Bible in 90 Days
Ukuu Wa Mwana Wa Mungu
1 Hapo zamani Mungu alisema na baba zetu mara nyingi na kwa namna mbali mbali kwa kuwatumia manabii. 2 Lakini katika siku hizi za mwisho, amesema na sisi kwa njia ya Mwanae, ambaye alim chagua kuwa mrithi wa vitu vyote. Na kwa njia ya Mwanae, Mungu aliumba ulimwengu. 3 Yeye Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa halisi ya nafsi yake, naye huudumisha na kuuendeleza ulim wengu kwa neno lake lenye nguvu. Alipokwisha kuwapatia wanadamu utakaso wa dhambi, alikaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi aliye juu. 4 Kwa hiyo Mwana alikuwa mkuu zaidi kuliko malaika, kama ambavyo jina alilorithi kwa Mungu ni kuu kuliko jina la malaika ye yote.
5 Kwa maana ni malaika gani ambaye Mungu aliwahi kumwambia: “Wewe ni mwanangu; leo hii nimekuzaa”? Au tena: “Mimi nita kuwa Baba yake na yeye atakuwa Mwanangu”? 6 Na tena Mungu ana pomleta mwanae, mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anasema: “Malaika wote wa Mungu wamwabudu yeye.” 7 Anapozungumza juu ya malaika anasema: “Anawafanya malaika wake kuwa upepo, watumishi wake kuwa ndimi za moto.” 8 Lakini kuhusu Mwana, anasema: “Kiti chako cha enzi, Wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na haki takuwa fimbo ya ufalme wako. 9 Umependa haki na kuchukia uovu. Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuchagua wewe na kukuweka juu ya wenzako kwa kukupaka mafuta ya furaha.” 10 Pia anasema: “Hapo mwanzo , Wewe Bwana, uliweka misingi ya ulimwengu, na mbingu ni kazi ya mikono yako. 11 Vyote vitaangamia lakini wewe unadumu; vyote vitachakaa kama nguo, nawe 12 utavikunja kama vazi na kuvibadilisha. Bali wewe hubadiliki, na miaka yako haitakwisha kamwe. ” 13 Lakini ni malaika gani amewahi kumwambia, “Keti kulia kwangu mpaka niwafanye adui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako”? 14 Malaika ni nani basi? Wao ni roho wa utumishi waliotumwa kuwahudumia wale watakaopokea wokovu.
Kuzingatia Mafundisho
2 Kwa hiyo, hatuna budi kuzingatia kwa makini mambo tuliyof undishwa tusije tukatanga-tanga mbali na yale tuliyosikia. 2 Kwa maana kama ujumbe ulioletwa na malaika ulithibitika kuwa kweli, na kila aliyeasi na kutokutii akaadhibiwa ilivyostahili, 3 sisi je? Tutaepukaje kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu kwanza ulitangazwa na Bwana, na ulithibitishwa kwetu na wale wal iomsikia. 4 Mungu pia aliushuhudia kwa ishara na miujiza na maaj abu mbalimbali, pamoja na karama za Roho Mtakatifu alizogawa kufuatana na mapenzi yake.
Wokovu Umeletwa Na Kristo
5 Maana Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, tunaouzungumzia, chini ya mamlaka ya malaika. 6 Bali kama inavyothibitishwa katika sehemu fulani ya Maandiko, “Mwanadamu ni kitu gani hata umfi kirie, au mwana wa binadamu ni nani hata umjali? 7 Umemfanya kuwa chini kidogo ya malaika; wewe umemvika taji ya utukufu na heshima, 8 umemfanya kuwa mtawala wa vitu vyote.” Mungu ali poweka vitu vyote chini ya mamlaka ya mwanadamu, hakubakiza cho chote ambacho mwanadamu hakitawali. Lakini kwa wakati huu hatuoni kama kila kitu kiko chini ya mamlaka yake. 9 Lakini tunamwona Yesu, ambaye kwa muda mfupi alifanywa kuwa chini kidogo ya mal aika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa, ili kwa neema ya Mungu, aonje mauti kwa ajili ya watu wote.
10 Kwa maana ilikuwa ni sawa kabisa kwamba Mungu, ambaye kwa ajili yake na kwa uweza wake vitu vyote vimekuwepo, amfanye Mwan zilishi wa wokovu wao kuwa mkamilifu kwa njia ya mateso, ili awalete wana wengi washiriki utukufu wake. 11 Maana yule anayetakasa na wale wanaotakaswa, wote wanatoka katika uzao mmoja. 12 Ndio maana Yesu haoni aibu kuwaita wao ndugu zake, akisema: “Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katikati yao nitakusifu.” 13 Na tena anasema, “Nitamwekea Mungu tumaini langu.” Na tena, “Niko hapa, mimi pamoja na watoto niliopewa na Mungu.”
Mungu.”
14 Basi, kwa kuwa watoto hao wana mwili na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kufa kwake apate kumwan gamiza yule mwenye mamlaka juu ya kifo, yaani shetani; 15 na hivyo awaweke huru wale ambao walikuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa kifo. 16 Maana ni wazi kwamba hakuja kuwa saidia malaika bali kuwasaidia uzao wa Ibrahimu. 17 Kwa sababu hii ilibidi awe kama ndugu zake kwa kila hali, apate kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika huduma ya Mungu, ili aweze kujitoa kama sadaka kwa ajili ya dhambi za watu. 18 Na kwa kuwa yeye mwenyewe ameteswa na kujaribiwa, anaweza kuwasaidia wanaoj aribiwa.
Yesu Ni Mkuu Kuliko Musa
3 Kwa hiyo, ndugu zangu watakatifu, ambao mmeshiriki wito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na kuhani mkuu wa imani tunay oikiri.
2 Kwa maana Yesu alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemchagua, kama vile Musa alivyokuwa mwaminifu katika nyumba ya Mungu. 3 Lakini Yesu amehesabiwa kuwa anastahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile mjenzi wa nyumba anavyopewa heshima zaidi kuliko nyumba aliyoijenga. 4 Maana kila nyumba hujengwa na mtu fulani bali aliyejenga vitu vyote ni Mungu. 5 Ni kweli kwamba Musa ali kuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, akishu hudia juu ya yale mambo ambayo Mungu angeyatamka baadaye, 6 lakini Kristo alikuwa mwaminifu katika nyumba ya Mungu kama mwana. Na sisi ni nyumba yake, ikiwa tutashikilia ujasiri wetu na lile tumaini tunalojivunia.
