Na tuchukulie kuwa mnaonyesha kumjali zaidi yule mtu aliyevaa mavazi mazuri na kusema, “Wewe keti hapa katika kiti hiki kizuri.” Lakini unamwambia yule mtu maskini, “Wewe simama pale,” au, “Keti chini karibu na miguu yetu.”
Ikiwa utamshughulikia zaidi yule mtu aliyevaa nguo maridadi ukamwambia, “Keti hapa kwenye kiti kizuri,” lakini yule fukara ukamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti sakafuni, miguuni pangu,”