Maelfu wengi wa watu walikusanyika. Walikuwepo watu wengi sana kiasi ambacho walikuwa wakikanyagana. Kabla Yesu hajaanza kuzungumza na watu wale, aliwaambia wafuasi wake, “Iweni waangalifu dhidi ya chachu ya Mafarisayo. Ninamaanisha kuwa hao ni wanafiki.
Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.