Akamwuliza, “Mwanamke, kwa nini unalia? Je, unamtafuta nani?” Yeye alifikiri kuwa huyu alikuwa ni mtunzaji wa bustani. Hivyo akamwambia, “Je, ulimwondoa Bwana? Niambie umemweka wapi. Nami nitaenda kumchukua.”
Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.”