Simoni Petro akaenda kwenye mashua na kuvuta wavu kuelekea ufukweni. Wavu huo ulikuwa umejaa samaki wakubwa, wapatao 153 kwa ujumla! Lakini pamoja na wingi wa samaki hao, nyavu hazikukatika.
Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.