Baada ya watu kuleta mtumbwi wa kuokolea, wakaifunga meli kamba kuizungushia ili iendelee kushikamana isipasuke. Waliogopa kwamba meli ingekwama kwenye mchanga wa pwani ya Sirti. Hivyo walishusha tanga na kuiacha meli ichukuliwe na upepo.
Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee.