Yesu akasema, “Tupeni nyavu zenu kwenye maji upande wa kulia wa mashua yenu. Nanyi mtapata samaki huko.” Nao wakafanya hivyo. Wakapata samaki wengi kiasi cha kushindwa kuzivuta nyavu na kuziingiza katika mashua.
Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua!