sana kuyasikia. 4 Watakataa kabisa kusikia kweli na watageukia hadithi za uongo. 5 Bali wewe uwe imara, katika mambo yote, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.
6 Maana mimi sasa ni tayari kutolewa kama sadaka, saa ya kuondoka kwangu imefika. 7 Nimepigana ile vita njema, nimemaliza shindano, nimeitunza imani. 8 Na sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanituza Siku ile; wala si mimi tu, bali na wote ambao wamengojea kwa hamu kuja kwake.
Maombi Ya Binafsi
9 Jitahidi kuja kuniona upesi 10 kwa sababu Dema, kwa kuu penda ulimwengu huu wa sasa, ameniacha akaenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia.
11 Ni Luka peke yake ambaye yupo hapa pamoja nami. Mchukue Marko uje pamoja naye kwa sababu ananisaidia katika huduma yangu. 12 Nimemtuma Tikiko Efeso. 13 Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu, hasa vile vya ngozi.
14 Aleksanda mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Mungu atamlipa kwa yale aliyonitendea. 15 Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu alipinga vikali ujumbe wetu.
16 Nilipojitetea mara ya kwanza hakuna hata mmoja aliyekuwa upande wangu, kila mmoja alinikimbia. Naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama nami akanitia nguvu kutangaza Habari Njema kwa ukamilifu ili watu wote wa mataifa wapate kusikia. Na niliokolewa kutoka katika kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa katika kila uovu na kunihifadhi mpaka niu fikie ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe Yeye milele na milele.
Salamu Za Mwisho
19 Nisalimie Prisila na Akila na wote waliomo nyumbani kwa Onesiforo. 20 Erasto alibaki Korintho. Trofimo nilimwacha akiwa mgonjwa huko Mileto.
21 Jitahidi kufika huku kabla ya majira ya baridi kali. Sal amu zako kutoka kwa Eubulo, Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.
1 Kutoka kwa Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo. Mimi nimetumwa kwa wale ambao Mungu amewateua ili niwaon goze katika imani na katika maarifa ya kweli yanayopatana na kum cha Mungu; 2 na katika tumaini la uzima wa milele ambalo Mungu, ambaye hasemi uongo, aliahidi hata kabla dunia haijakuwepo. 3 Naye kwa wakati aliopanga alidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo nilikabidhiwa kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.
4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki pamoja. Ninakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu
Kazi Ya Tito Kule Krete
5 Nilikuacha huko Krete kusudi urekebishe mambo yote yal iokuwa hayakunyooka na uchague wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa asiwe na lawama yo yote; awe mume wa mke mmoja; awe ni mtu ambaye watoto wake ni waamini na wala sio jeuri au wasiotii. 7 Kwa kuwa askofu amekabidhiwa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na lawama. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mgomvi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyokuwa ya halali. 8 Bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye kujitawala, mnyofu, mtakatifu na mwe nye kudhibiti na si yake. 9 Ni lazima alishike kwa uthabiti neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine na kudhihirisha makosa ya wale wanaolipinga.
Walimu Wa Uongo
10 Maana wapo wakaidi wengi, waliojaa maneno matupu na waongo, hasa kile kikundi cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamaz ishwe kwa sababu wanapotosha jamaa nzima kwa kufundisha mambo wasiyostahili kufundisha. Wanafanya hivyo kusudi wajipatie fedha. 12 Hata mmojawapo wa manabii wao amesema: “Wakrete ni waongo siku zote, ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu.” 13 Maneno hayo ni kweli kabisa. Kwa hiyo uwakemee kwa ukali ili wapate kuwa imara katika imani. 14 Wasiendelee kushikilia hadithi za Kiy ahudi au maagizo ya watu wanaokataa ukweli. 15 Kwa watu walio safi, kila kitu ni safi. Lakini kwa watu waovu na wasioamini, hakuna kilicho safi. Mawazo yao na dhamiri zao zimejaa uovu.
16 Wanajidai kuwa wanamjua Mungu lakini wanamkana kwa matendo yao. Ni watu wa kuchukiza, waasi, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.
Mafundisho Sahihi
2 Lakini wewe, mafundisho yako ni lazima yawe sahihi. 2 Wafundishe wazee kuwa na kiasi, watulivu, wenye busara na tha biti katika imani, upendo na subira. 3 Hali kadhalika akina mama wazee wawe na mwenendo wa unyenyekevu. Wasiwe wachonganishi, wala wasiwe watumwa wa pombe; bali waonyeshe mfano mwema. 4 Hivyo wawafundishe akina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto wao 5 na kuwa wenye kiasi na safi, wakitumia wakati wao kushughulika nyumbani mwao. Wawe wema na watii kwa waume zao, ili neno la Mungu lisije likadharauliwa kwa ajili yao. 6 Vile vile uwahimize vijana kuwa na kiasi. 7 Katika mambo yote wewe mwenyewe uwe kielelezo cha matendo mema. Uonyeshe usa hihi na uthabiti katika mafundisho yako. 8 Maneno yako yawe na kina na mantiki safi, mtu asiweze kuyatoa kasoro na hata yule anayepinga aaibike kwa kukosa lo lote baya la kusema juu yetu.
9 Wahimize watumwa kuwatii mabwana wao na kuwapendeza katika mambo yote; wasijibishane nao 10 wala kuwaibia, bali watumwa waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa ili katika kila hali mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yapate sifa njema.
11 Kwa maana neema ya Mungu iletayo wokovu imedhihirishwa kwa watu wote. 12 Neema hiyo inatufundisha kukataa uovu na tamaa za dhambi, tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu. Wakati huo huo 13 tukingojea tumaini letu lenye baraka - kuja kwa utukufu wa Mungu wetu Mkuu na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. 14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe katika uasi wote, na kutufanya tuwe safi kwa ajili yake; na tuwe watu wake kabisa, ambao wana juhudi katika kutenda mema.
15 Fundisha mambo haya; himiza na kemea kwa mamlaka yote. Mtu ye yote asikudharau.
Kutenda Mema
3 Wakumbushe watu kujinyenyekeza kwa watawala na watu wenye mamlaka; wawe watii na wepesi kufanya kazi yo yote halali. 2 Wakumbushe wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wapole na waonyeshe unyenyekevu kwa kila mtu.
3 Maana kuna wakati ambapo sisi wenyewe tulikuwa wajinga, wakaidi; tukidanganywa na daima kutawaliwa na tamaa mbaya na anasa za kila aina. Tulikuwa tukiishi maisha ya uovu na wivu, tukichukiwa na watu na kuchukiana sisi kwa sisi. 4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa, 5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. 7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele tunaoutumainia . 8 Neno hili ni kweli kabisa. Ninataka uyatilie mkazo mambo haya ili wale waliomwamini Mungu waone umuhimu wa kutenda mema wakati wote, maana mambo haya ni mazuri na tena ni ya manufaa kwa watu.
9 Lakini jiepushe na ubishi wa kipuuzi: mambo kama orodha ndefu za vizazi na ubishi na ugomvi juu ya sheria; haya hayana maana wala hayamsaidii mtu ye yote. 10 Mtu anayesababisha mafarakano, muonye mara ya kwanza na mara ya pili. Baada ya hapo, usijishughulishe naye tena. 11 Una jua kwamba mtu kama huyo amepotoka na tena ni mwenye dhambi ambaye amejihukumu mwenyewe.
Maagizo Ya Mwisho
12 Nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja Nika poli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya bar idi. 13 Wahimize Zena, yule mwanasheria, na Apolo waje upesi na uhakikishe kwamba hawapungukiwi na kitu cho chote. 14 Watu wetu hawana budi kujifunza kuona umuhimu wa kutenda mema, ili waweze kusaidia watu wenye mahitaji ya lazima na maisha yao yasikose kuwa na matunda.
1 Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, pamoja na ndugu yetu Timotheo. Tunakuandikia wewe Filemoni mfanyakazi mwenzetu mpendwa, na dada yetu Afia na askari mwenzetu Arkipo, 2 pamoja na kanisa linalokutana nyumbani kwako 3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu
Upendo Na Imani Ya Filemoni
4 Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapokuombea 5 kwa sababu ninasikia habari za upendo wako na imani uliyonayo kwa Bwana wetu Yesu na kwa watakatifu wote. 6 Ninakuombea kwamba unaposhirikiana na wengine juu ya imani yako upate kuelewa kikamilifu kila jambo jema ambalo tunapata ndani ya Kristo. 7 Ndugu yangu, upendo wako umenipa furaha kubwa na faraja, kwa maana wewe umechangamsha mioyo ya watakatifu.
Ombi Kuhusu Onesmo
8 Kwa sababu hii, ingawa nina ujasiri ndani ya Kristo kuku amuru ufanye linalotakiwa, 9 lakini kwa ajili ya upendo, ninaona ni bora zaidi nikuletee ombi. Mimi Paulo, balozi ambaye sasa ni mfungwa kwa ajili ya Yesu Kristo, 10 ninalo ombi kwako kuhusu mwanangu Onesmo; ambaye nimekuwa baba yake wa kiroho nikiwa gere zani. 11 Hapo awali huyu Onesmo alikuwa hakufai, lakini sasa amekuwa wa manufaa kwako na kwangu pia.
12 Ninamrudisha kwako, yeye ambaye ni kama moyo wangu mwe nyewe. 13 Ningelipenda akae nami hapa anisaidie badala yako wakati huu ambapo niko gerezani kwa ajili ya Injili. 14 Lakini sikupenda kufanya lo lote pasipo wewe kuniruhusu maana sipendi unisaidie kwa kulazimishwa, bali kwa hiari yako mwenyewe.
15 Pengine Onesmo aliondoka kwako kwa muda mfupi kusudi uta kapompata tena uweze kuwa naye daima; 16 na asiwe tena kama mtumwa tu, bali kama ndugu mpendwa. Yeye ni wa thamani sana kwangu lakini hasa zaidi kwako, maana pamoja na kuwa mtumwa wako, sasa ni ndugu yako katika Bwana.
17 Kwa hiyo ikiwa unanihesabu kama mshiriki mwenzako, basi mpokee kama vile ambavyo ungenipokea mimi. 18 Kama amekukosea jambo lo lote au ana deni lako, basi unidai mimi. 19 Mimi Paulo ninaandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe, nitalipa. Wala sidhani nina haja ya kukukumbusha kwamba wewe mwenyewe ni mdeni wangu kwa ajili ya nafsi yako. 20 Kwa hiyo ndugu yangu, ninaamini utafanya jambo hili kwa ajili ya Bwana. Burudisha moyo wangu katika Kristo.
21 Naandika nikiwa na hakika ya kuwa utatii ninalokuambia na kwamba utafanya hata zaidi ya haya. 22 Tena nakuomba unitayar ishie chumba cha kukaa, kwa maana natarajia kurudi kwenu kama jibu la Mungu kwa maombi yenu.
23 Salamu zenu kutoka kwa Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu; 24 na kutoka kwa Marko, Aristarko, Dema na
Copyright © 1989 by Biblica