Makuhani hawa hupata sehemu ya kumi, lakini wao ni binadamu tu wanaoishi kisha hufa. Lakini Melkizedeki, aliyepata sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu, anaendelea kuishi, kama Maandiko yanavyosema.
Kwa upande wa makuhani wa ukoo wa Lawi, sehemu ya kumi inapokelewa na binadamu ambao hufa; lakini kwa upande huu wa Melkizedeki, sehemu ya kumi inapokelewa na mtu ambaye tunahakikishiwa kuwa anaishi.