Mnaweza kuwa na uhakika wa hili: Hakuna atakayepata sehemu katika ufalme wa Kristo na wa Mungu kama mtu huyo atakuwa anafanya dhambi ya uzinzi, au akitenda mambo maovu, au kama atakuwa mtu wa kutamani vitu zaidi na zaidi. Mtu mwenye choyo kama huyo atakuwa anamtumikia mungu wa uongo.
Mjue hakika kwamba hakuna mwasherati wala mtu mwenye mawazo machafu, wala mwenye tamaa, yaani mwabudu sanamu, ambaye ataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu.