Lakini kazi ambayo tayari imetolewa kwa Yesu ni kuu zaidi ya kazi iliyotolewa na makuhani hao. Kwa jinsi hiyo hiyo, agano jipya ambalo Yesu alilileta kutoka kwa Mungu kuja kwa watu wake ni kuu zaidi kuliko lile la zamani. Na agano jipya limeelemea katika ahadi bora zaidi.
Lakini Yesu amepewa huduma iliyo bora zaidi kuliko yao, kama vile lile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake, lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani. Agano hili jipya limejengwa juu ya ahadi bora zaidi.