Jihadharini Na Kutokuamini
7 Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, mkiisikia sauti yake, 8 msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama mlivyofanya wakati wa uasi , siku ile ya majaribio jangwani, 9 ambapo baba zenu walinijaribu wakaona kazi zangu kwa miaka arobaini. 10 Kwa hiyo kizazi kile kilinikasirisha, nikasema, ‘Mioyo ya watu hao imepotoka; hawajapata kujua njia zangu.’ 11 Katika hasira yangu nikaapa, ‘Hawataingia kwenye pumziko langu kamwe.’
12 Angalieni, ndugu zangu, asiwepo miongoni mwenu mtu ye yote mwenye moyo wa dhambi, usioamini, unaomfanya ajitenge na Mungu wa uzima. 13 Bali muonyane kila siku maadamu bado ni ‘ ‘leo” ili asiwepo mtu kati yenu anayefanywa mkaidi na udangany ifu wa dhambi. 14 Kwa maana sisi ni washiriki pamoja na Kristo iwapo tutashikilia tumaini letu la kwanza kwa uaminifu mpaka mwisho. 15 Kama Maandiko yalivyosema: “Leo mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu. Kama mlivyofanya wakati wa uasi.” 16 Ni nani hao waliosikia lakini wakaasi? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17 Na ni nani waliom kasirisha Mungu kwa miaka arobaini? Si wale waliofanya dhambi wakafa jangwani? 18 Na ni nani ambao Mungu aliapa kuwa hawatain gia kwenye pumziko lake, isipokuwa wale waliokataa kutii? 19 Kwa hiyo tunaona kwamba walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. Pumziko La Sabato
4 Basi, maadamu ahadi ya Mungu ya kuingia katika pumziko lake bado ipo, tujihadhari asije mmoja wenu akakutwa ameshindwa kuin gia huko. 2 Maana sisi tumehubiriwa Habari Njema kama vile wao walivyohubiriwa. Lakini ujumbe waliosikia haukuwasaidia kwa sababu hawakuupokea kwa imani. 3 Kwa kuwa sisi tulioamini tunain gia katika pumziko hilo, kama Mungu alivyosema, “Na katika hasira yangu nikaapa, ‘Hawataingia kwenye pumziko langu kamwe.’ Mungu alisema hivyo ingawa kazi yake ilikamilika tangu ulimwengu ulipoumbwa. 4 Maana mahali fulani akizungumza kuhusu siku ya saba, alisema: “Mungu alipumzika siku ya saba baada ya kazi zake zote.” 5 Na tena mahali hapo alisema: “Hawataingia kwenye pum ziko langu kamwe.” 6 Basi kwa kuwa wapo watakaoingia kwenye pum ziko hilo, na wale ambao walihubiriwa Habari Njema hapo mwanzo lakini wakashindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii kwao, 7 kwa hiyo Mungu aliweka tena siku nyingine akaiita “Leo”; akasema kwa maneno ya Daudi miaka mingi baadaye, kama yalivyokwisha kukaririwa: “Leo mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu.”
8 Maana, kama Yoshua angalikuwa amekwisha kuwapatia pumziko, Mungu asingalizungumzia baadaye kuhusu siku nyingine. 9 Kwa hiyo basi ipo bado sabato ya mapumziko waliyowekewa watu wa Mungu; 10 kwa maana, mtu anayeingia katika pumziko la Mungu, pia hupum zika kutoka katika kazi zake kama vile Mungu alivyopumzika baada ya kazi zake.
11 Basi tujitahidi kuingia kwenye pumziko hilo asije mtu akaanguka kwa kutokuamini kama hao. 12 Kwa maana neno la Mungu ni hai tena lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili, linachoma kabisa na kutenganisha nafsi na roho, viungo vya mwili na mafuta yaliyomo ndani yake; na kutambua nia na mawazo ya mioyo ya watu. 13 Hakuna kiumbe cho chote kilichofi chika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye hatuna budi kueleza habari zetu zote kwake.
Kuhani Mkuu Yesu Kristo
14 Hivyo basi, kwa kuwa tunaye kuhani mkuu aliyepitia mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, tushikilie kwa uthabiti imani yetu tunayoikiri. 15 Kwa maana huyu kuhani wetu mkuu si kuhani ambaye hawezi kutuhurumia katika udhaifu wetu, bali ni kuhani ambaye kwa kila hali amejaribiwa kama sisi, lakini pasipo kutenda dhambi. 16 Kwa hiyo basi, tusogelee kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa shida.
Sifa Za Kuhani Mkuu
5 Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa watu huteuliwa kumtumikia Mungu kwa niaba yao, kutoa sadaka na dhabihu kwa ajili ya dhambi zao. 2 Anaweza kuwaonea huruma wale wasioel ewa na wanaopotoka kwa sababu yeye mwenyewe anasumbuliwa na udhaifu kama wao . 3 Kwa sababu hii, anawajibika kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za hao watu.
4 Hakuna mtu anayejichagulia heshima hii ya kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huitwa na Mungu kama vile Haruni alivyoitwa.
5 Kristo hakujichagulia mwenyewe utukufu wa kuwa kuhani mkuu. Bali aliteuliwa na Mungu ambaye alimwambia, “Wewe ni mwanangu, leo hii nimekuzaa;” 6 na tena kama asemavyo mahali pengine, “Wewe ni kuhani milele, katika ngazi ile ya ukuhani ya Mel kizedeki. 7 Yesu alipokuwa akiishi duniani, alitoa dua na maombi kwa kilio kikuu na machozi kwa Mungu ambaye angeweza kumwokoa na kumtoa katika kifo, naye Mungu alimsikia kwa sababu alikuwa mnyenyekevu na mtiifu. 8 Ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, aliji funza utii kutokana na mateso aliyopata; 9 na baada ya kufanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii, 10 akateuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu wa ngazi ile ile ya
Onyo Kuhusu Kuanguka
11 Kuhusu ukuhani huu, tunayo mengi ya kusema ambayo ni mag umu kuyaeleza, kwa maana ninyi si wepesi wa kuelewa. 12 Ingawa kwa wakati huu mngalipaswa kuwa walimu, lakini bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za kwanza za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu. 13 Kwa maana anayeishi kwa maziwa peke yake bado ni mtoto mchanga, hana ujuzi katika mafund isho kuhusu neno la haki. 14 Bali chakula kigumu ni kwa ajili ya watu wazima, watu ambao wamekomaa akili kutokana na mafunzo ya mazoezi ya kupambanua kati ya mema na mabaya.
6 Basi sasa tutoke katika yale mafundisho ya msingi kuhusu Kristo, tupige hatua kufikia ukamilifu katika kuelewa kwetu. Hatupaswi tena kuwaeleza ninyi yale mafundisho ya msingi kuhusu kutubu na kuacha matendo yaletayo kifo, na kuhusu kumwamini Mungu 2 pamoja na maagizo kuhusu ubatizo, kuwekea watu mikono, kufufuka kwa wafu na hukumu ya milele. 3 Mungu akitujalia tutaendelea mbele.
4 Kwa maana haiwezekani tena kuwarejesha katika toba watu ambao waliwahi kuongoka, ambao wameonja uzuri wa mbinguni, wakashiriki 5 Roho Mtakatifu, ambao wameonja wema wa neno la Mungu na nguvu za nyakati zijazo, 6 kama wakikufuru. Kwa sababu wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu mioyoni mwao na kumwaibisha hadharani. 7 Ardhi ambayo baada ya kupata mvua ya mara kwa mara, hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao wanailima na kupokea bar aka kutoka kwa Mungu. 8 Lakini kama ardhi hiyo itaotesha magugu na miiba, haina thamani, na inakaribia kulaaniwa. Mwisho wake ni kuchomwa moto.
Wanaopokea Ahadi Za Mungu
9 Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mazuri zaidi, yanayoandamana na wokovu. 10 Mungu si dhalimu hata asahau kazi yenu na upendo mliomwonyesha mlipowa saidia watu wake na mnavyoendelea kuwasaidia. 11 Tunapenda kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyo hiyo mpaka mwisho ili mpate kupo kea tumaini lenu. 12 Hatutaki muwe wavivu bali muige wale ambao kwa imani na subira hupokea yale yaliyoahidiwa na Mungu.
Uhakika Wa Ahadi Ya Mungu
13 Mungu alipompa Ibrahimu ahadi, aliapa kwa jina lake mwe nyewe kwa kuwa hapakuwa na mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake. 14 Alisema, “Hakika nitakubariki na kukupatia watoto wengi.” 15 Na hivyo baada ya kungoja kwa subira, Abra hamu alipata ahadi hiyo.
16 Watu huapa kwa mtu aliye mkuu kuliko wao, na kiapo hicho huthibitisha kinachosemwa na humaliza ubishi wote. 17 Kwa hiyo Mungu alipotaka kuwahakikishia warithi wa ahadi yake kuhusu maku sudi yake yasiyobadilika, aliwathibitishia kwa kiapo. 18 Mungu alifanya hivyo ili, kwa kutumia mambo haya mawili yasiyobadilika, na ambayo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tuliokimbilia usalama kwake tutiwe moyo, tushikilie kwa uthabiti tumaini lililowekwa mbele yetu.
19 Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho zetu yenye nguvu na imara. Tumaini hili linaingia hadi ndani ya pazia 20 ambamo Yesu ameingia akitutangulia; ameingia huko kwa niaba yetu. Yeye amekuwa kuhani mkuu milele, kama Melkizedeki.
Kuhusu Melkizedeki, Kuhani Mkuu
7 Huyu Melkizedeki alikuwa ni mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu aliye juu. Abrahamu alipokuwa akirudi kutoka vitani ambako aliua wafalme wengi, Melkizedeki alikutana naye, akambariki. 2 Abrahamu akampatia Melkizedeki sehemu ya kumi ya vitu vyote. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “Mfalme wa haki” na pia yeye ni “Mfalme wa Salemu,” maana yake, “Mfalme wa amani.”
3 Yeye hana baba wala mama wala ukoo; hana mwanzo wala hana mwisho, bali kama alivyo Mwana wa Mungu, yeye adumu kuwa kuhani milele.
4 Angalieni jinsi alivyo mkuu! Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. 5 Hata wana wa Lawi ambao ni makuhani, wameamriwa na sheria ya Mose kuwatoza Waisraeli ndugu zao, ambao ni wazao wa Abrahamu, sehemu ya kumi ya mapato yao. 6 Ingawa huyu Melkizedeki si wa ukoo wa Lawi, alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu , na akambariki huyu ambaye alikwisha pokea ahadi za Mungu. 7 Wala hakuna ubishi kuwa mtu mdogo hubarikiwa na mtu aliye mkuu kuliko yeye. 8 Kwa upande wa makuhani wa ukoo wa Lawi, sehemu ya kumi inapokelewa na binadamu ambao hufa; lakini kwa upande huu wa Melkizedeki, sehemu ya kumi inapokelewa na mtu ambaye tunahakikishiwa kuwa anaishi. 9 Mtu anaweza kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, 10 kwa maana Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado hajazaliwa. Mbegu yake ilikuwa bado iko mwilini mwa Abrahamu babu yake.
Yesu Na Melkizedeki
11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”
Melkizedeki.”
18 Sheria ya mwanzo imewekwa kando kwa kuwa ilikuwa dhaifu na tena haikufaa. 19 Kwa maana sheria haikufanya kitu cho chote kuwa kikamilifu, na sasa tumeletewa tumaini bora zaidi ambalo linatuwezesha kumkaribia Mungu.
20 Na tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wale waliofa nywa makuhani huko nyuma hapakuwepo kiapo. 21 Bali Yesu alipofa nywa kuhani aliwekewa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa wala hatabadili nia yake, ‘Wewe ni kuhani milele.”’
22 Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
23 Makuhani wa zamani walikuwa wengi kwa sababu kifo kiliwa zuia kuendelea daima na huduma yao. 24 Lakini yeye anaendelea na ukuhani wake daima kwa maana anaishi milele. 25 Kwa hiyo anaweza kwa wakati wote kuwaokoa wale wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye anaishi daima ili kuwaombea.
26 Huyu ndiye kuhani mkuu tunayemhitaji: yeye ni mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetenganishwa na wenye dhambi na aliyeinuliwa juu ya mbingu. 27 Yeye hahitaji kutoa dhabihu kila siku kwa ajili ya dhambi zake kwanza kisha dhambi za watu, kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu mara moja kwa wakati wote, alipojitoa mwenyewe. 28 Kwa maana sheria ya Mose huchagua watu wenye udhaifu kuwa makuhani wakuu. Lakini neno la Mungu la kile kiapo ambalo lilikuja baada ya sheria, lil imteua Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.
Kuhani Mkuu Wa Agano Jipya
8 Basi, katika hayo yote, tunalosema ni hili: tunaye huyo kuhani mkuu, ambaye ameketi upande wa kuume wa kiti cha Mwenyezi mbinguni. 2 Yeye ni mhudumu wa patakatifu katika ile hema ya kweli iliyowekwa na Bwana, na wala si na wanadamu.
3 Kila kuhani huteuliwa ili atoe sadaka na dhabihu, kwa hiyo ilikuwa muhimu kwamba huyu kuhani naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angalikuwa duniani asingalikuwa kuhani kwa sababu wapo makuhani wanaotoa sadaka kwa mujibu wa sheria ya Mose. 5 Wanahu dumu katika patakatifu iliyo mfano na kivuli cha ile iliyoko mbinguni. Ndio maana Mose alipokaribia kujenga ile hema takatifu aliamriwa na Mungu, akisema, “Hakikisha kuwa unafanya kila kitu kulingana na mfano ulioonyeshwa mlimani.” 6 Lakini Yesu amepewa huduma iliyo bora zaidi kuliko yao, kama vile lile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake, lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani. Agano hili jipya limejengwa juu ya ahadi bora zaidi.
7 Kama lile agano la kwanza lisingekuwa na upungufu, kusinge kuwapo na haja ya kuwa na agano jingine. 8 Lakini Mungu hakurid hika na watu wake, akasema, “Siku zinakuja, asema Bwana, nitaka pofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. 9 Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao siku ile nilipowashika mkono niwaongoze kutoka nchi ya Misri; kwa kuwa hawakuwa waaminifu kwa agano langu, nami nikawaacha, asema Bwana. 10 Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli siku zile zitakapowadia, asema Bwana: nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 11 Haitakuwapo haja tena kwao kumfundisha kila mtu mwenzake, au kila mtu ndugu yake, na kusema, ‘Mfahamu Bwana,’ kwa maana wote watanifahamu, tangu aliye mdogo kabisa hadi mkubwa kuliko wote. 12 Nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikum buka tena”.
13 Anapozungumza juu ya agano jipya Mungu anahesabu lile agano la kwanza kuwa limechakaa, na kitu kilichochakaa na kuzeeka kitatoweka baada ya muda mfupi.
Agano La Kwanza Na Agano Jipya
9 Basi hata lile agano la kwanza lilikuwa na kanuni zake za ibada pamoja na mahali pa kuabudia hapa duniani. 2 Hema la kuabu dia liliandaliwa likiwa na chumba cha kwanza ambamo mlikuwa na chombo cha kuwekea taa, na meza na mikate iliyowekwa wakfu. Chumba hiki kiliitwa Patakatifu. 3 Nyuma ya pazia la pili, pali kuwa na chumba kiitwacho Patakatifu pa Patakatifu. 4 Chumba hiki kilikuwa na madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba na sanduku la agano ambalo lilifunikwa kwa dhahabu pande zote. Sanduku hili lilikuwa na chombo cha dhahabu chenye ile mana na ile fimbo ya Aroni iliyochipuka, na yale mawe ya agano. 5 Juu ya sanduku kulikuwa na makerubi wa utukufu ambao kivuli chao kilifunika kiti cha rehema. Lakini mambo haya sasa hatuwezi kuyaeleza kwa undani.
6 Vitu vyote vilipokwisha kupangwa namna hii, makuhani wal iingia mara kwa mara katika kile chumba cha kwanza kutoa huduma yao ya ibada. 7 Lakini ni kuhani mkuu peke yake ambaye aliruhu siwa kuingia katika chumba cha ndani mara moja tu kwa mwaka. Tena ilibidi aingie huko na damu ambayo aliitoa kwa ajili yake mwe nyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda pasipo kujua. 8 Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa akionyesha kwamba maadamu hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa bado haijafunguliwa. 9 Hii ili kuwa ni kielelezo kwa wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizotolewa zilikuwa haziwezi kutakasa dhamiri ya mtu anayeabudu. 10 Hizi zilikuwa ni sheria zinazohusu chakula na vinywaji na taratibu mbalimbali za utakaso wa nje, kanuni ambazo zingetumika mpaka wakati wa matayarisho ya utaratibu mpya.
Damu Ya Kristo Husafisha Dhamiri
11 Kristo alipokuja kama kuhani mkuu wa mambo mema ambayo tayari yamekwisha wasili, alipitia kwenye hema ya kuabudia ambayo ni kuu zaidi na bora zaidi na ambayo haikujengwa na binadamu, yaani ambayo si sehemu ya ulimwengu huu ulioumbwa. 12 Yeye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa wakati wote, akichukua, si damu ya mbuzi na ndama, bali damu yake mwenyewe, na hivyo kutupatia ukombozi wa milele.
13 Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama hunyunyizwa juu ya watu wachafu kidini ikawatakasa kwa kuwaondolea uchafu wao wa nje, 14 damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia Mungu aliye hai.
15 Kwa sababu hii Kristo ni mjumbe wa agano jipya ili wale walioitwa wapokee urithi wa milele ulioahidiwa na Mungu; kwa kuwa alikufa awe fidia itakayowaweka huru na dhambi walizotenda chini ya agano la kwanza.
16 Ili hati ya urithi itambuliwe ni lazima pawepo na uthi bitisho kwamba huyo aliyeiandika amekwisha kufa. 17 Kwa maana hati ya urithi huwa na uzito tu wakati mtu amekwisha kufa; haiwezi kutumika wakati yule aliyeiandika angali hai. 18 Hii ndio maana hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu kumwagika. 19 Wakati Musa alipowatangazia watu amri zote za sheria, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo akanyunyizia kitabu cha sheria na watu wote, 20 akasema, “Hii ndio damu ya agano ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 21 Vivyo hivyo akanyunyizia damu hiyo kwe nye lile hema na vifaa vyote vilivyotumika kwa ibada. 22 Hakika katika sheria, karibu kila kitu hutakaswa kwa damu; na pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.
23 Kwa hiyo ilikuwa muhimu vitu hivi ambavyo ni mfano wa vile vya mbinguni vitakaswe kwa njia hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi. 24 Kwa maana Kristo hakuingia kwenye hema ya kuabudia iliyotengenezwa na bina damu kama mfano wa hema halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ambapo sasa anatuwakilisha mbele za Mungu. 25 Wala hakuingia mbinguni kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama kuhani mkuu ain giavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka na damu ambayo si yake. 26 Ingekuwa hivyo, ingalimpasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini ilivyo ni kwamba ametokea mara moja tu kwa wakati wote, katika siku hizi za mwisho, ili atokomeze dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. 27 Na kama ambavyo mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja tu, na baada ya hapo kukabili hukumu; 28 hali kadhalika Kristo alitolewa kama dhabihu mara moja tu ili azichukue dhambi za watu wengi; naye atakuja mara ya pili, si kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngojea kwa hamu.
Dhabihu Ya Kristo Ilikuwa Ya Mwisho
10 Basi kwa kuwa sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo na wala si mambo yenyewe, haiwezi kamwe, kwa njia ya dhabihu zito lewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaoabudu. 2 Kama isingekuwa hivyo, dhabihu hizo zingekuwa hazitolewi tena. Maana hao waabuduo wasingalijiona tena kuwa wana hatia kwa ajili ya dhambi zao baada ya kutakaswa mara moja. 3 Badala yake, dhabihu hizo zilikuwa ni ukumbusho wa dhambi mwaka hadi mwaka. 4 Kwa maana damu ya mafahali na mbuzi, haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
5 Kwa sababu hii, Yesu alipokuja duniani alisema: “Hukutaka dhabihu na sadaka bali umeniandalia mwili. 6 Hukupendezwa na sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi. 7 Ndipo nikasema, ‘Nipo hapa, kama ilivyoandikwa katika gombo la sheria kunihusu; nimekuja kutimiza mapenzi yako wewe Mungu.’ ”
8 Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi hukutaka, wala huku pendezwa nazo,” ingawa hizi zilitolewa kwa mujibu wa sheria. 9 Kisha akasema, “Niko hapa, nimekuja kutimiza mapenzi yako.” Anaweka kando ule utaratibu wa kwanza na kuanzisha utaratibu wa pili. 10 Na kwa mapenzi hayo, sisi tumetakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu, kwa wakati wote.
11 Kila kuhani husimama siku hadi siku akifanya huduma yake ya ibada na akitoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kuondoa dhambi. 12 Lakini Kristo alipokwisha kutoa dhabihu yake kwa ajili ya dhambi mara moja tu kwa wakati wote, aliketi upande wa kulia wa Mungu. 13 Tangu wakati huo anangoja mpaka Mungu atakapowafanya maadui zake kuwa kiti cha miguu yake. 14 Maana kwa dhabihu moja tu amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
15 Roho Mtakatifu pia anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: 16 “Hili ndilo agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao na kuziandika akilini mwao.” 17 Kisha anasema: “Dhambi zao na makosa yao sitayakumbuka tena kamwe.”
18 Basi, haya yakishasamehewa, hakuna tena dhabihu inayoto lewa kwa ajili ya dhambi.
Haja Ya Kuwa Imara
19 Kwa hiyo ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kupitia lile pazia, yaani kwa njia ya mwili wake, 21 na kwa kuwa tunaye kuhani mkuu anayemiliki nyumba ya Mungu; 22 basi tumkaribie Mungu kwa moyo wa kweli na imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya na miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi. 23 Tushikilie kwa makini tumaini tunalokiri kwa maana yeye ali yeahidi ni mwaminifu. 24 Na tujishughulishe kutafuta jinsi ya kuhimizana katika kuonyeshana upendo na kutenda mema. 25 Tusiache kukutana pamoja, kama wengine wanavyofanya, bali tutiane moyo, hasa zaidi tunapoona siku ile ikikaribia.
Hatari Ya Kukufuru
26 Kama tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kupokea na kufahamu ile kweli, hakuna tena dhabihu iliyobaki inayoweza kutolewa kwa ajili ya dhambi. 27 Kinachobakia ni kungojea kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza maadui zake. 28 Mtu aliyevunja sheria ya Mose aliuawa pasipo huruma kwa usha hidi wa watu wawili au watatu. 29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani zaidi anastahili kupewa mtu ambaye anamdharau na kum kataa Mwana wa Mungu, na ambaye anaona kuwa damu ya agano iliyom takasa si kitu, na ambaye amemtukana Roho wa neema? 30 Kwa maana tunamjua yeye aliyesema, “Kulipiza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipiza.” Pia alisema, “Bwana atawahukumu watu wake.” 31 Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha.
32 Kumbuka siku zile za mwanzo baada ya kupokea mwanga, jinsi mlivyovumilia mapambano makali na mateso. 33 Wakati mwin gine mlitukanwa na kuteswa hadharani; wakati mwingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa hivyo. 34 Mliwaonea huruma waliokuwa kifungoni, na mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu kwa maana mlifahamu kwamba mlikuwa na mali bora zaidi inay odumu.
35 Kwa hiyo msitupe tumaini lenu, ambalo litapewa tuzo kubwa. 36 Mnahitaji kuvumilia ili mkisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi. 37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu yeye anayekuja atakuja , wala hatakawia; 38 lakini mtu wangu mwenye haki ataishi kwa imani, na akirudi nyuma sitapendezwa naye.”
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaorudi nyuma wakaangamizwa, bali sisi ni miongoni mwa wanaoamini wakaokolewa.
Imani
11 Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni uhakika wa mambo tusiyoyaona. 2 Maana ni kwa imani wazee wa kale walipata kibali cha Mungu.
3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vinavyoonekana vilitengenezwa kutokana na vitu visiv yoonekana.
4 Kwa imani Abeli alimtolea Mungu sadaka bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alikubaliwa kuwa mtu mwenye haki, Mungu aliposi fia sadaka zake. Na kwa imani yake bado anasema ingawa amekufa.
5 Kwa imani, Enoki alichukuliwa mbinguni ili asife, hakuone kana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Basi, kabla haja chukuliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu. 6 Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa bidii.
7 Kwa imani Noe alipoonywa na Mungu kuhusu mambo yaliyokuwa hayajaonekana bado, alitii akajenga safina kuokoa jamii yake. Kwa sababu hii aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatika nayo kwa imani.
8 Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende kwenye nchi ambayo Mungu angempa kama urithi. Naye aliondoka akaenda ingawa hakujua aendako. 9 Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi ya ahadi. Aliishi katika nchi ya ugenini katika mahema pamoja na Isaki na Yakobo ambao pia walikuwa warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akitazamia mji wenye misingi ya kudumu ambao umebuniwa na kujengwa na Mungu mwenyewe.
11 Kwa imani Sara alipewa uwezo wa kupata mimba ijapokuwa alishapita umri wa kuzaa, kwa sababu aliamini kwamba Mungu ali yemwahidi ni mwaminifu na angelitimiza ahadi yake. 12 Kwa hiyo kutokana na huyu mtu mmoja, ambaye alikuwa sawa na mfu, walizal iwa wazao wengi kama nyota za mbinguni na kama mchanga usiohesa bika wa pwani.
13 Watu wote hawa walikuwa bado wanaishi kwa imani walipo kufa. Hawakupata yale waliyoahidiwa; lakini waliyaona na kuyafu rahia kwa mbali. Nao walikiri kwamba walikuwa ni wageni wasiokuwa na maskani hapa duniani. 14 Maana watu wanaosema maneno kama hayo, wanaonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Kama walikuwa wakifikiria kuhusu nchi waliyoiacha, wangali pata nafasi ya kurudi huko. 16 Lakini sasa wanatamani nchi iliyo bora zaidi, yaani, nchi ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa maana amewatayarishia mji.
17 Kwa imani Abrahamu alipojaribiwa alimtoa Isaki awe dha bihu. Yeye ambaye alikuwa amepokea ahadi za Mungu alikuwa tayari kumtoa mwanae wa pekee awe dhabihu, 18 ingawa Mungu alikuwa amemwambia, “Uzao wako utatokana na Isaki.” 19 Abrahamu aliamini kwamba Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu, na kweli ni kama alimpata tena Isaka kutoka katika kifo.
20 Kwa imani Isaki aliwabariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yatakayotokea baadaye.
21 Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea kichwa cha ile fimbo yake.
22 Kwa imani Yosefu alipokuwa amekaribia mwisho wa maisha yake, alitaja habari za kutoka kwa wana wa Israeli huko Misri, na akatoa maagizo kuhusu mifupa yake.
23 Kwa imani Mose alipozaliwa alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mwenye umbo zuri, wala hawakuogopa amri ya mfalme.
24 Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao, 25 badala yake akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu, kuliko kufurahia anasa za dhambi za kitambo kidogo. 26 Aliona kwamba kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni uta jiri mkubwa zaidi kuliko hazina ya Misri; maana alikuwa anataza mia kupata tuzo baadaye. 27 Kwa imani Mose alitoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme, kwa maana alivumilia kama amwonaye yeye asiyeonekana. 28 Kwa imani aliitimiza Pasaka na kunyunyiza damu ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.
29 Kwa imani watu wakavuka Bahari ya Shamu kama vile juu ya nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo, wakafa maji.
30 Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka, watu walipozizunguka kwa siku saba.
31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi.
32 Basi niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kuwaeleza habari za Gidioni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii. 33 Hawa, kwa imani walishinda milki za wafalme, walite keleza haki, walipokea ahadi za Mungu, walifunga vinywa vya simba; 34 walizima moto mkali, na waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini wakatiwa nguvu, walikuwa hodari vitani, wakafukuza majeshi ya kigeni yakakimbia. 35 Wanawake walipokea wapendwa wao waliokuwa wamekufa wakafufuliwa. Lakini wengine wal iteswa wakakataa kufunguliwa, ili wapate kufufukia maisha bora zaidi. 36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata wakafungwa pingu na kutiwa gerezani. 37 Walipigwa mawe, walikatwa vipande viwili kwa misumeno, waliuawa kwa panga, walizurura wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, walikuwa maskini, waliteswa na kutendewa mabaya. 38 Ulimwengu haukustahili kuwa na watu kama hao: walizungukazunguka jangwani, katika milima na katika mapango na mashimo ardhini.
39 Na wote hawa, ingawa walishuhudiwa vema kwa sababu ya imani yao, hawakupokea yale waliyoahidiwa, 40 kwa sababu Mungu alikuwa amepanga kitu bora zaidi kwa ajili yetu, kwamba wasinge likamilishwa pasipo sisi.
Tuige Mfano Wa Yesu
12 Basi na sisi kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi inay otusonga kwa urahisi; tupige mbio kwa ustahimilivu katika mashin dano yaliyowekwa mbele yetu. 2 Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu. Yeye, kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, alivumilia kifo cha msalaba bila kujali aibu, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Mtafakarini yeye aliyestahimili uadui wa namna hii kutoka kwa wenye dhambi; msije mkachoka wala kufa moyo. 4 Katika kushin dana kwenu na dhambi, bado hamjapigana na majaribu kiasi cha kufikia hatua ya kumwaga damu yenu. 5 Je, mmekwisha sahau yale maneno ya kuwatia moyo, yanayowataja kama wana? “Mwanangu, usid harau nidhamu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya. 6 Maana Bwana huwaadhibu wale awapendao na humpiga kila anayemkubali kuwa ni mwanae.”
7 Vumilieni mateso kama mafunzo. Mungu anawatendea kama wanawe. Maana ni mwana yupi asiyeadhibiwa na baba yake? 8 Kama mtaachiwa bila kuwa na nidhamu, na kila mtu hufundishwa kuwa na nidhamu, basi ninyi ni wana haramu, si wanawe wa halali. 9 Zaidi ya hayo, baba zetu waliotuzaa walituadhibu nasi tukawaheshimu kwa ajili hiyo. Je, si inatupasa kujinyenyekeza zaidi kwa baba wa roho zetu ili tuishi? 10 Baba zetu wa hapa duniani walituadhibu kwa muda mfupi kama wao wenyewe walivyoona kwamba inafaa. Lakini Mungu anatuadhibu kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11 Adhabu yo yote huonekana kuwa kitu cha kuumiza na kisichofu rahisha wakati ule inapotolewa. Lakini baadaye, matunda yake kwa wale waliofundishwa kwa nidhamu hiyo, ni haki na amani.
