Sheria huchagua makuhani wakuu ambao ni watu na wanao udhaifu ule ule ambao watu wote wanao. Lakini baada ya sheria, Mungu alisema kiapo ambacho kilimfanya Mwana awe kuhani mkuu. Na Mwana huyo, aliyekamilishwa kwa njia ya mateso, atatumika kama kuhani mkuu milele yote.
Kwa maana sheria ya Mose huchagua watu wenye udhaifu kuwa makuhani wakuu. Lakini neno la Mungu la kile kiapo ambalo lilikuja baada ya sheria, lil imteua Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.