Kwa mara nyingine tena Petro alikataa. Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesimama pale wakarudia tena kumwambia Petro, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa sababu wewe pia ni Mgalilaya.”
Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!”