12 Kwa hiyo imarisheni mikono yenu iliyolegea na magoti yenu yaliyo dhaifu. 13 Nyosheni njia za miguu yenu ili mguu ulioumia usilemae, bali upone.
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na utaka tifu, ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana. 15 Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu, na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua ikaleta matatizo na kuwachafua wengi. 16 Hakik isheni kwamba miongoni mwenu hamna mwasherati au mtu asiyemcha Mungu. Kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja, aliuza haki yake ya kuwa mzaliwa wa kwanza. 17 Maana mnafahamu ya kwamba baadaye, alipotaka kurithi ile baraka aliyokuwa apewe, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.
18 Hamkuja kukaribia mlima ambao unaweza kuguswa, na ambao unawaka moto; wala hamkuja kwenye giza, huzuni na dhoruba, 19 na mlio wa tarumbeta na sauti ikisema maneno kwa kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno lingine zaidi. 20 Kwa maana hawakuweza kustahimili amri iliyotolewa: “Kama hata mnyama atag usa mlima huu, atapigwa mawe.” 21 Kwa hakika waliyoona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” 22 Lakini ninyi mmekuja kwenye Mlima wa Sioni, na kwenye mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni, ambapo wamekusanyika kwa shangwe maelfu na maelfu ya malaika. 23 Mmefika kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu ambao majina yao yameandikwa mbin guni. Mmekuja mbele ya Mungu, hakimu wa watu wote, na mbele ya roho za watu wenye haki, waliofanywa wakamilifu. 24 Mmefika kwa Yesu, msuluhishi wa agano jipya, na kwa damu ile iliyonyunyizwa, inenayo maneno mema kuliko damu ya Abeli.
25 Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa hawa kuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi tutaepukaje tukimkataa yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 26 Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”
27 Maneno haya, “Kwa mara moja tena,” yanaonyesha kwamba vile vinavyotetemeshwa vitaondolewa, yaani vyote vilivyoumbwa, kusudi vibaki vile tu visivyoweza kutetemeshwa.
28 Kwa hiyo, tuwe na shukrani kwa kuwa tumepokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna itakay ompendeza, kwa unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto unaoteketeza.
Mwenendo Wa Mkristo
13 Endeleeni kupendana kama ndugu. 2 Msiache kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivyo watu wengine waliwakaribisha mal aika pasipo kujua. 3 Wakumbukeni waliofungwa gerezani kama vile mmefungwa pamoja nao; pia wakumbukeni wanaoteswa, kwa kuwa na ninyi bado mnaishi katika mwili.
4 Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.
5 Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia kamwe wala sitakuacha.” 6 Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu, sitaogopa kitu, mwanadamu anaweza kunifanya nini?”
7 Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Tafakarini jinsi walivyoishi na matokeo ya mwenendo wao, mkaige imani yao. 8 Yesu Kristo ni yule yule, jana, leo na hata milele. 9 Msipotoshwe na mafundisho ya kigeni ya namna mbalimbali. Ni vema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, na wala si kwa kutii mash arti kuhusu vyakula, ambavyo havina faida kwa wanaovila. 10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema ya kuabudia hawana haki ya kula vitu vilivyowekwa juu yake.
11 Nyama za hao wanyama ambao damu yao huletwa na kuhani mkuu katika Patakatifu pa Patakatifu kama dhabihu ya dhambi, huchomwa nje ya kambi. 12 Kwa hiyo Yesu naye aliteswa nje ya mlango wa mji ili awatakase watu kwa damu yake. 13 Kwa hiyo tum wendee nje ya kambi, tukashiriki aibu aliyostahimili. 14 Maana hapa hatuna mji wa kudumu, bali tunautafuta ule mji ujao.
15 Basi, kwa njia ya Yesu, tuendelee kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo ya watu wanaokiri jina lake. 16 Msiache kutenda mema na kushirikiana mlivyo navyo, kwa maana sadaka kama hizi ndizo zinazompendeza Mungu.
17 Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.
18 Tuombeeni, kwa maana tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi na tunapenda kufanya yaliyo sawa daima. 19 Ninawasihi zaidi mniombee ili nirudishwe kwenu upesi zaidi.
Sala
20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, 21 awape ninyi kila kitu chema, ili mpate kutimiza mapenzi yake akifanya ndani yenu lile linalopendeza machoni pake, kwa njia ya Yesu Kristo; yeye apewe utukufu milele na milele.
Maneno Ya Mwisho
22 Basi, ndugu zangu, nawasihi mpokee vema maonyo haya, maana nimewaandikia kwa ufupi.
23 Napenda kuwafahamisha kwamba ndugu yetu Timotheo amefun guliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja naye kuwaona.
24 Wasalimuni viongozi wenu wote pamoja na watu wote wa Mungu. Salamu zenu kutoka kwa ndugu wa Italia.
1 Kutoka kwa Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo. Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni. Salamu:
Imani Na Hekima
2 Ndugu wapendwa, mnapopatwa na majaribu mbalimbali, yahesab uni kuwa ni furaha tupu. 3 Kwa maana mnafahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu hujenga ustahimilivu. 4 Na ustahimilivu ukimaliza kazi yake mtakuwa wakamilifu pasipo kupungukiwa na cho chote.
5 Lakini kama mtu ye yote kati yenu akipungukiwa na hekima, basi na amwombe Mungu, ambaye huwapa watu wote kwa ukarimu pasipo kulaumu, naye atapewa. 6 Lakini aombe kwa imani pasipo shaka yo yote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari ambalo husu kumwa na upepo, likitupwa huku na huku. 7 Mtu kama huyo asidhani atapata kitu cho chote kutoka kwa Bwana; 8 kwa maana yeye ni mtu mwenye nia mbili asiyekuwa na msimamo katika jambo lo lote.
Umaskini Na Utajiri
9 Ndugu asiye na cheo afurahi kwa sababu Bwana amemtukuza; 10 na tajiri afurahi anaposhushwa kwa maana atatoweka kama ua la mwituni. 11 Maana jua huchomoza na kwa mionzi yake mikali hukausha mimea, na maua yake huanguka na uzuri wake hupotea. Vivyo hivyo tajiri naye atafifia akiwa katika shughuli zake.
Kujaribiwa
12 Amebarikiwa mtu ambaye anavumilia majaribu, kwa sababu akisha stahimili atapewa taji ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao. 13 Mtu akijaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu,” kwa maana Mungu hajaribiwi na uovu na yeye hamjaribu mtu ye yote. 14 Lakini kila mtu hujaribiwa anapovutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe. 15 Kisha tamaa hiyo ikisha chukua mimba, huzaa dhambi; na dhambi ikisha komaa, huzaa mauti.
16 Ndugu zangu wapendwa, msidanganywe. 17 Kila kipawa chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni, ikishuka kutoka kwa Baba wa nuru za mbinguni ambaye habadiliki kama kivuli. 18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mavuno ya kwanza katika viumbe vyake.
Kusikia Na Kutenda
19 Ndugu wapendwa, fahamuni jambo hili: kila mtu awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema wala kukasirika. 20 Maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. 21 Kwa hiyo epukeni uchafu wote na uovu ambao umeenea, mkapokee kwa unyenyekevu lile neno lililopandwa mioyoni mwenu ambalo linaweza kuokoa nafsi zenu.
22 Basi muwe watendaji wa neno na wala msiwe wasikilizaji tu, ambao wanajidanganya wenyewe. 23 Kwa maana kama mtu ni msi kilizaji tu wa neno na wala hatekelezi alilosikia, atafanana na mtu ajitazamaye uso wake katika kioo, 24 na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara moja husahau anavyofanana. 25 Lakini mtu anayeangalia kwa makini katika sheria kamilifu, ile sheria iletayo uhuru, na akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosi kia, bali akakitekeleza, atabarikiwa katika kile anachofanya.
26 Mtu akidhani kuwa ana dini na huku hautawali ulimi wake, anajidanganya mwenyewe na dini yake ni bure. 27 Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii: kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu.
Onyo Kuhusu Upendeleo
2 Ndugu zangu wapendwa, msiwe na upendeleo mnapoishika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu. 2 Tuseme mtu mmoja aliyevaa pete ya dhahabu na nguo maridadi anakuja katika mkutano wenu; kisha fukara mmoja mwenye nguo chafu na mbovu akaingia pia. 3 Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,” 4 je, hamtakuwa mmefanya ubaguzi mioyoni mwenu na kutoa hukumu itokanayo na mawazo maovu?
5 Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa: je, Mungu hakuwachagua wale walio fukara hapa duniani kuwa matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidi wale wampendao? 6 Lakini ninyi mmemvunjia heshima aliye fukara. Je, si matajiri ndio wanaowagandamiza na kuwapelekeni mahakamani? 7 Je, si wao wanaolikufuru jina lile jema mliloitiwa? 8 Kama kweli mnatimiza ile sheria ya kifalme iliyomo katika Maandiko, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe,” mnafanya vema. 9 Lakini kama mnafanya ubaguzi, mna tenda dhambi na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10 Kwa maana mtu ye yote anayetimiza sheria yote isipokuwa akashindwa kutimiza sehemu moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote. 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini” ndiye huyo huyo aliyesema, “Usiue.” Kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria yote.
12 Kwa hiyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. 13 Maana hukumu haina huruma kwa mtu asi yekuwa na huruma. Lakini huruma huishinda hukumu.
Imani Na Matendo
14 Kuna faida gani, ndugu zangu, ikiwa mtu atasema, “Ninayo imani,” na huku hana matendo? 15 Tuseme ndugu fulani au dada hana nguo wala chakula. 16 Ikiwa mmoja wenu atawaambia, “Nendeni salama, mkaote moto na kushiba,” pasipo kuwapatia mahitaji yao ya mwili, kuna faida gani? 17 Vivyo hivyo imani peke yake kama haina matendo, imekufa.
18 Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nita kuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. 19 Unaamini kuwa kuna Mungu mmoja. Vema. Lakini hata mashetani huamini hivyo, nao hutetemeka!
20 Ewe mpumbavu, unataka ushahidi wa kuthibitisha kwamba imani bila matendo ni bure? 21 Je, Abrahamu baba yetu hakuhesa biwa haki kwa matendo, alipomtoa mwanae Isaki madhabahuni? 22 Unaona jinsi ambavyo imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake na imani ikakamilishwa kwa matendo. 23 Kwa njia hiyo yaka timizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akahesabiwa kuwa mtu mwenye haki”; naye akaitwa rafiki wa Mungu.
24 Mnaona kwamba mtu huhesabiwa haki kwa matendo wala si kwa imani peke yake. 25 Hali kadhalika Rahabu, yule kahaba, yeye je, hakuhesabiwa haki kwa matendo yake alipowapokea wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? 26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika imani pasipo matendo imekufa.
Kuhusu Kuutawala Ulimi
3 Ndugu zangu, wengi wenu msiwe walimu, kwa maana mnafahamu kwamba sisi tufundishao tutahukumiwa vikali zaidi. 2 Sisi sote hufanya makosa mengi. Ikiwa kuna mtu asiyekosea kwa usemi wake, huyo ni mkamilifu, naye anaweza kuutawala mwili wake wote.
3 Tunapowawekea farasi lijamu vinywani mwao ili watutii, tunatawala miili yao yote. 4 Kadhalika meli, ingawa ni kubwa sana na huendeshwa na upepo mkali, lakini huongozwa na usukani mdogo sana, ikaenda ko kote anakotaka nahodha. 5 Ulimi nao ni kiungo kidogo sana lakini hujivunia mambo makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! 6 Ulimi pia ni kama moto. Ulimi ni ulimwengu wa uovu kati ya viungo vyetu. Humchafua mtu nafsi nzima na kuwasha moto maisha yake yote, nao ulimi huwashwa moto wa kuzimu. 7 Wanyama wa kila aina, ndege, nyoka na viumbe vya baharini wanafugwa na wamekwisha kufugwa na binadamu. 8 Lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu unaohangaika huku na kule, uliojaa sumu inayoua.
9 Kwa kutumia ulimi tunamsifu Bwana na Baba yetu na kwa ulimi huo huo tunawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa hicho hicho hutoka sifa na laana. Ndugu zangu, haipaswi kuwa hivyo. 11 Je, chemchemi yaweza kutoa kutoka katika tundu moja maji matamu na maji machungu? 12 Je, ndugu zangu, mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu waweza kuzaa tini? Pia haiwezekani chemchemi ya chumvi kutoa maji matamu.
Copyright © 1989 by Biblica