Paulo na Barnaba wakayapinga mafundisho haya na wakahojiana na kubishana na watu hawa juu ya hili. Hivyo kundi la waamini likaamua kuwatuma Paulo, Barnaba, na baadhi ya watu wengine Yerusalemu ili kujadiliana na mitume na wazee kuhusu suala hili.
Paulo na Barnaba walikuwa na mabishano makali nao wakipinga mafundisho haya. Ikaamuliwa kwamba Paulo na Barnaba na waamini wengine waende Yerusalemu wakawaulize mitume na wazee juu ya jambo hili.